Mifumo ya Uendeshaji wa Serikali ya Awamu ya Tano, iangaliwe upya! Watanzania "tutachoka" vibaya sana ndani ya hii miaka 10 ya Mhe. Rais Magufuli

Mifumo ya Uendeshaji wa Serikali ya Awamu ya Tano, iangaliwe upya! Watanzania "tutachoka" vibaya sana ndani ya hii miaka 10 ya Mhe. Rais Magufuli

Fumadilu Kalimanzila,

Wewe huoni hizi Mega projects zinazoendelea, unafikiri duniani kuna nchi haikopi? USA mwenyewe ana madeni sembuse TZ

Kwasasa tunajenga nchi waambie wawe wavumilivu, wajukuu zao watafaidi sana na waendelee kuchagua CCM na JPM 2020 maana nchi inajengwa na jemedari JPM kwa manufaa ya baadaye na ikiwezekana hata wafanye kazi bila mishahara..

Hao wafanya biashara ni wapiga dili na huko benki walikuwa wapiga dili na wezi CHADEMA sasa jemedari JPM ananyoosha njia wezi wote chali na sasa amerudisha weledi na utiifu kila mahala, heko JPM.

Tuwe wazelendo tumuunge mkono jembe letu JPM, maana watu wa hivi wanapatikana mara moja kama kakakuona.. Ni neema kwa watanzania kumpata JPM tumlinde na tumuongezee ulinzi ikiwezekana mabeberu wasije kumdhuru...
Aisee....nimekuelewa vizuri!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAPIGA DILI ambao leo wamevaa koti la UZALENDO hawataki taarifa za CAG aliyepita Prof.Musa Assad,hawataki manunuzi kama ya Ndege yafuate sheria za manunuzi na wala hawataki idhini ya Bunge!

Hao wazalendo mkuu wanataka nchi iende mbele, tumenunua ndege wenyewe halafu utukague ili iweje mbona wengine hawakununua baadala yake waliuza scraper zote alizoacha JKN.. Mkuu kuwa Mzalendo chagua JPM 2020 ushindi 99.9%
 
Ninacho juwa mm japo sina uwakika mwisho wake ni mgumu sana maana usie mpenda amekuja. Mh Rais anachowaza sio kitakcho tokea. Kagame kampoteza njia Tz sio Rwanda ndio maana wenye akili wapo kimya sana kiasi hata yeye mwenye taifa anajiuliza. Yes they are cool na wote wanapiga makofi. Wanajizuwia ila wanajuwa hard time to come. Hakuna urafik kati ya bunge,mahakama na serikali kuu. Ndio maana wenye akili wapo kimya ila yeye anafikiri ni wamoja. Kwaheri
Aisee umenena Mkuu...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunyweni bia tusheherekee Christmas nchi iko kwenye mikono salama ya jembe Dr JPM chini ya askari wake wa miavuli RC Makonda, RC Mnyeti, Kangi Lugola, DC Jokate, RC Dr pale Mbeya, DC Sabaya, Mh Jafo, Mh Karemani, Mh Biteko, Polepole, Dr Bashiru nk..

Chrismass tamu haijawahi kutokea ng'ombe, mbuzi, kondoo na kuku wamechinjwa balaa maduka ya nguo yako bize mpaka jana usiku wa manane, kariakoo imekesha wiki hizi mbili... 2020 chagua Dr JPM ushindi wa kishindo 99.9%..
 
Hujui usemalo. Sasa hivi serikali inapora watu (wastaafu hawalipwi, wafanyakazi hawajapata increments ambazo zimeainishwa kwenye mikataba yao ya ajira,wakulima wanadai, marejesho ya VAT hayajafanyika tangu 2016, wafanyabiashara wanabambikiziwa kodi za kutunga kila siku, ofisi za umma hazipewi OC etc) halafu umekalia ngonjera eti uchumi unakua kwa 7%!
Kwa nini serikali hailipi madeni yake hayo kama uchumi unakua kiasi hicho?
Aisee hebu tuliza akili soma kwa utulivu,utamuelewa vizuri Mkuu.....!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ni propaganda za CDM na ACT..

Watumishi wa Serikali kwasasa wanaenjoy maisha ukiondoa wale wapiga dili ila wale wote waadilifu maisha yao safi kabisa na 2020 wote kura kwa JPM wanampa miaka mitano mingine..

