Mifuko ya Plastiki yaanza kuzagaa tena mitaani

Mifuko ya Plastiki yaanza kuzagaa tena mitaani

Chadema wanamtaka jiwe tena. Duh kweli bila unafiki dunia haiendi.
UNafikiri Jiwe alifanya everything 100% wrong! Kuna aliyofanya vizuri likiwemo hili la plastics na kuna aliyofanya vibaya likiwemo la Demokrasia nchini.
Unachopaswa kujua ni kuwa kazi kubwa ya opposition ni kuona mapungufu na kuonyesha njia ambayo wao wanadhani ni bora; si kupongeza. Na wasipo pongeza haina maana hakuna mazuri
 
Kama mnaongelea hii mifuko milaini mbona ipo tu kabla mwendazake hajaenda?

Mengine mumpunguzie mama wa watu.

Kama imerudi ile mingine basi hapo SAWA tulijadili, ila kama hii ya kufungia barafu, karanga, vitu vya kupima madukani haijawahi kukosekana
 
Kama hatutakuwa na suluhisho thabiti kupiga marufuku kitu chochote tutakuwa kama tunacheza sindimba.. utoto tu
 
Wakati wa utawala wa awamu ya tano tulishapiga hatua kwenye ishu ya kudhibiti mifuko ya plastiki iliyokuwa inageuza nchi yetu kuwa kama jalala.

Sasa hivi mifuko na vifungashio vya plastiki imerea tena nchini, uharibifu wa mazingira unaendelea kama kawaida.

Mifuko inatupwa hovyo mitaani, na hata inapochomwa moto ule moshi unasambaa majumbani na kutishia afya za watu.

Serikali ya Samia iko wapi kwenye suala hili nyeti, Mbona Hayati Magufuli alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti mifuko hii ya plastic?
Story bila picha ni takataka
 
Ni mifuko gan? Au hii meupe midogo? Km n hii mbna iko tangu zama za Magufuli.
 
Wakati wa utawala wa awamu ya tano tulishapiga hatua kwenye ishu ya kudhibiti mifuko ya plastiki iliyokuwa inageuza nchi yetu kuwa kama jalala.

Sasa hivi mifuko na vifungashio vya plastiki imerea tena nchini, uharibifu wa mazingira unaendelea kama kawaida.

Mifuko inatupwa hovyo mitaani, na hata inapochomwa moto ule moshi unasambaa majumbani na kutishia afya za watu.

Serikali ya Samia iko wapi kwenye suala hili nyeti, Mbona Hayati Magufuli alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti mifuko hii ya plastic?
Kamfufue aje kudhibiti hiyo mifuko,mnaangaika kila kukicha na jitu liliokufa na halirudi tena.
Acheni aliyepo afanye kazi.
 
NEMC wapo wananenepa!
Serikali nayo ipo inanepanepa!
Tangu JPM aliposepa!
 
Weka picha
Wala halihitaji picha, mifuko ipo kweli. Kama wanataka kuiondoa wafanye jitihada kuiondoa, Kama hawataki waache.
Mm binafsi naipenda, Kuna sehemu inanifaa sana
 
Back
Top Bottom