Lamomy
JF-Expert Member
- Sep 4, 2023
- 25,425
- 59,309
Nitajioa mwenyewe mkuu πππππππππ Kwenye ndoa hakuna uhuru. Sasa we utaweza ndoa Kweli au hutaki kuolewa kabisa wala kuisikia NDOA
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nitajioa mwenyewe mkuu πππππππππ Kwenye ndoa hakuna uhuru. Sasa we utaweza ndoa Kweli au hutaki kuolewa kabisa wala kuisikia NDOA
umenikumbusha wikiend moja hivi juzi kati hapa hapa kuna sista duu mmoja alinicheki na viswanglish vingi kama kawaida yao ananiambia twende kwenye show ya christian bella nikamwambia it's ok but we will split all bills. Ghafla sista duu akapotea hewani. ππππ ajira 50/50, elimu 50/50, uongozi 50/50, mgawanyiko wa mali 50/50. Haya sasa tumetoka out tumetumia laki moja kila mtu atoe elfu 50 hapo utaambiwa ilo jukumu la mwanaume kwa 100%.Wanawake bhana, wanadai 50/50, ila kwenye suala la pesa hawataki 50/50
Hamna kaka unajua yakitokea hayo jua kuna mahali kaka yetu alilegeza kamba.Wanawake ni mashetani kuliko Lucifer mwenyewe, kaka yangu anateswa na Lucifer wake mpaka na mimi naogopa kuoa.
Aiseeππππππππumenikumbusha wikiend moja hivi juzi kati hapa hapa kuna sista duu mmoja alinicheki na viswanglish vingi kama kawaida yao ananiambia twende kwenye show ya christian bella nikamwambia it's ok but we will split all bills. Ghafla sista duu akapotea hewani. ππππ ajira 50/50, elimu 50/50, uongozi 50/50, mgawanyiko wa mali 50/50. Haya sasa tumetoka out tumetumia laki moja kila mtu atoe elfu 50 hapo utaambiwa ilo jukumu la mwanaume kwa 100%.
Astagafiru πππππNitajioa mwenyewe mkuu ππππ
Tumisifu Yesu KristuAstagafiru πππππ
Nimemueleza mpaka mifano nimemtolea ila aiseeee jamaa mbishi.Mkuu katika hoja zako kuna kitu unajichanganya kidogo. Hakuna popote niliposema wanaume hawana makosa. Kama binadamu na mwanaume pia ana makosa hatuwezi kuanza kueleza makosa yote yanayofanywa na mwanaume na mwanamke. Mjadala unahusu namna mifumo inavyomkandamiza mwanaume na mwanamke anatumia nafasi iyo kutimiza malengo maovu. Ni kweli kuna wanaume wakatili, wabakaji, wanyanyasaji n.k lakini mada haihusiani na hayo
Milele aminaaaaTumisifu Yesu Kristu
Ili kuepuka yote hayo ni kutofunga ndoa.Tulikosea sana kuipokea hii sera ya 50/50 mbaya zaidi jukumu la kuieneza tukawaachia mafeminia vilaza wa type ya joyce kiria.
Sasa kati ya mimi na wewe ni nani ana mboyoyo mingi, wewe ndio unashusha magazeti lakini sioni cha maana ulichoandika, zaidi ya assumptions zako binafsi ambazo hazina uhalisiaAisee una mboyoyo nyingi sana.
Embu fikirisha ubongo kama jamaa alivyokuambia hata kidocho.
Ngojea nikuulize maswali kadhaa;
1)Kumpiga mtu na kusingiziwa umembaka mtu/umemlawiti mtu vinafanana??
2)Asilimia ya baba wa kambo watesi na mama wakambo watesi ipi kubwa?
3)Mke wa Ashraf Hakimi alikua na sababu gani ya kudai talaka na kutaka mgawanyo wa mali??
Naanza kuhisi naongea na mtu ambae hana exposure na mambo mengi.
Unawezaje leta uwiano kati ya mwanamke na mwanaume kulalamika??
Unaweza ukanipa sababu ya wale wanawake wanaosingizia wame zao ubakaji/ulawiti na upigaji kesha kudai fidia za uongo??
Kwani nimesema nampangia mtu kosa kuwa ni dogo au ni kubwa??
Tuchukulie una watoto,wakaanza kuonesha tabia tofauti,mmoja mkorofi anapiga sana wenzake ila mwingine ana tabia ya kuchezea wenzake makalio na michezo michafu ya kingono,jibu kama MWANAUME NA MZAZI lipi kosa kubwa hapa la kulitazamia na kuhangaika kumnasua mtoto!!??
