Industrialisation2022
New Member
- Sep 8, 2022
- 3
- 2
Mapinduzi ya nne ya viwanda, yajulikanayo kama 4IR au 4.0, ni mapinduzi ya kidijitali yenye sifa za muunganisho wa teknolojia kati ya nyanja za kimwili, kidijitali na kibayolojia. Mapinduzi haya ya viwanda ni tofauti na yale matatu ya kwanza kwa sababu yale yalilenga kuongeza na kuendesha viwanda pamoja na uzalishaji wa kiotomatiki. Licha ya teknolojia ya 4.0 kuendelea kusaidia uundaji wa uzalishaji wa wingi na wa kiotomatiki, ukuaji huu wa viwanda umepenya kwenye tasnia nyingi ukiongeza ufanisi na kuboresha hali ya maisha ya watu katika nyanja tofauti, kuanzia kwenye uagizaji wa usafiri hadi ufanyaji wa mikutano ya kibiashara.
Mabadiliko kwenye sekta mbalimbali yanafanyika kwa kasi kubwa haswa kwenye mifumo ya uzalishji, usimamizi na utawala. Mifano michache ya teknolojia zinazoibuka ni pamoja na Akili Bandia (AI), Block chains, Roboti na Uchapishaji wa 3-D. Klaus Schwab alisisitiza kwamba teknolojia zinazoibuka, kwa kiasi kikubwa, zitazidisha uwezekano wa watu kuunganishwa na vifaa, hususani vifaa vya simu, kwa nguvu isiyo na kifani. Hili ni jambo ambalo linaendelea kufanyika hatua kwa hatua.
Je, hii ina maana gani kwa Afrika?
Afrika imechukua fursa ya 4.0 kwenye maboresho katika sekta ya ICT, yakichochewa hasa na kupanua huduma za kifedha za kidijitali hususani simu kama vile M-Pesa na Nala. Hata hivyo, ili kuongeza ushindani wa bara kimataifa kuna haja ya kwenda zaidi ya mifano iliyopo na kuongeza ubunifu na ujuzi wa ushindani miongoni mwa vijana kupitia upatikanaji wa habari na elimu, ushirikiano kati ya sekta mbalimbali, utekelezaji wa sheria na kanuni za ulinzi wa watumiaji na mengineyo.
Ni utaratibu gani wa kisera unaweza kuwekwa?
Kwa mujibu wa Ujumbe wa kaulimbiu ya Dhana ya Umoja wa Afrika "Utumiaji wa Mapinduzi ya Nne ya Viwanda kushughulikia Ukosefu wa Ajira kwa Vijana barani Afrika", Bara la Afrika liliorodheshwa kama nchi changa isiyo na uwezo wa uzalishaji na viwezeshaji muhimu vya sehemu ya uzalishaji inayohitajika kuongeza utayari wao kwa 4.0. Mabadiliko yanahitajika ili Afrika iweze kupokea mapinduzi ya nne ya viwanda kikamilifu.
Kwanza, bara linahitaji kubuni ujuzi wa kazi kwa ajili ya siku zijazo. Kuibuka kwa 4.0 kumesababisha waajiri kuelekeza utafutaji wao kwa watu binafsi walio na ujuzi tofauti. Ili kusonga mbele, nchi za Kiafrika zinahitaji kuwekeza katika elimu ili kutoa elimu bora.
Kwenye umri mdogo, watoto wanahitaji kufundishwa ujuzi ambao utashindanisha ubunifu wao, namna ya kukabiliana na changamoto, huruma pamoja na ujuzi wa kutatua matatizo mbalimbali. Watoto wanapofundishwa jinsi ya kufikiria nje ya boksi katika umri mdogo, inakuwa rahisi kwao kuona fursa, kuzitumia na kuboresha uchumi wa nchi.
Watoto wanaokua wakijua jinsi ya kuishi na wengine, jinsi ya kuhusiana na kuwajali wengine ni rasilimali kubwa kwa sababu taaluma zao zitapelekea kuvumbua masuluhisho kwa manufaa ya jamii ama kupitia miongozo ya sera, kanuni, miradi ya kuanzia na mengineyo.
Mbali na kuongeza kiwango cha elimu miongoni mwa vijana, silabasi kutoka ngazi za kati zinahitaji kusahihishwa na kujumuisha mafundisho na miradi ya kufurahisha na kushirikisha ambayo inakuza ujuzi wa ubunifu na uchambuzi. Hii inaweza kujumuisha, miradi ya ya utafiti ya kufurahisha ya kujifunza kuhusu tamaduni tofauti, kazi za kujitolea ili kukarabati kituo cha kulelea watoto kilicho karibu, kucheza michezo na mazungumzo baina ya vijana na wazee katika jamii, na zaidi.
Pia walimu, kuanzia elimu ya awali mpaka sekondari, wanahitajika kuongeza ujuzi wao, kwa kuhudhuria programu zinazoundwa ili kuboresha elimi yao kwenye teknolojia na pia kuhudhuria mafunzo ya kuwasaidia kuwaonyesha na kukuza uongozi, uchambuzi muhimu na ufumbuzi wa ubunifu katika madarasa yao. Serikali zinaweza kufanya kazi pamoja na sekta nyingine kuratibu na kutoa mafunzo haya kwa walimu ndani ya nchi, na kwa bajeti ya kutosha kimataifa.
