Miezi miwili bila mawasiliano ameachwa?naomba ushauri

Miezi miwili bila mawasiliano ameachwa?naomba ushauri

Sashay

Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
38
Reaction score
1
Hodini wana jamii,
naombeni ushauri, kuna rafiki yangu ana boyfriend wake wanapendana sana, kwa miaka mitatu alikuwa masomoni USA,miaka yote mawasiliano yao yalikuwa bomba, akarudi mwaka jana, alipokuwa nchini mapenzi yao yalikuwa motomoto, akamwambia kuwa amekuja kurenew visa yake na atakuwa hapa kwa wiki tatu tu, kama akipata visa ataondoka kwani bado anataka kukaa kidogo huko, kuna vitu anamalizia. Akamuomba rafiki yangu awe anasali ili afanikiwe kupata visa, wakaomba na alipoenda ubalozini visa ikatiki, akamuuliza kuwa itakuwaje kuhusu wao kama anaondoka tena, akamwambia asiwe na wasiwasi akifika atamtumia mualiko aende kumtembelea halafu wataoana huko huko. Sasa toka afike mawasiliano yapo mabovu, jamaa hapokei simu, hajibu sms wala e-mail sasa inakaribia miezi miwili, rafiki yangu yupo na wakati mgumu aelewi nini tatizo na kwa nini jamaa hawasiliani naye. Mimi ni rafiki yake mkubwa ananiomba ushauri, mimi sikuweza kumjibu haraka, nikaanza kutafuta input kwanza. Naombeni ushauri wana jamii
 
Hajawahi kupokea simu kabisa tangu aondoke? Kama ni hivyo labda kuna tatizo limempata. Huyo rafiki yako hana email ya mtu mwingine aliye karibu na huyo jamaa yake huko USA?

Ila kazi za kubeba maboksi nazo zinachosha sana, ukichanganya na yale mabarafu yanavyodondoka ndio kabisa watu hata simu za wapenzi wao wanaona kama zinawazingua tu! 🙂
 
mhhh inakaribia miezi 2, yaani hiyo cm inaitaga tu, hapo kuna walakini kabisa...nitarudi.
 
wabeba-boksi SIO WAOAJI!...mnatuacha vijana waoaji hapa n'chini mnachanganyikiwa na hao wahuni!.....

pole sana!
mwambie kwa G ''milango i wazi..''
 
wabeba-boksi SIO WAOAJI!...mnatuacha vijana waoaji hapa n'chini mnachanganyikiwa na hao wahuni!.....

pole sana!
mwambie kwa G ''milango i wazi..''

sasa hata mail hajibu, hivi kwanini wanaume hamuwi wa kweli ili wengine waendelee na mahusian mengine kuliko kuendelea kusubiri vicvyosubirika.....
 
mhhh inakaribia miezi 2, yaani hiyo cm inaitaga tu, hapo kuna walakini kabisa...nitarudi.

Hapo amesha nyolewa tayari aanze mikakati mingine labda jamaa alipata story kuhusu mchumba alipo rudi bongo kuwa hajatulia au amepata mchumba mwenye sifa zaidi ya huyu.
 
Hapo amesha nyolewa tayari aanze mikakati mingine labda jamaa alipata story kuhusu mchumba alipo rudi bongo kuwa hajatulia au amepata mchumba mwenye sifa zaidi ya huyu.

na kama amezipata c angefanya ustaarabu tu kumwambia mwenzie ukweli kuliko kumsubirisha, enzi zangu nilikuwa naogopa uchumba wa ulaya, mana unaweza subiri mpaka machweo....ni wachache sana wanatimiza ahadi.
 
Ndo maana waswahili wanasema ukiona mwenzio ananyolewa na wewe tia maji. Dalili za ukimyaa katika mahusiano maanake mwenzako amekuchoka cha kufanya ni kutuliza moyo na unaendelea na hamsini zako vinginevyo utasubili mpaka Yesu arudi mm na ndugu yangu walifunga mpaka harusi jamaa akaenda Canada mpaka leo hajarudi huu mwaka wa 15.
 
wewe! walikuwa na mtoto/watoto au ndio wamefunga tu jamaa akandoka?
 
Sashay,
mwambie rafikiyo MILANGO IKO WAZI in 22 days only!..AACHANE NA WATU WA ULAYA!wanaolewa na vibibi vya kizungu huko wanawasahau wapenzi wao!...
 
Yeah baada ya kufunga ndoa kanisani jamaa akaondoka hawakubahatika kupata mtoto.

na muachwa yupo kwenye hali gani kwasasa, alishaolewa au bado anamsubiria mume wake, haya mambo hayatabiriki ee.
 
Huyo kamwagwa kikubwa,akutukanaye si azima akutamkie tusi,matendo tu yanatosha!!!

lakini kwann hawanaga ujacri wa kusema ukweli hawa watu, angemuambia ukweli kwamba bwana mie naona hakitaeleweka ili dada wa watu aendelee na ustaarabu mwngine?
 
Hapa nashindwa kutoa neno mie inawezekana kweli ana matatizo ..au ndo hivyo binti kishapigwa kibuti mambo haya hayatabiliki kabisa ..

Pole Binti ongeza miezi mingine minne ifike sita tutajua cha kushauri hapa kama uanze kutafuta mwanakondoo mwingine au lah
ooops nilisahau huyu kijana hana hata ndugu TZ wanaoweza kumpa huyu mdada habari za ndugu yao??????????????
 
Nashukuru sana kwa kunipa input, huyo jamaa aliwahi kupokeaa simu siku ya tatu toka alipoondoka, akasema kuwa kafika salama, toka hapo simu inaitaa hapokei, sms hajibu, email hajibu, na sms zinaonyesha zimeenda. Rafiki yangu anampenda sana jamaa wametoka mbali sana yaani amedata.
 
Hapa nashindwa kutoa neno mie inawezekana kweli ana matatizo ..au ndo hivyo binti kishapigwa kibuti mambo haya hayatabiliki kabisa ..

Pole Binti ongeza miezi mingine minne ifike sita tutajua cha kushauri hapa kama uanze kutafuta mwanakondoo mwingine au lah
ooops nilisahau huyu kijana hana hata ndugu TZ wanaoweza kumpa huyu mdada habari za ndugu yao??????????????

A very good question. Au uchumba wao ni wa kuibia ibia? Halafu miaka mitatu ina maana huyo demu hapa Kibongo bongo alikuwa anavumilia kweli? I dought it!
 
na muachwa yupo kwenye hali gani kwasasa, alishaolewa au bado anamsubiria mume wake, haya mambo hayatabiriki ee.

Huyo anti bado yupo anamsubili jamaa ambae amesha mkatia mawasiliano siku nyingi aliondoka akimwahidi atakuja kumchukua waende wote.
 
Huyo anti bado yupo anamsubili jamaa ambae amesha mkatia mawasiliano siku nyingi aliondoka akimwahidi atakuja kumchukua waende wote.

Duh! Lazima atakuwa ameathirika sana kisaikolojia. Mpeni ushauri nasaha, huwezi kukaa miaka 15 unasubiri kuja kuchukulia. Atazeeka bila kuwa na watoto!
 
Back
Top Bottom