Au hayo yanafanana!!???
HUNA EXPOSURE NARUDIA HUNA EXPOSURE.
Bro kipindi chetu kuna mambo mengi yalikua yanafanyika ni nje na ustaarabu,kwa akili ya kawaida ni busara mwanamke kuwa kifua wazi??
Embu nijibu hapo.
Tulikua tunakeketana je ni sawa kisa ni mila zetu za zamani??
Pia nimeongea kikubwa umeshindwa kuing'amua hiyo kauli.
Hivi mwanamke ana kikomo cha miaka mingapi mpaka yeye ashindwe kuzalisha??
Hivi kikawaida heshima ya mwanaume na mwanamke ipi rahisi kuanguka kutokana na sababu za maumbile??
Aiseeee!!!!
Embu usilazimishe kuweka usawa mkuu ilhali kuna mambo yamepishana mizani hapa.
Kuhusu mama na baba wa kambo kafuatilie tena asilimia kubwa wapi kuna tatizo.
Fuatilia asilimia nadhani nikitumia neno asilimia utaelewa.
Kila mtu ajitawale mwenyewe kusiwe na wa kumtawala mwenzie, kuoa au kuolewa ni dhana tu iliyotengenezwa wala haina uhalisia, hata wanaosema kuoana wako sahihi kwa upande wao vile vileKwahiyo nani anatakiwa amtawale mwenzie? Nani aliyemuoa mwenzie?
Ni majukumu mangapi yanayoitwa ya mwanamke ambayo wewe unayafanya, labda ukijiuliza hilo swali utapata majibu ya swali lako, au bado hata hujaoaLine ya mwisho umesema washirikiane na wasaidiane, hebu niambie mnatusaidia nini cha maana kwenye ndoa?
Ni upumbavu upi na umesababishwa na niniTimu kataa ndoa ni kwasababu ya upumbavu wa wanawake.
Yaani hata hujamuelewa aliyeandika, mwanamke kushindwa kutembea kifua wazi alimaanisha maumbile ya mwanamke ni tofauti na ya mwanaume, mwanamke anakoma kuzaa akiwa na miaka 45-50, je akichelewq kuolewa huoni hatopata mtoto? Bado hujaona uhusiano wa kimaumbile wa mwanamke na kuchelewa kuolewa? Na kuhusu mama wa kambo mbona umefukia fukia? Kwa kesi ulizozisikia kati ya baba wa kambo na mama wa kambo nani anaongoza kutesa watoto? Yaani kama hata wanawake hampendani wenyewe kwa wenyewe, mtatupenda sisi wanaume? Mliongea Nini na shetani kule Eden?
Sasa kati ya mimi na wewe ni nani ana mboyoyo mingi, wewe ndio unashusha magazeti lakini sioni cha maana ulichoandika, zaidi ya assumptions zako binafsi ambazo hazina uhalisia
1. Kwanza kabisa kwanini umpige mwanamke halafu kwanini useme "kusingiziwa umembaka au umemlawiti mtu", kwani si kweli kwamba kuna wanaume wanabaka na wanalawiti wake zao, kwanini umeassume kwamba wanaume wote wanaoshitakiwa kwa hayo makosa wanasingiziwa tu
2. Nimeshakuambia suala la wamama wa kambo kuwa watesi kuliko wababa wa kambo lina sababu nyingine kabisa, haliko kisheria hakuna sheria inayowatetea wanawake wa aina hiyo, hapa tunaongelea kuhusu mahusiano kati ya wanaume na wanawake
3. Kama Achraf Hakimi alikuwa anachepuka ulitaka mke wake asiombe talaka avumilie ujinga kama mliowaaminisha wanawake wa kiafrika, sababu ya kutaka mgawanyo wa mali ni majukumu aliyokuwa anayafanya huyo mwanamke, hasa kulea watoto ambayo probably mume alikuwa hafanyi hayo
Sasa hapo kwenye maumbile mbona unaongelea habari za umri wa kuzaa na kuzalisha, wakati mimi naongelea habari za kuoa na kuolewa hebu nioneshe, ni wapi nimeongelea habari za umri wa kuzaa na kuzalisha kati ya mwanaume na mwanamke
Mimi nilichoongelea ni habari za ndoa kwamba kwanini huku kwetu mwanaume akichelewa kuoa, hatukanwi wala hadhalilishwi kama anavyofanyiwa mwanamke akichelewa kuolewa wewe unaniletea habari za kuzaa na kuzalisha, kwani mtu kupata mtoto ni hadi asubiri ndoa kwani haiwezekani mtu kuoa au kuolewa akiwa tayari na watoto