Mashirika ya sekta binafsi na ya umma yanahitaji kushirikiana na taasisi za elimu, ili kuunda programu za vitendo zinazoendana na uhalisia wa jumuiya zao za ndani. Makampuni, mashirika na taasisi, kupitia Wajibu wao wa Kijamii, wanaweza kuajiri wanafunzi kujitolea katika kazi zao za kijumuiya, kwenye kutoa mahitaji kwa watu wasio na uwezo, kuunda vichujio vya maji kwa jumuiya inayohitaji na hata kuunda programu za kufundisha ujuzi, lugha na michezo katika jamii.
Kwa njia hii, wanafunzi wanaweza kushiriki kikamilifu katika kuunda suluhu zinazoweza kufikiwa na jamii. Shule lazima zitafute njia shirikishi za kukuza matumizi ya teknolojia kuanzia hatua za awali za masomo ili wanafunzi wanavyokua, ujuzi wao uimarishwe pia. Taasisi za juu, kwa kutumia teknolojia, zinaweza kutengeneza fursa za kuongeza ujuzi wa wanafunzi.
Hii inaweza kufanikishwa kwa kushirikiana na taasisi nyingine kwa ajili ya programu kama vile mijadala, uundaji wa sera, na uvumbuzi wa vifaa vya kutumika katika dawa au kilimo. Ili kunafikisha haya, ushiriki unapaswa kuambatanishwa na sifa za kuhitimu za mwanafunzi. Elimu juu ya uhalifu wa mtandaoni na usalama wa mtandao lazima itolewe kwa umati.
Hii sio tu kwa ajili ya kuongeza uaminifu na faragha kwa biashara ndogo za mtandaoni na za ukweli lakini pia kukuza matumizi yaliyokusudiwa kwa teknolojia, yaani mawasiliano, kujenga mitandao, benki na zaidi.
Pili, serikali inahitaji kuanzisha na kutekeleza sheria na mifumo ya udhibiti ambayo itakuza manufaa ya 4.0. Kwa kushirikiana na wadau katika sekta mbalimbali, serikali inaweza kuweka sheria zenye manufaa ya moja kwa moja kwa wadau.
Vigezo wazi vinahitaji kuwekwa katika sheria za kila sekta, ikijumuisha ubia na ushirikiano kati ya sekta. Vigezo hivi pia vinapaswa kuimarisha maendeleo katika ngazi ya kitaifa na bara. Nchi zinahitaji kuweka miongozo iliyo wazi pamoja na sheria za ulinzi kwa watumiaji biashara (startups) na ubunifu ulioanzishwa na vijana, ili kurahisisha uanzishaji wa biashara zao na kulinda ubunifu wa kazi zao.
Ushuru unaotozwa kwenye hatua za mwanzoni, uundaji au utengenezaji wa biashara unahitajika kuwa kwenye kiwango kidogo au kuondolewa kabisa, ili kuruhusu vijana kukuza mawazo na uvumbuzi wao bila vizuizi vya kifedha ambavyo vimekuwa vikizuia nafasi zao za kushiriki katika kuibuka kwa 4.0.
Pia serikali lazima iunde sheria za kukabiliana na uhalifu wa mtandaoni na kutoa mafunzo kwa wananchi kuhusiana na jinsi ya kutekeleza usalama wa mitandao, kama njia ya kuongeza uaminifu na dhamana ya faragha wakati wa kutumia mtandao.
Tatu, ili bara liweze kutumia mustakabali wa uzalishaji kikamilifu, sekta nyingi zinahitaji kupokea na kuanzisha matumizi ya teknolojia. Serikali zinapaswa kuipa teknolojia kipaumbele kwenye sekta za afya, kilimo na viwanda. Hili linawezekana kwa kukuza ubunifu wa vijana na kuunda mashine pamoja na vifaa vinavyoweza kutumika kutoa huduma ya dawa, taarifa za afya na uchunguzi kwa wananchi, hasa wale wanaoishi vijijini. Serikali inapaswa pia kuweka bajeti kwa ajili ya utafiti wa matibabu kufanywa kikamilifu.
Uwekezaji katika elimu ya afya ya wahudumu wa afya ni muhimu ili waweze kuwa sambamba na teknolojia zinazotumika katika dawa. Kupitia ushirikiano kati ya nchi na nchi, sekta ya afya inaweza kufaidika kutokana na tafiti shirikishi ili kupata tiba na mbinu za kuzuia magonjwa ya kawaida, vifo vya mapema na mengineo.
Sekta na nchi kwa ujumla zinapaswa kushirikiana ili kuwapa vijana ujuzi unaokuza ufanisi katika kilimo na kurahisisha upatikanaji wa masoko kwa wakulima.
Mafunzo ya ufundi stadi yanaweza pia kuanzishwa ili kuwafundisha vijana na watu wengine jinsi gani wanaweza kutumia teknolojia kutengeneza mashine na vifaa vitakavyoongeza mazao shambani.

Upvote
4