Wafanyabiashara wote kwasasa wanafanya biashara zao bila bugudha Serikali ya awamu ya tano inawajali kuanzia wale wakubwa, saizi ya kati na machinga, mama ntilie nk.. Rais wawanyonge ameruhusu machinga na mama ntilie wasibughuziwe na wafanye biashara kwa utulivu.. wote 2020 kura kwa JPM ushindi 99.9.%.

Awamu ya tano chini ya jemedari JPM aka masiha imejenga chato Airport na Burigi nation park kufungua kanda mpya ya utalii na soon madege yatatua pale Chato kuleta maelfu ya watalii na fedha za kigeni kwa manufaa ya watanzania wote na kuongeza vipato vya wakazi wa hayo maeneo.. JPM oyee kura zote kwake 2020 ushindi 99.9%.

Nimekuelewa chief🤣
 
Zakaria Lang'o,

Mkuu wacha tu, kuna kampuni moja huko Arusha inaitwa Quality food nilikuwa nafanya biashara, wameamua kufunga kampuni yao huku ajira zaidi ya 500 zikipotea! Huo ni mfano halisi wa kile kinachoendelea nchini. Pata picha watu 500 wapoteze ajira kisha piga uchumi unakuwa katika hali gani, na hizo familia zilizopoteza ajira zinakuwa kwenye hali gani!
Halafu wenye takataka kichwani humu wanakalia kuimba sifa!!
Inachofanya serkali ni uharamia dhidi ya jamii. Maelfu tayari wako vijiweni kwa jina la Machinga, na kama haitoshi bado secta binafsi inayoweza kukomboa watu nayo inatazamwa kwa jicho la husuda na watawala ambao wanapaswa kuisaidia ili iajiri zaidi.
Nafikiri kuna kitu si sawa kichwani kwa watawala hawa wa awamu ya tano japo tunajua CCM ni ile ile tangu kale!!!
 
Hao wazalendo mkuu wanataka nchi iende mbele, tumenunua ndege wenyewe halafu utukague ili iweje mbona wengine hawakununua baadala yake waliuza scraper zote alizoacha JKN.. Mkuu kuwa Mzalendo chagua JPM 2020 ushindi 99.9%
2020 hakutakuwa na mgombea anaitwa JPM kwenye kinyan'ganyiro cha urais.
 
U
Wewe utakuwa mpiga dili au kibaraka wa Mbow kule CHADEMA.

Hela ipo mtaani nyingi tu, wewe fanya kazi kwa bidii tu mlizoea vya bure bure havipo sasa.. "Hapa kazi tu"

Wanaolalamika wengi ni CHADEMA, wapiga dili, vyeti feki na wale waliotumbuliwa lakini kwa wapiga kazi hali ni shwali kabisa..

Uchumi unakua kwa zaidi ya 7%, Hali ya umasikini mtaani imepungua, tuna hifadhi ya dola ya kutosha, shilingi imeimarika, SGR, Stieggler, Maflyover kila kona nk..

Watanzania mnataka nini? wakati mmeletewa masiha aka mkombozi JPM ambaye mpaka USA, UK huko ni gumzo huku wakenya wakitamani awe Rais wao..
Tulia basi mavyama ya nn mbona unanongwa jamani amekosea kwa hekima tu hapo no tusi unaanza kubwabwaja kwan ni dhambi kumkosoa raisi? Sis ndo mabosi zake wananchi anawajibika kwetu
 
Naandika waraka huu mfupi nikitambua kuwa kuna watu leo katika Nchi hii hawataki kusikia mawazo mbadala wala kukosolewa kwa mwenendo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Mhe.Rais Magufuli chukua muda sikiliza pia mawazo mbadala kutoka kwa watu ambao hawakusifii tu!

Mhe.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekiri katika kitabu chake cha My Life, My Purpose kuwa kuna "wahuni" walimpotosha!

Lakini kumbuka alikuwa bingwa wa kuita wenye mawazo tofauti na yeye Wavivu wa kufikiri, leo yako wapi?!

Mhe.Rais Kikwete amelifanyia Taifa hili mambo mengi pia mazuri tena kwa unyenyekevu na uungwana wa hali ya juu!

