Miezi 3 inaelekea NFRA hawajalipa mahindi mkoa wa Ruvuma kwa wakulima. Pia kodi kwenye malipo kuna kodi mkulima anakatwa

Frustration

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,134
Reaction score
4,124
Habari za asubuhi Watanzania wenzangu.

Kwenye nchi hii kuna mambo yanaenda hovyo sana toka utoaji wa taarifa,maandalizi na mfumo mzima wa NFRA kama wakala wa chakula nchini.

Ikumbukwe wakala huyu alijinabaisha kuwa sasa atajiongezea jukumu lingine la kufanya biashara na wakulima wa mahindi nchini.

Ukiingia kwenye tofuti na matangazo yao utakuta wanasema nchi mbalimbali zinahitaji mahindi mfano kongo na Zambia na Mawali wanahitaji Unga toka nchini kwetu. Kwa maelezo yao sio chini ya tani 1.1Milion za mahindi zinatakiwa na nchi kama Kongo na Zambia.

Usanii ulianza kwenye bei ya ununuzi wa mahindi kwa wakulima, bei hazikutamkwa na NFRA bali Rais akiwa kwenye ziara zake za kikazi alianza kwa Tsh 600 kijijini na Tsh 650 mjini. Wala haikupita saa 24 akatengua kuwa mahindi yatanunuliwa Tsh 650 kwa Tsh 700.

Mapoja na maelekezo hayo NFRA hawajawahi kutoa tamko la bei ya mahindi vijijini na mjini bali mawakala wamewaachia wanunue kwa Tsh 500,550 na 600 kulingana na upepo ulivyo.

Pamoja na janja janja za mkulima kulipwa kwa kukatwa kodi n.k bado hizo hela hazitoki.

Nini kinasumbua NFRA na wakati wameingia mkataba na baadhi yq nchi kununua mahindi?
 
Soko la mahindi ni kubwa sana mnapelekaje NFRA na kila siku wanasumbua kulipa. Kusumbua kulipa hawajaanza leo kila mwaka ni wasumbufu. Vumilia tulia serikali hela imepeleka kwenye uchaguzi.
Wapeleke wapi na huyo ndio mnunuzi Mkuu na anatoa bei nzuri? Soko liko wapi? Marufuku Kuuza Nje ya Nchi
 
Habari za asubuhi Watanzania wenzangu.
Kwenye nchi hii kuna mambo yanaenda hovyo sana toka utoaji wa taarifa,maandalizi na mfumo mzima wa NFRA kama wakala wa chakula nchini.
Ikumbukwe wakala huyu alijinabaisha kuwa sasa atajiongezea jukumu lingine la kufanya biashara na wakulima wa mahindi nchini.
Ukiingia kwenye tofuti na matangazo yao utakuta wanasema nchi mbalimbali zinahitaji mahindi mfano kongo na Zambia na Mawali wanahitaji Unga toka nchini kwetu. Kwa maelezo yao sio chini ya tani 1.1Milion za mahindi zinatakiwa na nchi kama Kongo na Zambia.
Usanii ulianza kwenye bei ya ununuzi wa mahindi kwa wakulima, bei hazikutamkwa na NFRA bali Rais akiwa kwenye ziara zake za kikazi alianza kwa Tsh 600 kijijini na Tsh 650 mjini. Wala haikupita saa 24 akatengua kuwa mahindi yatanunuliwa Tsh 650 kwa Tsh 700.
Mapoja na maelekezo hayo NFRA hawajawahi kutoa tamko la bei ya mahindi vijijini na mjini bali mawakala wamewaachia wanunue kwa Tsh 500,550 na 600 kulingana na upepo ulivyo.
Pamoja na janja janja za mkulima kulipwa kwa kukatwa kodi n.k bado hizo hela hazitoki.
Nini kinasumbua NFRA na wakati wameingia mkataba na baadhi yq nchi kununua mahindi?
Ondoa hiyo avatar picha yako. Yani utapita mlo kukosa mahindi ndo umekonda hivyo
 
Kama ni kweli, serikali haina huruma na wananchi wake.

Yaani kila kona malalamiko, huku wakulima wanadai chao, hapa wastaafu wanadai, kule wanasiasa wa upinzani wanadai haki zao

serikali kawa m'bade kuliko wenye nchi
 
Niliuza mpunga morogoro kg 1 TSH 900 nashukuru nilipokea malipo yangu last week na nilipima September 23, it took like 3 weeks. Bei ya mtaani efu 75 NFRA wamenunua kwa ef 90,000
 
Shida wafanyabiashara wanawauzia NFRA. Serikali kununua haya mazao lengo ni kuwapa soko wakulima.

Na sijui kwa nini mkurugenzi wa NFRA hawasimamii mameneja wake kuzingatia hili.

Mkulima ndiye anatakiwa aiuzie NFRA, siku serikali ikiamua kusimamia hili kuna watu watafilisika.
Magufuli aliwanyoosha kwenye korosho kwa kufanya uhakiki kama kweli ni mkulima.

Hii inabidi iwe kwa mazao yote yanayonunuliwa na NFRA, ni lazima uwe mkulima ili uweze kuuza NFRA.

Haya malalamiko huwezi kuyasikia, isipokuwa hawa traders ndio vimbelembele tu. Ole wenu, nasema tena ole wenu. Nimewafungulia code, kilio kipo jirani.
 
Back
Top Bottom