Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amejikuta akitokwa na machozi wakati akimsikiliza Makazi wa jijini Arusha ajulikanae kwa jina la Respis Brasius ambaye amekiri kwamba angekunywa Sumu kama asingesikiliza Hotuba yake ya Bajeti ya Mwaka 2024/2025 wakati akiwasilisha Bungeni Dodoma tarehe 27 Mei 2024.
Mkazi huyo alifikia hatua hiyo baada ya kuteseka kwa muda mrefu akitafuta haki yake bila mafanikio kwa kuwa alivunjiwa nyumba yake pamoja na watu wengine katika mtaa wa Unga Limited jijini Arusha.