Mifumo mitano ya ulinzi wa anga ya Israel inavyofanya kazi

Mifumo mitano ya ulinzi wa anga ya Israel inavyofanya kazi

Narumu kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
1,888
Reaction score
4,489
Israel imetumia mifumo yake ya ulinzi wa anga kukabiliana na mashambulizi ya makombora na droni katika miezi ya hivi karibuni.
Imeshambuliwa na Iran, Hezbollah kutoka Lebanon, Hamas kutoka Gaza na waasi wa Houthi nchini Yemen.
Marekani imepeleka mfumo wa kukabiliana na makombora ili kuimarisha ulinzi wa Israel. Mfumo wa ulinzi wa Terminal High-Altitude Area Defense (Thaad), utakuwa pamoja na mifumo mengine iliyopo ya Israel - ya Iron Dome, David’s Sling, Arrow 2 na Arrow 3.
Inaaminika kuwa Israel ilitumia mifumo yake yote ya ulinzi wa anga kukabiliana na shambulio la Iran tarehe 1 Oktoba. Shambulio hilo lilihusisha zaidi ya makombora 180, na baadhi yalipiga ndani ya Israel.
Hata hivyo, mifumo hiyo haikuweza kuzuia shambulio la ndege isiyo na rubani ya Hezbollah kwenye kambi ya jeshi la Israel karibu na Binyamina kaskazini mwa Israel tarehe 13 Oktoba, ambalo liliua wanajeshi wanne na kujeruhi makumi.
Pia unaweza kusoma

Mfumo wa Iron Dome​

Iron Dome unaelezwa kuwa ndio mfumo wa ulinzi wa anga uliojaribiwa zaidi duniani

Chanzo cha picha,Getty Images
Maelezo ya picha,Iron Dome unaelezwa kuwa ndio mfumo wa ulinzi wa anga uliojaribiwa zaidi duniani
Iron Dome ndiyo ngao ya ulinzi wa anga inayojulikana zaidi kati ya ngao za Israel. Imeundwa kuzuia roketi za masafa mafupi, yanayorushwa kutoka kilomita 4 na 70.
Kuna mifumo ya Iron Dome kote Israel. Kila betri moja ya Iron Dome ina matundu matatu hadi manne yenye makombora 20 kila moja.
Iron Dome hutambua na kufuatilia roketi zinazoingia kwa kutumia rada na kukokotoa ni zipi huenda zikaanguka kwenye maeneo yenye watu wengi. Kisha inarusha makombora kuzuia roketi hizi, huku roketi nyingine zikiachwa zianguke kwenye ardhi ya wazi.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema Iron Dome huharibu 90% ya roketi za adui. Makombora ya mfumo huo yaitwayo "Tamir" hugharimu takribani dola za kimarekani 50,000 kila moja.
Mfumo huo ulianzishwa baada ya "Vita vya Majira ya joto" vya 2006 kati ya Israel na Hezbollah. Kundi la lenye makao yake nchini Lebanon lilirusha takribani roketi 4,000 nchini Israel, na kusababisha uharibifu mkubwa na vifo vya makumi ya raia.
Mfumo huo uliundwa na makampuni ya Israel ya Rafael Advanced Defence Systems na Israel Aerospace Industries - kwa usaidizi kutoka Marekani - Iron Dome ilianza kutumiwa mwaka 2011.
Ilitumika kwa mara ya kwanza katika mapigano mwaka huo, kuzuia roketi zilizorushwa kutoka Gaza.
Tangu Oktoba 2023, mfumo wa Iron Dome umeharibu maelfu ya makombora yaliyorushwa na Hamas na makundi mengine ya wapiganaji kutoka Gaza.

Mfumo wa David’s Sling​

David's Sling missile launcher on an Israeli armed forces exercise

Chanzo cha picha,Getly Images
Maelezo ya picha,Mfumo wa David's Sling wakati wa mazoezi ya jeshi la Israel
David’s Sling, huitwa "Magic Wand" kwa Kiebrania, unaweza kuzuia makombora yanayotoka umbali wa hadi kilomita 300.
Umeundwa na kampuni ya Rafael Advanced Defence Systems ya Israel na Raytheon ya Marekani, ulianza kufanya kazi mwaka 2017.
Kama Iron Dome, David’s Sling unatungua tu makombora ambayo yanatishia kuanguka katika maeneo ya watu.
David’s Sling na Iron Dome zimeundwa pia kuzuia ndege, droni na makombora.
Kila kombora la David’s Sling linaloitwa "Stunner" linagharimu takribani dola za kimarekani milioni 1.

Mfumo wa Arrow 2​

An Arrow-2 missile being test-fired in the US in 2004.