Wakati wake kuna wapambe nuksi walikuwa hawawezi kumuita Mhe.Kikwete bila kuanza na neno "Dakta" tena kwa mbwembwe kweli! leo neno "Dakta" wamelisahau kabisa!

Hata wewe Mhe.Rais wetu Dr. Magufuli umezungukwa na wachumia tumbo wengi kweli ambao hawakwambii ukweli!

Wanajitahidi sana kutaja majina yako yote manne tena kwa mbwembwe ila wengine tunajua tu ni unafiki wa kutengenezea Ugali.

Kama unadhani nasema uongo Mhe.Rais Magufuli naomba uniwie radhi lakini nakuhakikishia tukiwa hai hapo utakapo kabidhi kijiti cha Urais pengine ukawa Rais Mstaafu utakayebezwa kuliko wenzako wote!

Na hata hawa wachumia tumbo uliowapa nafasi wanashindana kukutaja muda wote kwa majina manner(4) ya " Dokta John Pombe Joseph Magufuli" watapungua sana ama hutawasikia kabisa, na hata huko Chato hutawaona kabisa!

Ninatoa ushauri huu nikiamini kuwa viongozi tunapowachagua ni katika dhana ya kuwatanguliza mbele ili muongoze njia lakini si kwamba nyie mnajua kila kitu na mna hatimiliki ya kuhodhi mawazo na ubunifu wa kila jambo !

Mhe.Rais Dr.Magufuli hebu jaribu kuangalia kwamba Mfumo wako wa Utawala umeziua Halmashauri za miji,majiji na manispaa! ( ugatuzi wa madaraka haupo) ,kila kitu ni wewe tu ndo mpaka uamue!

Hii si sawa Tanzania ni Nchi kubwa! na Wananchi wanapaswa kujiamulia mambo yao kwa upana! Mwl.Nyerere alisisitiza sana umuhimu wa Serikali za Mitaa zenye Nguvu!

Hivi karibuni umepiga marufuku Wakurugenzi wasikope wasubiri Serikali iwape pesa za kujiendesha, hii si sawa unachelewesha maendeleo!

Pendekezo langu kwako ni kuwa rejesha Wizara ya TAMISEMI chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ,maana hata Waziri Mkuu kwa sasa ni sawa tu na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum!

Kingine Mhe.Rais Dr.Magufuli tambua kuwa popote Duniani Serikali ndiye mchezeshaji Mkuu wa Uchumi katika Nchi husika!

Leo wewe mifumo yako ya uendeshaji wa Nchi inaua sekta binafsi ( Private sector) na hata Ma- Guru wa sekta Binafsi wanaondoka nayo ( refer Mzee Mengi na Ali Mufuruki).These Guys knew the truth na perhaps wamemezwa na Depression tu!

Leo kuna vitu kama "Force Account" ,NHC,TBA na Suma JKT ndio Contractors wanaofanya kazi za Serikali!

Mhe.Rais watu wako watapata fedha kutoka wapi na kwa kazi zipi?

Rais Barack Obama alivyoingia madarakani nchini Marekani wakati wa recession alichofanya ni kuingiza fedha mitaani kupitia kufufua miradi mikubwa ya ujenzi na kupunguza budget za Vita ya Afghanistan na Iraq.

Wachumia tumbo waliokuzunguka wanakudanganya Mhe.Rais wetu,hawakuambii ukweli!

Uendeshaji wako wa Nchi unawafukarisha Watanzania wengi!

Mhe.Rais Dr.Magufuli kuhusu uchapaji kazi wako sijawahi kuwa na mashaka nawe hata kidogo.Wewe ni mchapakazi kweli kweli na kwa hili vizazi vingi katika Taifa hili vitakukumbuka Mzee.

Ila kwenye eneo la uzalishaji ( productivity) nina mashaka sana na taarifa tunazopewa na Serikali yako!

Umenunua Ndege, Unajenga Reli,Unajenga Stiglers Gorge na Structures kibao zingine na unasema kwa fedha za Ndani!

Fedha za Ndani zipi? Mbona Deni la Taifa tunaambiwa ulikuta ni Trillion 29 na leo limepanda hadi Trillion 52!

Kwanini Deni hilo lipande kama kuna uzalishaji na uwekezaji wa maana?!

