MIELEKA... (Don`t try this at home!)

MIELEKA... (Don`t try this at home!)

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,199
Reaction score
8,761
Swali langu wana JF ni juu ya huu mchezo hatari wa MIELEKA (wrestling), ambayo tunaiona kwenye TVs ikichezwa na mabaunsa wa huko majuu.
Je kwanini watu wale hawaumii, kutokwa damu au kufa kabisa, maana nionavyo mimi upiganaji ule ni wa MAUAJI, au labda kuna aina fulani ya USANII wa computer unatundikwa pale ili tu kuwaburudisha watazamaji? May you solve this querry for me.
 
Its entertainment so they are acting, though sometimes they get hurt in the process even losing their life.
 
Mie nafikiri zimegawanyika katika sehemu mbili. Kuna usanii na ukweli ndani yake.

Ukiangalia huu mchezo ni sawa na mapigano kama K-1. Huko utawakuta akina Badr Hari, Remmy Bonjasky, Musashi, Karayev nk ambao unaweza kuona wanapigana bila kuumia. Katika michezo yote miwili, jambo muhimu wanalojifunza ni UVUMILIVU wa maumivu. Wanakuwa ni watu waliopa mafunzo makali ya kupokea KIPIGO CHA MBWA na bado unaona jamaa anakuja tu. Ndiyo maana hadi ufaulu kuingia kupigana kwenye K-1, basi wee kweli unaweza kupokea kipigo na kugawa kipigo. Mapigano ya K-1 waweza yaona hata kwenye YOUTUBE.

Kitendo cha kurushwa na kuangukia Kichwa, au kupigwa na kiti hadi kinavunjika, kweli Usanii upo ila na MSULI lazima uwepo.
 
Kama ukifanikiwa kupata mkanda wa mieleka jaribu kuangalia slow-motion kuona wanavobadilishana vipigo. Utakuta hakuna kupiga ngumi unapiga kwa kutumia nyuma sa kiwiko, na pia hata kumkaba mtu inakuwa ktk hesabu maalumu. Ila mara nyingine mzuka unapanda na wanaumizana kisawasawa.
Kuna acting ndani yake na uhalisia ila wako well trained kwa hilo si kila mtu anaweza kuingia kupigana kule tu ndo maana kila mmoja anakuja aina yake ya mapigo au hata silaha anayotumia. Mtu asiseme usanii wa kompyuta maana sidhani kama wale audience nao ni computer generated pixs au ni watazamaji wa show ya kurekodi mieleka....
 
Mie nafikiri zimegawanyika katika sehemu mbili. Kuna usanii

...Yes, the outcomes are almost (if not) always predetermined. There is a storyline in these so called wrestling matches. It's not even called wrestling. It is sports entertainment

na ukweli ndani yake.
Ukweli being the athleticism showcased by the participants.

So no matter how you slice and dice it, it is still fake because of the predetermined outcomes.
 
Wrestling ni FAKE sana, siyo TNA-Total non stop action au WWE, ambaoko kuna makundi kama ECW mimi ni mpenzi sana wa huu mchezo na nimefanya mazoezi nikifikiri siku moja nitacheza hamna kitu, every thing is acting hata audience wanatengenezwa studio kama ungefanikiwa kushiriki live performance ungeamini ni tofauti sana, au je uliwahi kuona live match? zile zinatengenezwa miezi miwili iliyopita kwa mfano tu WRESTLEMANIA TZ mnaonyeshwaga April au begining of May in USA zinachezwa the end of Febr. na na kuonyeshwa the end of March. Kipindi cha kina Hulk Organ kidogo ilikuwa afadhali sasa ni too artificial. Some moves ni kweli na ndio maana watu wanakufa jukwaani. Anavyo ruka Jeff Hard Ni kweli kbs ila Damu kutoka viti kupigana navyo zote ni Fiksi.
 
Wrestling ni feki kama zilivyo movie....
 
Kaka inaonekana we si mfuatiliaji wa kitambo, watu wanaumia mpaka damu na watu wanavunjika miguu na mikono hata shingo, mfano john sina, tipple h na wengine wengi shawn michael aliumia sana jicho...mchezo ulio na ukweli so dont try to your lovely one
 
Nafikiri unahitaji kusoma na kuuelewa huu mchezo, mtu akienda likizo huo wanatengeneza kisingizio kwamba ameumia na huwa hastep kwenye ring for six month...hata kwenye olimpiki hauruhusiwi iko ile ya West Africa ya kuangushana pamoja sumo
 
NN,

Huo mchezo kweli kuna USANII ila si FEKI kama mnavyotaka kuuonyesha. Kwangu mie ni sawa na kuangalia film na hapo unasema ahh ni feki. Ukiangalia wakati wanatengeneza, utaona HATARI inayokuwa inawakabili. Tumeshaona waliopoteza maisha (Bruce Lee Son), kuumia, kuvunjika nk. Sasa sijui unaposema FEKI una maanisha nini.

Unajua unaweza kusema hata ule Mchezo wa kufukuzwa na ng'ombe pale Spain nao ni Feki. Mashindano ya kukaa kwenye mgongo wa Bull/farasi kichaa huku akikurusha, nao ni feki, na michezo mingine kibao. Kila mchezo una masharti yake. Kwa mwingine unaweza kuona FEKI. Mie siwezi kuita hivyo kwani hawa watu hujiandaa vilivyo kabla hawajaingia hapo ulingoni. Mke wangu yeye anasema:-
MASHINDANO YOTE HUWA NI FEKI.

1. Mpira wa miguu, ngumi, mieleka, mpira wa kikapu, nk huwa ni feki na kupanga matokeo tangu siku nyingi. Au huamini? Hebu jikumbushe tukio la kununua mechi katika ligi ya Italy.

