Migomo Kariakoo: Serikali kuendelea kulea utamaduni wa kulinda wahalifu utakutokea puani

Migomo Kariakoo: Serikali kuendelea kulea utamaduni wa kulinda wahalifu utakutokea puani

Doslamari

New Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
4
Reaction score
1,499
Ni mara ya 2 wanaoitwa wafanyabiashara wa Kariakoo kugoma ndani ya muda mfupi. Baada ya ule mgomo wao wa kwanza tukaanza kuona migomo Iringa, Mwanza na maeneo mengine.

Migomo yote ni wafanyabiashara kukataa maelekezo halali ya serikali ikiwa pamoja na kutotaka mfumo wa wazi unaobana wizi na ukwepaji kodi.

Leo ni mara ya pili wamegoma tena, sababu kikosi kazi kimerudi. Kwanini mtu asiye mhalifu aogope uwepo wa polisi mitaani, mimi mlipa kodi mwaminifu nitaogopaje uwepo wa kikosi kazi km mm siyo mhalifu namba moja? Nilitegemea wafabiashara wazalendo wangeipa hicho kikosi ushirikiano mkubwa. Badala yake wahalifu wameungana.

Ni ukweli hakuna anayependa kulipa kodi maana hupunguza kipato chako, mnyonge pekee ambaye hawezi kwepa kodi nchi hii ni mfanyakazi aliyeajiriwa, huyu hukatwa kodi kabla ya kupata mshahara wenyewe.

Rais huhitaji compromise na wezi wa mapato ya serikali vinginevyo utatujenga Taifa la hovyo, Taifa lisilotawalika, lisiloheshimu wala kuitambua serikali, nimesikitika sana kumwona kijana moja alivyomjibu mkuu wa mkoa, nilitamani afufuke Magufuli, nilitamani Kagame awe Rais wa nchi hii.

Rais kama huwezi kutumia madaraka ya urais bora uachie ngazi. Nchi yetu ni kubwa sana, hilo ni kundi dogo sana wasituharibie nchi yetu na nina uhakika pale hakuna wa kukupigia kura, kwanza hawawezi kwenda kupanga foleni siku ya kupiga kura.

Rais tulindie heshima ya nchi yetu kikosi kazi iache ìendelee kufanya kazi yake, unawapa wakati mgumu sana wasaidizi wako kutekekeleza majukumu yao.

Pia soma
Tetesi: - Wafanyabiashara Kariakoo kugoma muda wowote kutokana na madai yao kupuuzwa

Kwa Mtazamo wangu

TATIZO LA KARIAKOO NI ZAIDI YA WAFANYABIASHARA,WACHUUZI..LETS BE SERIOUS.

Tatizo la kariakoo haliwezi Kwisha ikiwa total supply chain ya mizigo inayouzwa kariakoo isiporekebishwa au kudhibitiwa kupitia maamuzi magumu na kutooneana haya wala aibu..

Bidhaa nyingi zinazouzwa kkoo zinaingizwa (Imported) toka China,India,Uturuki,Thailand,Vietnam,Zambia,Uganda,etc..Mfumo wa uingizaji na ulipiaji kodi wa mizigo husika ndio mzizi wa shida na tatizo lililopo na litakalokuwepo..

Cartel inayoratibu Logistics na supply chain ya mizigo ya wafanyabiashara wa karikoo isipodhibitiwa kila nyakati tutaona fukuto na migomo isiyohitaji siasa Bali utashi wa maamuzi magumu kudhibiti wahujumu uchumi tunaowalinda..

Mathalani,Mfanyabiashara akiagiza mzigo wa viatu Kwa kontena na kulipa ushuru stahiki kisha kuwa na nyaraka zote Za kikodi (Import duties,Port charges,Wharfage,VAT) inamgharimu milioni 45….NOTE:- Ila akiagiza mzigo huo huo kwa kutumia Logistics Cartels inamgharimu Milioni 15 tu pasipo nyaraka zozote lakini Ana uhakika wa kufikishiwa mzigo dukani au warehouse kwake pasipo usumbufu..