Wewe ndio ambaye huna exposure kwa sababu ungekuwa nayo ungeweza kugundua kwamba hayo masuala ya maumbile yapo africa tu, ni mitazamo tu watu waliyojijengea vichwani mwao toka enzi na enzi na wala hayana uhalisia wowote, huko kwa wenzetu wanawake wengi wanachelewa kuzaa na kuolewa na wala hawatukanwi wala kudhalilishwa kwenye jamii zao na ndoa zao zinadumu vizuri kabisa
Kuhusu kutembea kifua wazi nimekuuliza kwanini hata hizo enzi ambazo wanawake walikuwa wanatembea vifua wazi bado hawakuwa sawa na wanaume, wewe unaona siyo ustaarabu kwa sababu uko kwenye dunia ya leo ambayo kila mtu anavaa nguo na kutembea uchi unaonekana kichaa, lakini zamani huo ulikuwa ustaarabu na ilionekana kitu cha kawaida kabisa
Mimi nimekuuliza ni kanuni gani ya asili inayoamua kwamba mtu kutembea kifua wazi ndio ishara ya mamlaka na kwanini iwe kutembea kifua wazi na si kitu kingine, wengine wanasema eti kisa mwanaume anakojoa amesimama sijui upuuzi gani sasa ndio mtuelezee ni kwanini hayo ndio yawe sababu ya utawala, vipi na wanawake nao wakiamua kusema kwamba wao ndio wanatakiwa wawe watawala kwa sababu ndio wanaoleta viumbe duniani je watakuwa sahihi au la
Watu ni wagumu sana kuelewa. Ndugu zanguni sijasema kwamba wanaume hawana makosa, sijatetea wanaume wanyanyasaji au wanacheat wake zao. Tukianza kuangalia kosa moja moja ni kweli kila upande una machafu yake lakini mada yangu nimeongelea mifumo imesimikwa katika namna ambayo inamkandamiza mwanaume mfano mgawanyo wa mali ndoa ikivunjika, mwanaume kubambikiwa mtoto n.k. Ni kweli kuna wanaume wanyanyasaji, makatili n.k lakini iyo sio content ya mada yangu.Bandiko refu ila lina uongo wa hapa na pale na hisia kwa wingi......
Inshort ni kwamba, msingi wa jamii iliyostaarabika ni familia, na familia ni baba, mama na watoto.
Sasa kama wanaume wanaona fahari kuzalisha na kuhepa na wanawake washaona ni sawa kuzaa na kulea watoto wenyewe bila mababa basi mtalalamika sana mpaka nature iamue yenyewe kuchekecha
Solution ya hayo yote ni familia zinazoishi bila kuviziana, baba anaona kucheat ni haki yake na mama anatafuta vyake kimya kimya ili kikinuka asepe..... lazima kuwe na mvurugano
Mkishaona hilo... wababa waleeni watoto wenu katika njia ya maadili ya kiume, lakini hii system ya kuzaa kama mifugo watoto wanalelewa na wamama tu, tena wamama walio busy mnazidi kuwa na kizazi cha wanaume wasiojiaminiYou see right there hakuna aliyepo top, but in the end mwanaume ndio kichwa cha familia. But anakuwaje if mtoto wa kike ndio anapewa powers za kusimama kwneye hiyo nafasi huku mwanaume akiachwa apambane kivyake? It a bot unfair
Hilo siyo suala binafsi bali ndio mitazamo ya wanaume wengi na wanaume wengi waliooa hufanya hivyo na huona sawa kabisa, sasa kama unajua kuwa na wanaume wana makosa kwanini badala ya kuanza kwanza kurekebisha makosa ya wanaume mnalazimisha kurekekebisha ya wanawake tu, uhalisia ni kwamba wanaume hawakandamizwi bali wana inferiority complex tu ya kuhisi kama wanaporwa mamlaka yao waliyozoea kuyatumia vibaya na kwamba wataenda kuukosa ule uvumilivu waliokuwa wanaupata toka kwa wanawakeSuala la kutembea na dada wa kazi ilo ni binafsi sana. Halafu hakuna sehemu nimesema kwamba wanaume hawana makosa. Nimeongelea jinsi mifumo ilivyosukwa kumkandamiza mwanaume.