Miezi mitatu kabla ya kuandamana Wenyeviti wa vijiji 80 vya Ngorongoro walikwenda kumsihi RC Makonda awarudishie huduma za kijamii

Miezi mitatu kabla ya kuandamana Wenyeviti wa vijiji 80 vya Ngorongoro walikwenda kumsihi RC Makonda awarudishie huduma za kijamii

Wamaasai waliibembeleza sana serikali kabla hawajaamua kuandamana.

Hapa chini kuna video ya wenyeviti wa vijiji waliokwenda kumuomba RC Makonda awarudishie huduma za kijamii katika maeneo yao.

Bila shaka viongozi hao wa wananchi hawakusikilizwa, na matokeo yake ni maandamano makubwa tuliyoyashuhudia.

Serikali yetu na CCM wanawachukulia Watanzania kama makondoo wasioweza kusimamia haki zao.

Soma Pia: Rais Samia Aagiza urejeshwaji wa huduma za kijamii Ngorongoro

Fuatilia video hii hapa chini.

Makonda angekuwa Rais angewafyeka Masai wote huku akijiita mtetezi wa wanyonge. 😂😂
 
Mzee unatafuta teuzi? Hivi kweli watuu wanaweza kunyimwa huduma za jamii bila Rais kuhusika kwa nchi yetu hii? Samia sio msikivu, amebanwa imebidi a retreat. Hana usikivu na nia ovu bado ipo palepalle....
Hivi Samia akitoka leo na kukemea utekaji utasema watu wa chini yake wawajibiswe?
Ku retreat ndio usikivu wenyewe.Zoezi la kuwahamisha Kwa hiari linaendelea huku Huduma zikiendelea.
 
Makonda alikuwa off kwenye shughuli za serikali msimsingizie

..umeangalia hiyo video?

..viongozi wa vijiji walikwenda kumuona Makonda miezi mitatu kabla ya maandamano. Wakati huo Makonda hakuwa likizo.

..maandamano yametokea baada ya Wamaasai kujaribu njia zote za amani na kushindwa.
 
Wakati anawaaagiza wafute vile vijiji Alikuwa amevaaa ile sura ya Chura kiziwi??
Wewe unadhani Mchengerwa Aliamka tu akaamua kufuta vijiji vyote na kuzuia huduma za kijamiii?
Ni maagizo ya huyo mama yenu, maji yalipofika shingoni akajirudi,
Hiii nchi tuendeleee kujitathimini na kujipanga ipo siku CCM, itaondoka.

..vijiji vilifutwa kwasababu Serikali ilishaondoa huduma kwa Wamaasai miaka 3 nyuma.

..Huwezi kufuta vijiji bila kwanza kuwa umefuta huduma.

..Tunapaswa kujiuliza vyombo vya habari vilikuwa wapi wakati mambo yote haya yanatokea?
 
ila serikali yake sio sikivu kabisa!. Nimeshauri waliotufikisha hapa kwenye hili la Ngorongoro wawajibishwe
Hapa itakuwa ni kutaka kutafuta mbuzi wa kafara tu.

Kwa mujibu wa hii katiba yetu mbovu, maamuzi mazito kama haya kwa vyovyote vile yametoka kwenye kichwa na kinywa cha rais.

Kama kuna anayepswa kuwajibika/kuwajibishwa basi rais awe ndiye nambari one.
 
Back
Top Bottom