Nimefika leo asubuhi mji wa madini Shinyanga nikataka supu tu wala si chochote wanakwambia supu bila chapati hawauzi.
Ina maana hata ukitaka wali dagaa watakwambia dagaa ni wa ugali tu
Wana limit ya supu na ukitaka zaidi hawa kupi.Ni rahisi sana nunua vyote kwa bei ya vyote kula unachotaka bakiza kingine hapo ni lack of communication mtu ameshapanga kwamba chapati kadhaa supu kadhaa ndio anapata faida (kiduchu) akicheza na mahesabu imekula kwake; Ukizingatia bosi hajampangaia bei ya supu peke yake (costing ya kipimo kuona ni vipi ata-break even) na sio kubaki na machapati yakamchachia
Kuna Buffet sehemu vinywaji bure unanunua chakula sidhani kama unaweza kuwaambia nimekuja kunywa soda yangu ya bure
Huenda hicho kiwango cha supu tuseme kwa bei ya buku ni hasara, yaani supu wanaweka tu kuuzia chapati ambazo kwa mbili kwa jero jero huenda ndio kuna faida tamu; yaani hapo supu wanaleta tu kwa hio buku huenda wanapoteza 200/= hivyo imekuja kabisa imepimwa ili iweze kuuza chapati zilizopo....Wana limit ya supu na ukitaka zaidi hawa kupi.
Yani supu ya 2000 yenye nyama nne lazima chapati mbili.
Bora kwenye migahawa....Mimi hakuna kero naipata kwa kwenda saluni na kuombwa namba ya Simu na wafanyakazi za hizo saluni...!!! Kisha wanaanza kukuomba wakupatie huduma ambazo hukuzitaka Wala kuonyesha dalili ya kuzitaka....mara hooo sauna....mara ooo! 'meseji'....yaani kero tupu!!!Ina maana hata ukitaka wali dagaa watakwambia dagaa ni wa ugali tu
Ni kweli siyo kila mteja anapenda chapati kuna watu wengine siyo wapenzi wa Chapati, Labda mteja alipotoka ameshakula kwahiyo anataka Soup tu.Ndio maana unakuta mtu anafanya biashara ile ile miaka tele bila mabadiliko wala mafanikio sababu ya ukiritimba aliojiwekea
Mkuu ni sehemu nyingi ata ukienda Dukani kununua nguo utakuta muuzaji anakuonyesha uchukue nguo wakati hujaipenda na bado unaendelea kuchagua. Wafanyabiashara wanataki wamuache mteja achague bidhaa anayoipenda bila kumuingilia kila mteja ana aina zake za nguo, Viatu. Na mteja anajua kwa kuingalia nguo hii itanitosha.Bora kwenye migahawa....Mimi hakuna kero naipata kwa kwenda saluni na kuombwa namba ya Simu na wafanyakazi za hizo saluni...!!! Kisha wanaanza kukuomba wakupatie huduma ambazo hukuzitaka Wala kuonyesha dalili ya kuzitaka....mara hooo sauna....mara ooo! 'meseji'....yaani kero tupu!!!