KERO Miezi mitatu nafuatilia Passport mpya, napigwa kalenda tu, ni kweli UHAMIAJI mmeishiwa material ya kuprinti Passport mpya?

KERO Miezi mitatu nafuatilia Passport mpya, napigwa kalenda tu, ni kweli UHAMIAJI mmeishiwa material ya kuprinti Passport mpya?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sasa sikiliza mkuu, hii ni corrupt country yaan hapo inabidi utembee na bahasha yenye mpunga kunja km 250 au 300 wafuate wale maafisa pale ongea nao kibingwa waambie hio passport naitaka leo leo mshikishe kibunda akiwa anazihesabu msikilize anasemaje lazima atakwambia sawa subiri hilo sio suala la siku 2 au 3 ni suala la siku 1 tu ila kwa sababu hii Nchi inanuka rushwa kila sehemu ndio maana mambo yanakua na mlolongo mrefu sana na bila kutoa rushwa utasubiri na kusubiri wenzio wanaotoa unashangaa wanahudumiwa wanakupita wewe usietoa unapigwa kalenda

Kwa hio fanya hivyo nenda kawape hela wale maafisa siku hio hio waambie naitaka passport watakufanyia chapu chapu utaipata haichukui Muda
 
Sikutaka usumbufu nilitoa 750,000/= na ndqni ya wiki moja tu ikawa tayari.
 
Nilianza kufanya mchakato wa maombi ya kupata Pasi ya Kusafiria kwa kufuata njia halali, awali nilienda Kibaha Mkoani Pwani, kuna staff mmoja wa pale akanishauri kuwa kama nina haraka nifanye mambi yangu mtandaoni kisha nielekeze nikachukue Passport yangu hiyo Dar es Salaam

Nikafanya hivyo, baada ya kukamilisha kila kitu baadaye nikaanza mchakato wa kufuatilia, kila nikienda nikaanza kuwa nazungushwa naambiwa hivi mara vile.

Kila walichokuwa wakihitaji nikakifanya na kutimiza, ofisa mmoja ambaye jina na vithibitisho vyote ninavyo akaniambia “Niongee vizuri ili niweze kupata Passport yangu ndani ya muda mfupi” sikulifanya hilo kwa kuwa sikuwa na haraka na Pasi yenyewe, nimeamua kuchukua kwa kuwa ni haki yangu na ninaweza kuitumia siku za mbeleni.

Ningekuwa Mdada ningesema labda jamaa anataka kutumia njia hiyo kunitongoza lakini mazingira yanaonesha wazi kuwa bila kutumia mlango wa nyuma ni vigumu kupata huduma haraka kama Viongozi wa Uhamiaji wanavyojinadi.

Huu sasa ni mwezi wa tatu sijapata Passport yangu licha ya kukamilisha kila kitu, kila nikifuatilia naambiwa “njoo wiki ijayo”, kibaya zaidi kuna watu nawajua na tunajuana wao wamekuja mbele yangu wamepata Passport ndani ya muda mfupi.

Mimi nikiuliza naambiwa ipo kwenye mchakato wa kuprintiwa, mbona za wengine zinaprintiwa fasta?

Kamishna Dr. Anna P. Makakala hivi unajua kinachoendelea, je ni kweli kuna watu ambao wao ni maalum Nchini ndio wanapata Pasi mapema au ni kweli kuwa UHAMIAJI mmeishiwa material ya kuprinti Passport mpya?

Nimesoma uzi sehemu jamaa anasema kule Kibaha kuna ambao wameomba Passport huu ni mwezi wa Sita sasa hawajapata.

Pia soma
~
Upatikanaji wa Passport kwenye ofisi ya Uhamiaji pale Kibaha Mjini bado ni changamoto
~ Paul Mselle: Wenye changamoto ya kucheleweshewa “Passport” wafike
 
Kupata Passport ni kimbembe. Mm nilifatilia huku mkoani kwangu nikaferi afisa mmoja akanimbia tafuta 350 ukija dar nicheki wiki 1 tu unapata. Nikaona ngoja kwanza nitafute nauli
 
Back
Top Bottom