Maana kuongezeka kwa uzalishaji na uwekezaji ndo kuongezeka kwa mapato (Kodi) ya Serikali ambayo tungesema ndiyo unatumia kujenga hiyo miundombinu!

Kuongezeka kwa Deni la Taifa ni kielelezo cha kutokuwepo kwa ongezeko katika uzalishaji na uwekezaji na matokeo yake ndo ukosefu wa ajira tunaouona katika kipindi chako!

Sekta binafsi imekufa na haiwezi kuajiri na pia Serikali yako haiajiri japo kuna matamko eti Rais kasema waajiriwe elfu 40!

Mhe.Rais hutakiwi wewe useme watu waajiriwe kanuni za uchumi uzungumza zenyewe!

Automatically waajiriwa huuitajika pale uchumi unapo- perform!

Mhe.Rais Dr.Magufuli niwie radhi nirudie kauli ya yule Mtanzania pale Igunga!

Mhe.Rais ACHIA HELA! Serikali yako imeua Liquidity katika Mabenki! Rudisha fedha kwenye commercial banks toka BOT ili watu wakopeshwe wafanye kazi!

Watu wenye nguvu sasa wameamua kukaa vijiweni wanapiga soga,wana bet n.k hakuna mitaji!

Naomba kwa leo niishie hapa Mhe.Rais.

Mhe.Rais Dr.Magufuli nakutakia wewe pamoja na Mama yetu mpendwa Mama Janet Magufuli heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2020.
Swali fikiri je una uhakika ya kuishi miaka 10 au 5 ijayo ''you have to think out side the box with this question before you give an answer''
 
U
Tulia basi mavyama ya nn mbona unanongwa jamani amekosea kwa hekima tu hapo no tusi unaanza kubwabwaja kwan ni dhambi kumkosoa raisi? Sis ndo mabosi zake wananchi anawajibika kwetu

Mkuu hizo ni hadithi za kufurahishia genge, kwamba wananchi ndio maboss wa rais? Una uhakika rais anapatikana kwa kura za hao wananchi?
 
Mkuu upo sahihi sana, hii ni nchi ya wanyonge.
Hahaaa
Fumadilu Kalimanzila,

Wewe huoni hizi Mega projects zinazoendelea, unafikiri duniani kuna nchi haikopi? USA mwenyewe ana madeni sembuse TZ

Kwasasa tunajenga nchi waambie wawe wavumilivu, wajukuu zao watafaidi sana na waendelee kuchagua CCM na JPM 2020 maana nchi inajengwa na jemedari JPM kwa manufaa ya baadaye na ikiwezekana hata wafanye kazi bila mishahara..

Hao wafanya biashara ni wapiga dili na huko benki walikuwa wapiga dili na wezi CHADEMA sasa jemedari JPM ananyoosha njia wezi wote chali na sasa amerudisha weledi na utiifu kila mahala, heko JPM.

Tuwe wazelendo tumuunge mkono jembe letu JPM, maana watu wa hivi wanapatikana mara moja kama kakakuona.. Ni neema kwa watanzania kumpata JPM tumlinde na tumuongezee ulinzi ikiwezekana mabeberu wasije kumdhuru...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibwengo anakusanya pesa na kuzigawa mwenyewe ajuavyo. Kwenye Taasisi za chini hazifiki kabisa.

Ndio maana kila kitaasisi sasa ili kiishi, kimeamua na chenyewe kukusanya fedha zake chenyewe:

- TARURA
- NEMC
- TRA
- SERIKALI ZA MITAA
- HALMASHAURI
- FIRE
- TRAFFIC POLICE
Na hapo wanaoumia kwa kuwa bombarded na michango yote hiyo ni wale wale, WANANCHI.
 
Naandika waraka huu mfupi nikitambua kuwa kuna watu leo katika Nchi hii hawataki kusikia mawazo mbadala wala kukosolewa kwa mwenendo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Mhe.Rais Magufuli chukua muda sikiliza pia mawazo mbadala kutoka kwa watu ambao hawakusifii tu!

Mhe.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekiri katika kitabu chake cha My Life, My Purpose kuwa kuna "wahuni" walimpotosha!

Lakini kumbuka alikuwa bingwa wa kuita wenye mawazo tofauti na yeye Wavivu wa kufikiri, leo yako wapi?!