Sasa wale wafanyabiashara waliokuwa wakikomaa na kufuata taratibu stahiki wamejikuta wakishindwa kushindana ktk soko na kufirisika ama kufa kibiashara sababu ya ughali wa bidhaa dhidi ya wale wanaotumia Logistics Mafia..

On the other hand wanaotumia huduma za logistics cartel au mafia inawawia Vigumu sana kufanya compliance za kikodi sababu ya kukosa nyaraka muhimu kussuport mapana ya stock zao..Mauzo yao,returns zao..Hapa ndio kwenye shidaa haswaa…Wengi wana stock kubwa kuliko vielelezo vya manunuzi ya stock husika..Wamegeuka wachuuzi..Wanaouza ambacho hawana nyaraka Za wametoa wapi..SHIDA.

Logistics Cartel/Supply chain Mafia:-Ni kundi hatari lenye nguvu kupitia wanasiasa wakubwa waliopo na wastaafu..Wana ukwasi mkubwa na umaarufu mkubwa ktk Kiwango cha kuogopeka na Wakubwa wa TRA,Polisi,Etc..Wana nguvu mnooo ya kufanya wakubwa ktk mamlaka Za kodi watumbuliwe,Wafanyakazi wahamishwe,Wawe demoted..Wapate Stroke..Nina hakika hata CG wa TRA anawaogopa..Hana la kuwafanya..Inasemekana baadhi ya viongozi ni marafiki wakubwa..

Cartels hizi zimehodhi Supply chain Za uagizaji bidhaa,usafirishaji,Ulipaji kodi,Udanganyifu (under declaration&Falsa Declarations),Uzungushaji mizigo (Taarifa Za kampuni Za tracking devices Za mizigo ya transit zina mengi)..Wanamiriki makampuni ya uagizaji,Usafirishaji,Bonded Warehouses,ICD’s,CFS..yaani acha tu..

Kwa hakika tunapoteza kodi nyingi sana zinazoingia mifukoni mwa wachache tunaowaimbia mapambio ya utajiri na ubilionea huku wachache wakikamuliwa hata kuzirai kibiashara..Bila maamuzi magumu na dhabiti tutaendelea kukwama na kuumiza wasiostahili..

Tukiamua Tunaweza..Viongozi wenye dhamana Simameni kwenye haki na ukweli..
 
Hao ni kucheza nao hivyo hivyo, wakigoma serikali wanakaa nao chini, wanarudi kufunguwa maduka, simply wapo "bored" tu.

Chalamila kawaambia maneno mazuri sana leo, kawaambia wanogoma watalindwa na serikali na wasiwaingilie wasiogoma nao pia wanalindwa na serikali. Kwa ufuipi kawaambia wanaogoma wagome, wasiogoma wasigome, hasara ni kwa wenye kugoma, watagoma na kodi watalipa.

Tatizo nini, hata mama aingilie haki za watu za kugoma? Wagome tu lakini wasitishe au kulazimisha wasiotaka kugoma.

Kwa mama, ukitaka kugoma, goma, utasikiliswa, ukitaka kufanya maandamano fanya utasikilizwa.

Hivi maandamano yua chadomo yameishia wapi? Si unaona falsafa ya maa ya kuwawachia wafanye maandamano, kila mtu kabaki shwari.

Mama Samia apewe hongera sana kwa mageuzi ya uongozi anayoyafanya.
 
Cartel unayoongelea ni gsm sasa jiulize juanzia yamga mpaka kina mwana fa, mpka kwa mkubwa unaweza kupambana na gsm. Hakuna anayeweza. Wao ndio wanapanga nani awe port manager, nani anafaa bandarini na long room
 
Hapo ndipo lilipo tatizo.

Kuna mafia wanaoingiza bidhaa nchini Kupitia be andari hiyo hiyo na hawalipi hiyo VAT,

Ndio hao wanaouza Kwa wafanyabiashara, sasa haesabu lazima zichengane.