Chanzo cha picha,Getty Images
Maelezo ya picha,Mfumo wa Arrow-2 ukiwa majaribioni nchini Marekani mwaka 2004.
Mfumo wa ulinzi wa Arrow 2 umeundwa kuharibu makombora ya masafa mafupi na ya masafa ya kati yanaporuka katika anga ya juu, kilomita 50 juu ya dunia.
Mfumo huo uliundwa baada ya Vita vya Kwanza vya Ghuba mwaka 1991, wakati Iraq ilipofyatua makumi ya makombora ya Scud yaliyotengenezwa na Usovieti hadi Israel. Mfumo huo ulianza kutumika mwaka 2000.
Unaweza kugundua makombora kutoka umbali wa kilomita 500. Unaweza kuzuia kombora la adui hadi kilomita 100 kutoka eneo kombora hilo liliporushwa.
Makombora ya mfumo huo husafiri kwa kasi mara tisa ya sauti, na yanaweza kushambulia hadi shabaha 14 kwa wakati mmoja.
Arrow 2 uliripotiwa kutumika kwa mara ya kwanza mwaka 2017, na kudungua kombora lililorushwa kutoka Syria.

Mfumo wa Arrow 3​

Mfumo wa Arrow 3 ulianza kufanya kazi 2017, na umeundwa kuzuia makombora ya masafa marefu yanaposafiri nje ya angahewa ya dunia. Mfumo huo unaweza kuzuia kombora lililo umbali wa kilomita 2,400.
Kwa mara ya kwanza ulitumika mwaka 2023, kunasa kombora la balistiki ambalo waasi wa Houthi nchini Yemen walilirusha katika mji wa pwani wa Eilat, kusini mwa Israel.
Mfumo huo ulitengenezwa na kampuni inayomilikiwa na serikali ya Israel Aerospace Industries, kwa usaidizi wa kampuni ya Boeing ya Marekani.

Mfumo wa Thaad​

Thaad missile launch

Chanzo cha picha,Getty Images
Maelezo ya picha,Mfumo wa Thaad umeundwa kupiga makombora ya adui katika angahewa ya dunia na nje ya anga hiyo
Baada ya shambulio la Oktoba la Iran dhidi ya Israel, Marekani ilisema itaipatia Israel mfumo wa ulinzi wa anga wa Thaad.
Mfumo wa Thaad umeundwa kufanya kazi kama David’s Sling, kuzuia makombora ya adui katika hatua ya mwisho, yakiwa yamesaliwa na umbali wa maili 93-125 (150-200km) kabla kutua.
Vilevile, mfumo huo unaweza kuzuia makombora ya adui ndani na nje ya angahewa ya dunia.
Betri za Thaad zinakuwa na matundu sita ya kurushia makombora, na kila tundu moja lina makombora manane.
Marekani imepeleka takribani wanajeshi 100 kuendesha mfumo huo ndani ya Israel. Mfumo huo na wafanyakazi wake tayari wamewasili.
Wanajeshi wa Marekani wamekuwa wakiutumia mfumo wa Thaad tangu 2015. Marekani imeuuza mfumo huo kwa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.
 
Myahudi wa kazuramimba unasema Israel wana ulinzi wa anga imara ila Iran karusha makombora yake ya majaribio yaliyosafiri zaidi ya 2000+ KM na yameenda kupiga Target Nevatim base hadi leo haifai tena kwa matumizi
 
Hivi kusifia kitu ambacho hakipo mnapata faida gani?
Mpo kwenye playlist ya ubalozi wa Israel?
 
Myahudi wa kazuramimba unasema Israel wana ulinzi wa anga imara ila Iran karusha makombora yake ya majaribio yaliyosafiri zaidi ya 2000+ KM na yameenda kupiga Target Nevatim base hadi leo haifai tena kwa matumizi
acha mahaba toa analysis
 
Myahudi wa kazuramimba unasema Israel wana ulinzi wa anga imara ila Iran karusha makombora yake ya majaribio yaliyosafiri zaidi ya 2000+ KM na yameenda kupiga Target Nevatim base hadi leo haifai tena kwa matumizi
Muiran wa Mwanachihangu hapo Mpitimbi
 
Sasa pamoja na mifumo yote ya ulinzi mbona Marekani amerazimika kuleta mfumo wake ili kuisaidia kuilinda Israel?
marekani imemwongezea mfumo mmoja wa dhaad ambao ni kama wanaufanyia majaribio tuu maana huu mfumo haujawah ingia mzigoni ukaonyesha cheche zake,
 
acha mahaba toa analysis
Analysis ya nini? Tarehe 1 oct Iran waliichakaza Nevatim Milliary Airbase ya Israel ambayo ndo home of F-35 fighter jet na ndege zote zilizokuwepo ziliharibiwa pamoja na kuua na kujeruhi, oct 2 serekali ikaomba wananchi wajitolee kwenda kutoa damu kwaajili ya kusaidia majeruhi
 
Analysis ya nini? Tarehe 1 oct Iran waliichakaza Nevatim Milliary Airbase ya Israel ambayo ndo home of F-35 fighter jet na ndege zote zilizokuwepo ziliharibiwa pamoja na kuua na kujeruhi, oct 2 serekali ikaomba wananchi wajitolee kwenda kutoa damu kwaajili ya kusaidia majeruhi
chanzo cha habari ili tukuamini maana najua uko yombo
 
Back
Top Bottom