2. Dopping, hufanya ushindani uwe feki kwani mwingine anatumia nyenzo.

3. Uchaguzi Tanzania, Kenya, Uganda nk huwa ni feki kwani nako watu hununua kura.

4. Hebu ongeza mwenyewe........

5. Makalio ya akina mama Feki (Lola Love), Matiti feki, hips feki, bikira feki, miili ya wanaume feki (madawa ya kukuza mwili) na hii hadi "ukubwa wa jogoo feki", nk nk,

Sasa tukishasema hivyo, kipi ni GENUINE???
 
Sasa tukishasema hivyo, kipi ni GENUINE???

Katika dunia ya leo ni vitu vichache sana vilivyo genuine. Siku hizi, kwa mfano, kuna kila aina ya cosmetic surgeries kuanzia penile enlargement, breast enhancement, hadi face transplants.
 
Katika dunia ya leo ni vitu vichache sana vilivyo genuine. Siku hizi, kwa mfano, kuna kila aina ya cosmetic surgeries kuanzia penile enlargement, breast enhancement, hadi face transplants.

Hapa sasa naona tunaongea lugha moja. Ila ukienda kuangalia picha au unapoazima film na kuangalia si inakuwa kwamba unakubali mtu mzima udanganywe? Hizi film si ni sawa na bibi yangu enzi hizo akitupa simulizi wakati wa jioni kwa kuanza na maneno kama "hadithi hadithi /Kali kakawuka.............hapo zamani za kale......"

Ila uishi dunia ya leo, lazima ukubali udanganywe. Ukisema sitaki kudanganywa basi itabidi sijui ukaishi wapi. Kila kitu ni feki. Nasikia Wasomali hawataki kudanganywa na Wanasiasa, matokeo yake hadi leo hawana nchi. Haya jamani ili dunia iende basi lazima tukubali tudanganywe. Kikwete ana theory yake anayosema "UKITAKA KULA BASI LAZIMA UKUBALI NA WEWE ULIWE KIDOGO>>>"
 
Hehehehehee...hasa majuu ndiko kuna udanganyifu (maybe wala sio udanganyifu kwa sababu wanakwambia kabisa) wa hali ya juu. Sio kila kitu mnachokula majuu ni cha kweli. Mmewahi kusikia imitation steak au imitation crab meat?
 
Marehemu sister alikuwa akitupa hela ya mkate asubuhi na siagi/blue band na yeye huomba achemshiwe Mihogo au viazi vitamu kwa ajili ya kifungua kinywa. Kama hamna basi ataomba kiporo cha wali wa jana. Mkate akawa hali kabisa. Nilipokuja kusikia wanavyochanganya unga wa ngano kwa kutumia mig.........., Mungu bariki siku hizi wanatumia mashine.

Nilipoenda kusoma nchi za watu nikapata habari kuwa sausage huwekwa vitu kama nywele za watu, na takataka nyingine, mikuku hulishwa dawa za kuzuia mimba za akina mama, USA ng'ombe wanapewa sijui dawa gani ili kutoa maziwa mengi, Cocacola inakwangua kila kitu, ..............grrrrrrrrrr.

Naona nikikalie tu huku Sikonge maana najitahidi sana kutumia vyakula ninavyolima mwenyewe. Kuku wa kienyeji (siyo wale wa Zeutamu), nyama, mazima, nk viko karibu na nature. Mara moja moja twaenda kuvua makambale (ninapenda kuwakunja).

Nyie mnaofaidi huko majuu, mfaidi tu vingi. Ni kama ile alama ya 666 vile. Kuwa hutaweza kuuza au kununua kama huna alama. Kwa kwel sasa hivi au unaingia kwenye uongo au uache kuishi.

Kweli nilishasikia coffee like, sugar like, meet like, girl lile, men like, juice like (hii wanasema periodic table yote iko pale), beer like, wine like, oxygen like, cotton like, wife like, husband like..... sasa nasikia Wajapan wanatengeneza robot awe kama binadamu. Mambo mswano.
 
Jamani mbona mmehama kwenye swali, Swali alilouliza ni la maana nasi pia tungependa kujua, anayefahamu tafadhali tujulishe
 
Jamani mbona mmehama kwenye swali, Swali alilouliza ni la maana nasi pia tungependa kujua, anayefahamu tafadhali tujulishe

Ukweli umeandikwa na mifano kibao kuwekwa. Sasa yaliyobaki ni kwako kuamua kuwa huu mchezo ni FEKI au siyo FEKI. Ukweli unabaki palepale kwamba hata kama ni FEKI, kwa mtu wa kawaida ni hatari sana kuufanya nyumbani kwani hawa jamaa wanakuwa wanafanya mazoezi ya muda mrefu hadi wanakuwa wavumilivu wa maumivu na Actor wazuri sana.

Unachouliza wewe ni sawa na swali kuwa Drogba kakosa goli, je amekosa kikweli au kajikosesha kwani alipewa pesa? Kwa watu wazoefu kama hao, kitu chochote chawezekana na huwezi kusema alifanya kwa makusudi kwani atakujibu yeye ni binadamu na anaweza kukosea. Dawa ni pale tu utakapomkamata anachukua pesa.

Hawa jamaa pia huumia na hata kufa ndani ya mieleka. Sasa hiyo unaweza sea bahati mbaya tu na mwingine akasema ni kweli wanapigana.

Ila kwa dunia ya leo, KIPI NI CHA KWELI UNATAKA KUJUA NDUGU YANGU?
Tafuta sana labda siku moja utapata Mchezo wa kweli.
 
Back
Top Bottom