TULETEENI DIKTETA MWINGINE TAFADHALI 🙏
 
Hao ni kucheza nao hivyo hivyo, wakigoma serikali wanakaa nao chini, wanarudi kufunguwa maduka, simply wapo "bored" tu...
Ill call it bullshit, i thought ungekuja na analysis ya kitaalam of nn hasa mzizi wa tatizo and how to solve it, seems you have no idea na si ajabu huna hata biashara yoyote, umeandika blah blah tu

Amna mfanya biashara anakuwa bored so watengeneze drama, no body has time for that shit. Hawa watu wana serious issue need to be addressed.

This is not a game, chalamila hili ni beyond his paygrade, maneno na vitisho havisaidii
 
Hao CARTEL ni wafadhili wa Ccm.

Ndio wanaoiweka Ccm madarakani wakishirikiana na vyombo vya dola.

Serikali / Ccm haiwezi kuwashughulikia Cartels, ndio maana inakandamiza wafanyabiashara.
 
Kwa Mtazamo wangu

TATIZO LA KARIAKOO NI ZAIDI YA WAFANYABIASHARA,WACHUUZI..LETS BE SERIOUS.

Tatizo la kariakoo haliwezi Kwisha ikiwa total supply chain ya mizigo inayouzwa kariakoo isiporekebishwa au kudhibitiwa kupitia maamuzi magumu na kutooneana haya wala aibu..

Bidhaa nyingi zinazouzwa kkoo zinaingizwa (Imported) toka China,India,Uturuki,Thailand,Vietnam,Zambia,Uganda,etc..Mfumo wa uingizaji na ulipiaji kodi wa mizigo husika ndio mzizi wa shida na tatizo lililopo na litakalokuwepo..

Cartel inayoratibu Logistics na supply chain ya mizigo ya wafanyabiashara wa karikoo isipodhibitiwa kila nyakati tutaona fukuto na migomo isiyohitaji siasa Bali utashi wa maamuzi magumu kudhibiti wahujumu uchumi tunaowalinda..

Mathalani,Mfanyabiashara akiagiza mzigo wa viatu Kwa kontena na kulipa ushuru stahiki kisha kuwa na nyaraka zote Za kikodi (Import duties,Port charges,Wharfage,VAT) inamgharimu milioni 45….NOTE:- Ila akiagiza mzigo huo huo kwa kutumia Logistics Cartels inamgharimu Milioni 15 tu pasipo nyaraka zozote lakini Ana uhakika wa kufikishiwa mzigo dukani au warehouse kwake pasipo usumbufu..

Sasa wale wafanyabiashara waliokuwa wakikomaa na kufuata taratibu stahiki wamejikuta wakishindwa kushindana ktk soko na kufirisika ama kufa kibiashara sababu ya ughali wa bidhaa dhidi ya wale wanaotumia Logistics Mafia..

On the other hand wanaotumia huduma za logistics cartel au mafia inawawia Vigumu sana kufanya compliance za kikodi sababu ya kukosa nyaraka muhimu kussuport mapana ya stock zao..Mauzo yao,returns zao..Hapa ndio kwenye shidaa haswaa…Wengi wana stock kubwa kuliko vielelezo vya manunuzi ya stock husika..Wamegeuka wachuuzi..Wanaouza ambacho hawana nyaraka Za wametoa wapi..SHIDA.

Logistics Cartel/Supply chain Mafia:-Ni kundi hatari lenye nguvu kupitia wanasiasa wakubwa waliopo na wastaafu..Wana ukwasi mkubwa na umaarufu mkubwa ktk Kiwango cha kuogopeka na Wakubwa wa TRA,Polisi,Etc..Wana nguvu mnooo ya kufanya wakubwa ktk mamlaka Za kodi watumbuliwe,Wafanyakazi wahamishwe,Wawe demoted..Wapate Stroke..Nina hakika hata CG wa TRA anawaogopa..Hana la kuwafanya..Inasemekana baadhi ya viongozi ni marafiki wakubwa..