Mhe.Rais Kikwete amelifanyia Taifa hili mambo mengi pia mazuri tena kwa unyenyekevu na uungwana wa hali ya juu!

Wakati wake kuna wapambe nuksi walikuwa hawawezi kumuita Mhe.Kikwete bila kuanza na neno "Dakta" tena kwa mbwembwe kweli! leo neno "Dakta" wamelisahau kabisa!

Hata wewe Mhe.Rais wetu Dr. Magufuli umezungukwa na wachumia tumbo wengi kweli ambao hawakwambii ukweli!

Wanajitahidi sana kutaja majina yako yote manne tena kwa mbwembwe ila wengine tunajua tu ni unafiki wa kutengenezea Ugali.

Kama unadhani nasema uongo Mhe.Rais Magufuli naomba uniwie radhi lakini nakuhakikishia tukiwa hai hapo utakapo kabidhi kijiti cha Urais pengine ukawa Rais Mstaafu utakayebezwa kuliko wenzako wote!

Na hata hawa wachumia tumbo uliowapa nafasi wanashindana kukutaja muda wote kwa majina manner(4) ya " Dokta John Pombe Joseph Magufuli" watapungua sana ama hutawasikia kabisa, na hata huko Chato hutawaona kabisa!

Ninatoa ushauri huu nikiamini kuwa viongozi tunapowachagua ni katika dhana ya kuwatanguliza mbele ili muongoze njia lakini si kwamba nyie mnajua kila kitu na mna hatimiliki ya kuhodhi mawazo na ubunifu wa kila jambo !

Mhe.Rais Dr.Magufuli hebu jaribu kuangalia kwamba Mfumo wako wa Utawala umeziua Halmashauri za miji,majiji na manispaa! ( ugatuzi wa madaraka haupo) ,kila kitu ni wewe tu ndo mpaka uamue!

Hii si sawa Tanzania ni Nchi kubwa! na Wananchi wanapaswa kujiamulia mambo yao kwa upana! Mwl.Nyerere alisisitiza sana umuhimu wa Serikali za Mitaa zenye Nguvu!

Hivi karibuni umepiga marufuku Wakurugenzi wasikope wasubiri Serikali iwape pesa za kujiendesha, hii si sawa unachelewesha maendeleo!

Pendekezo langu kwako ni kuwa rejesha Wizara ya TAMISEMI chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ,maana hata Waziri Mkuu kwa sasa ni sawa tu na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum!

Kingine Mhe.Rais Dr.Magufuli tambua kuwa popote Duniani Serikali ndiye mchezeshaji Mkuu wa Uchumi katika Nchi husika!

Leo wewe mifumo yako ya uendeshaji wa Nchi inaua sekta binafsi ( Private sector) na hata Ma- Guru wa sekta Binafsi wanaondoka nayo ( refer Mzee Mengi na Ali Mufuruki).These Guys knew the truth na perhaps wamemezwa na Depression tu!

Leo kuna vitu kama "Force Account" ,NHC,TBA na Suma JKT ndio Contractors wanaofanya kazi za Serikali!

Mhe.Rais watu wako watapata fedha kutoka wapi na kwa kazi zipi?

Rais Barack Obama alivyoingia madarakani nchini Marekani wakati wa recession alichofanya ni kuingiza fedha mitaani kupitia kufufua miradi mikubwa ya ujenzi na kupunguza budget za Vita ya Afghanistan na Iraq.

Wachumia tumbo waliokuzunguka wanakudanganya Mhe.Rais wetu,hawakuambii ukweli!

Uendeshaji wako wa Nchi unawafukarisha Watanzania wengi!

Mhe.Rais Dr.Magufuli kuhusu uchapaji kazi wako sijawahi kuwa na mashaka nawe hata kidogo.Wewe ni mchapakazi kweli kweli na kwa hili vizazi vingi katika Taifa hili vitakukumbuka Mzee.

Ila kwenye eneo la uzalishaji ( productivity) nina mashaka sana na taarifa tunazopewa na Serikali yako!

Umenunua Ndege, Unajenga Reli,Unajenga Stiglers Gorge na Structures kibao zingine na unasema kwa fedha za Ndani!

Fedha za Ndani zipi? Mbona Deni la Taifa tunaambiwa ulikuta ni Trillion 29 na leo limepanda hadi Trillion 52!

