Aiseee tunarudi palepale.
Hivi mtu kukupiga ngumi unajiona na mtu kukuvizia akakupiga kisogoni ipi inauma???
Labda nijitahidi kufafanua kwa mara ya mwisho.
Mwanamke kimaumbile huwezi mfananisha na mwanaume,ndio maana mwanaume anaweza tembea kifua wazi ila je mwanamke anaweza?
Kwahiyo mwanamke akichelewa kuolewa kesha akasemwa ni maumbile ndio yako hivyo.
Kuhusu ndoa kuvunjika tusidanganyane wanaume siku hizi tumeshapewa jina la wanyanyasaji.
Tukija katika suala la mtoto wa nje ya ndoa nadhani unafahamu kati ya baba wa kambo na mama wa kambo nani ana afadhali hilo sitaki kulizungumza.
Kuhusu hao masingle mother hukuwahi kukutana nao nadhani ila ungekutana nao nahisi ungeelewa,kwanza fuatilia sababu za wanawake kuwa masingle mother ni zipi utaelewa lawama zitaenda wapi.
Pia wanaume sie mambo yetu zoelefu yani hatuna mambo mengi pia huwezi fananisha athari ya matendo ya mwanamke na ya mwanaume.
Hivi kupigwa na kumsingizia mtu kesi ya ulawiti hivi vinafanana??
Mwanaume hajawahi play victim,mwanaume akilalamika ana sababu ya kulalamika.Ila mwanamke anaweza akaamua kukufanyia mambo ambayo ukijiuliza awali yake nini hupati tena kwa kutumia mgongo wa sheria inayomlinda.Hiyo ndio ku play victim.
Na siku hizi wamejisahau kabisa wao ni kina nani.
Ila tutawanyo
Hivi hapa tunajadili uhalisia au mawazo yako tu hebu fafanua kwanza ili nijue nadeal na mtu wa aina gani, yani haiwezekani bila aibu unasema kabisa eti makosa ya mwanaume yanajulikana, na hayaumizi kama ya mwanamke
Wewe ni nani wa kumuamulia au kumpangia mtu kiasi cha maumivu anayopata kutokana na makosa uliyomfanyia, yani umemkosea mtu halafu unasema hilo kosa lako ni dogo sasa hilo kosa linakuwa dogo kwa kipimo cha nani cha kwako wewe mkosaji au cha mkosewaji, asee hii sijawahi kuona hili nalo ni ajabu lingine la dunia dooh
Vipi na wanawake nao wakiamua kusema kwamba, makosa yao ni madogo kuliko ya wanaume nao watakuwa sahihi kwa upande wao siyo, halafu kuhusu suala la kutembea kifua wazi umetumia vigezo gani kusema kwamba kutembea kifua wazi ndio ishara ya kuwa superior
Zamani kabla ya wazungu kutuletea hizi nguo hata wanawake walikuwa wanatembea vifua wazi matiti yako nje, je hiyo ilimfanya mwanamke kuwa sawa na mwanaume katika namna yoyote ile, unaweza ukafafanua hapo
Bado sijaona uhusiano wa mwanamke kuchelewa kuolewa na maumbile yake, unaweza kufafanua maumbile ya mwanamke, yanahusiana nini na yeye kuwahi au kuchelewa kuolewa
Hapo uliposema kwamba ukiona mwanaume analalamika ujue ana sababu, hiyo ipo hivyo hata kwa wanawake wanapolalamika nao huwa wana sababu ila kama nilivyosema, huwezi kumuamulia au kumpangia mtu sababu ya kukulalamikia ikiwa wewe ndiye uliyemkosea huo ni umajnuni
Kuhusu suala la baba wa kambo na mama wa kambo hilo ni tabia za watu binafsi, na lina sababu zake tofauti kabisa hilo haliko kisheria, na wala hakuna sheria inayowatetea wamama wa kambo wanaotesa watoto