Mifuko ya Plastiki yaanza kuzagaa tena mitaani

Mifuko ya Plastiki yaanza kuzagaa tena mitaani

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Wakati wa utawala wa awamu ya tano tulishapiga hatua kwenye ishu ya kudhibiti mifuko ya plastiki iliyokuwa inageuza nchi yetu kuwa kama jalala.

Sasa hivi mifuko na vifungashio vya plastiki imerea tena nchini, uharibifu wa mazingira unaendelea kama kawaida.

Mifuko inatupwa hovyo mitaani, na hata inapochomwa moto ule moshi unasambaa majumbani na kutishia afya za watu.

Serikali ya Samia iko wapi kwenye suala hili nyeti, Mbona Hayati Magufuli alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti mifuko hii ya plastic?
 
Wakati wa utawala wa awamu ya tano tulishapiga hatua kwenye ishu ya kudhibiti mifuko ya plastiki iliyokuwa inageuza nchi yetu kuwa kama jalala. Sasa hivi mifuko...
Mimi mwenyewe kila nikinunua matunda jioni nikiwa njiani kurudi nyumbani mifuko ya palastiki inahusika kama kifungashio! Sijajua tatizo liko wapi? Au ni mifuko maalum iliyoidhinishwa? Ila kama ni tofauti na hapo tunarudi kule kule! Kuna viwanda wa palastiki vinatumia fursa hii ya serkali ya ngoja liende!
 
Na wafanyakazi hewa wamerudi kwa kasi

Usisahau bei ya korie kaka
 
Watu kuacha kutumia ile mifuko ya plastic ilikuwa ni nidhamu ya uoga, bila ile nidhamu ya uoga basi yawezekana ile mifuko bado ingeendelea kuwepo hadi leo.
 
Wakati wa utawala wa awamu ya tano tulishapiga hatua kwenye ishu ya kudhibiti mifuko ya plastiki iliyokuwa inageuza nchi yetu kuwa kama jalala. Sasa hivi mifuko na vifungashio vya plastiki imerea tena nchini, uharibifu wa mazingira unaendelea kama kawaida. Mifuko inatupwa hovyo mitaani, na hata inapochomwa moto ule moshi unasambaa majumbani na kutishia afya za watu.

Serikali ya Samia iko wapi kwenye suala hili nyeti, Mbona Hayati Magufuli alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti mifuko hii ya plastic?
Hili suala nimeliongelea tangu mwaka jana humu

Kuna uzi humu nilisema Makamu wa Rais ambaye Ofisi yake ndo inahusika na mazingira azunguke Dodoma kuona mifuko ya plastiki ilivyoanza kuzagaa hadi kwa wauza chips Ila wapi!

Kabla ya kwenda kwa Samia tumuulize Makamu wa Rais ambaye Ofisi yake inashughulikia mazingira kuwa inakuwaje anaacha mifuko ya plastiki kuanza kuzagaaa?

Kuhusu Jaffo kusema kweli sijawai kumkubali! Sioni kama ni Waziri makini
 
Acha roho mbaya.
Hyo mifuko laini meupe inasaidia sana.
 
Back
Top Bottom