Kwanini Deni hilo lipande kama kuna uzalishaji na uwekezaji wa maana?!

Maana kuongezeka kwa uzalishaji na uwekezaji ndo kuongezeka kwa mapato (Kodi) ya Serikali ambayo tungesema ndiyo unatumia kujenga hiyo miundombinu!

Kuongezeka kwa Deni la Taifa ni kielelezo cha kutokuwepo kwa ongezeko katika uzalishaji na uwekezaji na matokeo yake ndo ukosefu wa ajira tunaouona katika kipindi chako!

Sekta binafsi imekufa na haiwezi kuajiri na pia Serikali yako haiajiri japo kuna matamko eti Rais kasema waajiriwe elfu 40!

Mhe.Rais hutakiwi wewe useme watu waajiriwe kanuni za uchumi uzungumza zenyewe!

Automatically waajiriwa huuitajika pale uchumi unapo- perform!

Mhe.Rais Dr.Magufuli niwie radhi nirudie kauli ya yule Mtanzania pale Igunga!

Mhe.Rais ACHIA HELA! Serikali yako imeua Liquidity katika Mabenki! Rudisha fedha kwenye commercial banks toka BOT ili watu wakopeshwe wafanye kazi!

Watu wenye nguvu sasa wameamua kukaa vijiweni wanapiga soga,wana bet n.k hakuna mitaji!

Naomba kwa leo niishie hapa Mhe.Rais.

Mhe.Rais Dr.Magufuli nakutakia wewe pamoja na Mama yetu mpendwa Mama Janet Magufuli heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2020.

Onyeaha kwanza wewe umekosoa vipi na ukatafutwa au ukalaumiwa?
 
😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Hilo la Wakurugenzi wa Halmashauri kukopa hapana aisee?!

Hata mimi binafsi siliungi mkono!

Tena sikuwahi kuwaza kama kitu cha namna hiyo kinaweza kufanyika kwenye Halmashauri zetu nchini.

Wao waimarishe ukusanyi wa mapato, wabuni vyanzo vya mapato visivyoumiza watu.

Ruzuku na OCs wanazipewa wachanganye pamoja kisha watekeleze miradi ya maendeleo kwa ufanisi mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
samurai,
Hio miradi hata ikijakamilika japo atujui uhakika wa kukamilika kwake itamsaidia vipi mtu aliyepigika maana itakuwa ni mapambo kama hakuna purchasing power uwezo Wa watu kuitumia.Mfano ATC nauli mwanza dar si chini ya laki tano kwenda na kurudi hali fastjet ilikuwa laki na nusu,kwann zisiende tupu,hio sgr usidhani nauli itakuwa buku si chini ya laki au zaidi kwa purchasing power nani atamudu ili irudishe Pesa?

Umeongea vizuri sana.....

Lakini kwa kuongezea tu kwenye hoja yako ni kuwa ishu si kutekelezwa ama kutotekelezwa kwa mega development projects kama vile mradi wa umeme wa Stiglers Gorge, ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR), ufufuaji Airline Charter ya nchi (ATCL) nk nk....

Na nadhani tuwaambie wote watoa sifa na serikali kwa ujumla kuwa, hakuna anayepinga nchi kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya maendeleo kama inavyotajwa....

Sisi wakosoaji (na nadhani ndiyo lengo na mantiki ya makala hii ya Fumadilu Kalimanzila), pamoja na nia njema ya miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na nchi yetu, lakini tunataka mambo yafuatayo yaende sambamba na hayo;

å MOSI, kuwe na uwiano ulio sawa kati ya maendeleo ya vitu na wakati huo huo tukiwaangalia watu kwa kuhakikisha kuwa wana uwezo wa kuuza na kununua, wana uwezo wa kumudu kupata mahitaji yao muhimu ya kila siku nk. Wengine wanasema tuangalie maendeleo ya watu zaidi kuliko vitu....!!!

Ukichunguza sana utagundua kuwa popote palipo na mitafaruku na migongano ya kijamii, chanzo chake ni watu kuchoka kwa kushindwa kumudu kupata mahitaji yao ya kila siku....

Kwa lugha rahisi na ya kueleweka, ni kuwa, fedha kuwa mikononi mwa wachache hususani tabaka la watawala huku wananchi wanyonge walio mengi kwa zaidi ya 95% wakiachwa bila kitu....!!

