Aisee una mboyoyo nyingi sana.Hivi hapa tunajadili uhalisia au mawazo yako tu hebu fafanua kwanza ili nijue nadeal na mtu wa aina gani, yani haiwezekani bila aibu unasema kabisa eti makosa ya mwanaume yanajulikana, na hayaumizi kama ya mwanamke
Wewe ni nani wa kumuamulia au kumpangia mtu kiasi cha maumivu anayopata kutokana na makosa uliyomfanyia, yani umemkosea mtu halafu unasema hilo kosa lako ni dogo sasa hilo kosa linakuwa dogo kwa kipimo cha nani cha kwako wewe mkosaji au cha mkosewaji, asee hii sijawahi kuona hili nalo ni ajabu lingine la dunia dooh
Vipi na wanawake nao wakiamua kusema kwamba, makosa yao ni madogo kuliko ya wanaume nao watakuwa sahihi kwa upande wao siyo, halafu kuhusu suala la kutembea kifua wazi umetumia vigezo gani kusema kwamba kutembea kifua wazi ndio ishara ya kuwa superior
Zamani kabla ya wazungu kutuletea hizi nguo hata wanawake walikuwa wanatembea vifua wazi matiti yako nje, je hiyo ilimfanya mwanamke kuwa sawa na mwanaume katika namna yoyote ile, unaweza ukafafanua hapo
Bado sijaona uhusiano wa mwanamke kuchelewa kuolewa na maumbile yake, unaweza kufafanua maumbile ya mwanamke, yanahusiana nini na yeye kuwahi au kuchelewa kuolewa
Hapo uliposema kwamba ukiona mwanaume analalamika ujue ana sababu, hiyo ipo hivyo hata kwa wanawake wanapolalamika nao huwa wana sababu ila kama nilivyosema, huwezi kumuamulia au kumpangia mtu sababu ya kukulalamikia ikiwa wewe ndiye uliyemkosea huo ni umajnuni
Kuhusu suala la baba wa kambo na mama wa kambo hilo ni tabia za watu binafsi, na lina sababu zake tofauti kabisa hilo haliko kisheria, na wala hakuna sheria inayowatetea wamama wa kambo wanaotesa watoto
Embu fikirisha ubongo kama jamaa alivyokuambia hata kidocho.
Ngojea nikuulize maswali kadhaa;
1)Kumpiga mtu na kusingiziwa umembaka mtu/umemlawiti mtu vinafanana??
2)Asilimia ya baba wa kambo watesi na mama wakambo watesi ipi kubwa?
3)Mke wa Ashraf Hakimi alikua na sababu gani ya kudai talaka na kutaka mgawanyo wa mali??
Naanza kuhisi naongea na mtu ambae hana exposure na mambo mengi.
Unawezaje leta uwiano kati ya mwanamke na mwanaume kulalamika??
Unaweza ukanipa sababu ya wale wanawake wanaosingizia wame zao ubakaji/ulawiti na upigaji kesha kudai fidia za uongo??
Kwani nimesema nampangia mtu kosa kuwa ni dogo au ni kubwa??
Tuchukulie una watoto,wakaanza kuonesha tabia tofauti,mmoja mkorofi anapiga sana wenzake ila mwingine ana tabia ya kuchezea wenzake makalio na michezo michafu ya kingono,jibu kama MWANAUME NA MZAZI lipi kosa kubwa hapa la kulitazamia na kuhangaika kumnasua mtoto!!??
Au hayo yanafanana!!???
HUNA EXPOSURE NARUDIA HUNA EXPOSURE.
Bro kipindi chetu kuna mambo mengi yalikua yanafanyika ni nje na ustaarabu,kwa akili ya kawaida ni busara mwanamke kuwa kifua wazi??
Embu nijibu hapo.
Tulikua tunakeketana je ni sawa kisa ni mila zetu za zamani??
Pia nimeongea kikubwa umeshindwa kuing'amua hiyo kauli.
Hivi mwanamke ana kikomo cha miaka mingapi mpaka yeye ashindwe kuzalisha??
Hivi kikawaida heshima ya mwanaume na mwanamke ipi rahisi kuanguka kutokana na sababu za maumbile??
Aiseeee!!!!
Embu usilazimishe kuweka usawa mkuu ilhali kuna mambo yamepishana mizani hapa.
Kuhusu mama na baba wa kambo kafuatilie tena asilimia kubwa wapi kuna tatizo.
Fuatilia asilimia nadhani nikitumia neno asilimia utaelewa.