Cartels hizi zimehodhi Supply chain Za uagizaji bidhaa,usafirishaji,Ulipaji kodi,Udanganyifu (under declaration&Falsa Declarations),Uzungushaji mizigo (Taarifa Za kampuni Za tracking devices Za mizigo ya transit zina mengi)..Wanamiriki makampuni ya uagizaji,Usafirishaji,Bonded Warehouses,ICD’s,CFS..yaani acha tu..

Kwa hakika tunapoteza kodi nyingi sana zinazoingia mifukoni mwa wachache tunaowaimbia mapambio ya utajiri na ubilionea huku wachache wakikamuliwa hata kuzirai kibiashara..Bila maamuzi magumu na dhabiti tutaendelea kukwama na kuumiza wasiostahili..

Tukiamua Tunaweza..Viongozi wenye dhamana Simameni kwenye haki na ukweli..
Ukinunua bidhaa bila supporting documents na unauza bila documents lazima TRA utawaona majambazi ,wahuni,na kila jina baya .wakati TRA ukienda nao sheria kwa sheria ,document kwa document wanakupongeza unakuwa rafiki
 
Shida ya Kariakoo inaanzia pale mizigo inapoingia kwani kuna wafanyabiashara wengi huagiza mizigo kwa kutumia mtu mmoja na mzigo ukifika unatolewa kwa jina la huyo myu mpaka kwenye stoo zao. Sasa akija uza anaonekana kazua mzigo mwingi kuliko alionunu na ndiyo maana hata risiti hawataki kutoa.

Kama unakumbuka issue ya mgomo wa mwanzo walikuwa hawataki stoo zao zijulikane wala kuulizwa risiti za efd. Mimi wito kwa serikali na waziri wa Fedha pamoja na Viwanda na Biashara sheria lazima ifate mkondo wake. Kesho wataibuka la lingine sababu imekuwa ni mchezo kwao.

Well kuna vitu kweli vya msingi nipo nao nawasapoti kama la machinga kutafutiwa nao utaratibu wa eneo na walipe nao kodi. Unakuta mtu anasema ni machinga lakini jeki za gari ,sub woofer huyo anapaswa naye kulipa kodi. Wachina ni kweli nipo nao hoja inamashiko kuwa wawe na biashara kubwa ambazo zitatengeneza ajira na mapato makubwa kwa serikali maana kutakuwa na kodi ya mapato, kodi katika ajira.

Kariakoo ukiingia hata unacholipa ukidai risiti hawakupoi au wakikupa ya bei ya chini tofauti na ulicholipa. Huu ni wizi kwa serikali na wito wangu Mhe Raisi usilegeze mama yetu watakuchezea hawa.

Imekuwa desturi yao kutupia lawama mara utasikia TRA mara sijui halmashauri sasa kama hao tra wanaweka watu kukagua risiti shida ipo wapi kama unatoa hizo risiti. Shida ni kwamba ni wajanja hawatoi na anaweza toa risiti ikwatumika kusindikiza mizigo hata 10 kwa siku mtu anapewa kwenda na rsiti kuvusha mizigo anarudi nayo na akitokea mteja mwingine anaenda tena anarudi nayo ndiyo mchezo mkubwa. Nimeshafanya tafiti sana kariakoo michezo yao ni hiyo sana.

Kodi stahiki zikilipwa wakati wa uingizaji bidhaa huwezi Ona TRA wakihangaika sana..

Real importers wakihusika na michakato yote ya uagizaji na ulipaji kodi Hakuna shida ya kutoa risiti

Tatizo mtuma mzigo ndio Mpokea mzigo..Ndio mtoa mzigo (Clearing Agent),Ndio ICD (Bandari kavu),Ndio mhifadhi,,Ndio msafirishaji ..muagizaji halisi anabaki kuwa muuzaji pekee..Pasipo kuwa na nyaraka zozote
 
Ukinunua bidhaa bila supporting documents na unauza bila documents lazima TRA utawaona majambazi ,wahuni,na kila jina baya .wakati TRA ukienda nao sheria kwa sheria ,document kwa document wanakupongeza unakuwa rafiki
Haswaaa

Mzizi na shina la tatizo hatudiri nalo Bali matawi..

Penye nia pana njia
 
Back
Top Bottom