å MBILI, tabaka la WATAWALA na WATOA MAAMUZI liache kuhodhi nguvu ya uhuru wa watu kutoa maoni yao, hisia zao na grievances zao kwa mujibu wa sheria....

Mfano wanafunzi wa vyuo vikuu juzi kati hapa kufukuzwa chuo eti tu waliamua kudai haki yao ya kupata mikopo.....

Kwa lugha rahisi kabisa, tuachilie demokrasia ishike mkondo wake sawasawa na katiba na sheria zetu zinavyotuongoza.....

å TATU, tuachilie mifumo ya kiutawala na kisheria ifanye kazi kwa uhuru na kwa mujibu wa majukumu yao ya kikatiba na kisheria pasipo kuingiliwa......

Mwandishi wa makala tunayoijadili ameeleza vizuri sana kuhusu hili....

Kwamba, ilivyo sasa Binge, Mahakama na vyombo vingine vyote vinavyosimamia mwenendo wa kijamii kama polisi, TISS, ofisi ya CAG, msajili wa vyama vya siasa viko compromised na Executive (kwa maana ya Rais).....

Kwamba mifumo na vyombo hivi kwa sasa, ingalau kwa miaka hii minne zaidi (2015 - 2019), imejikita kufanya kazi kumlinda mtu mmoja zaidi aitwaye RAIS kuliko kulinda maslahi mapana ya nchi na watu wake.....!!

Bunge haliko huru kabisa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba. Vivyo hivyo mahakama ukiachilia mbali Jaji na Hakimu mmoja mmoja....

Executive hujiamulia tu mambo ikiwemo kupanga matumizi ya fedha za umma huku kazi hiyo kikatiba na kisheria ikiwa ni ya Binge la wananchi na hakuna wa kuuliza....!!

MWISHO, namalizia tena kwa kusema, hakuna mwenye ishu na miradi mikubwa ya maendeleo. Na in fact, hakuna asemaye miradi hii ni mibaya na kwamba, haina faida yoyote kwa nchi na watu wake wa sasa na wa vizazi vijavyo vya miaka inayokuja....

The problem ni namna inavyotekelezwa kwa maamuzi ya mtu mmoja aitwaye RAIS......

Na yeyote anayejaribu kuhoji, kukosoa au kushauri anaweza kujikuta amepoteza maisha ama kupotea kusikojulikana....

Ndipo hapo watu tunajiuliza, kulikoni? Kuna nia njema kweli kwenye hii miradi? Na je, ni miradi ya wananchi kweli au ni ya viongozi tu kupigia fedha za umma? Kwanini CAG anaposema kinyume na matarajio yao kuhusu projects hizi wahusika wanang'aka na kutaka hata kuua? Kulikoni????

Na mara nyingi sana miradi inayoanzishwa kwa njia za ulaghai laghai na ujanja ujanja wa wizi siku zote huwa siyo sustainable na hata ukamilikaji huwa ni wa taabu sana....

Mfano halisi ni mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.....

Kwa kuwa ulianzishwa kilaghai, ndo hivyo tena umeishia njiani....

Who knows, kwamba, miradi kama ya SGR na Bwawa la uzalishaji umeme la Stiglers Gorge haitakuja kukumbwa na dhahama kama ulivyoikumba Bandari ya Bagamoyo??

Are we sure kuwa aliyeanzisha projects hizi Bwana Pombe Magufuli atakuwepo kesho au keshokutwa?

Anaweza kufa ama asiwe Rais tena in a just a near future. Who knows??

Na akiondoka kwa namna yoyote ile, maana yake atakuwa ameondoka na SGR yake kama Kikwete alivyoondoka Bandari ya Bagamoyo, Atakuwa aneondoka na Chato International Airport kama ile ya Mobutu Seseseko wa Zaire....!!

Inakuwa ni nini hiyo?

Ni matumizi mabaya na ya hovyo ya fedha za umma and in fact lazima waliohusika wawe answerable in future....

Tuache mifumo itende kazi yake. Maamuzi ya mtu mmoja tu katika nchi bila kuwa CHECKED and BALANCED ni janga kwa taifa....

Ndivyo ilivyo katika TZ yetu leo
 
Back
Top Bottom