Hakuna kundi hatari na lisilotabirika katika nchi yoyote kama wanafunzi wa elimu ya juu. Na hakuna watu ambao wanatakiwa kudhibitiwa, kugawanywa na kukwaza inavyowezekana kama kundi hilo. Kama nchi yoyote inautawala wa kimabavu, wa kiimla au unachezea sheria na Katiba ni kwa manufaa ya watawala mara zote kudhibiti mwamko katika elimu ya juu.
Hii ni kweli Ulaya, Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali, Marekani, na hata Afrika ya Kusini.
Tunaweza kuwalaumu hawa vijana n.k lakini ukweli utabakia pale pale ambapo sisi wengine tumeuimba miaka nenda rudi, kuwa kuna tatizo katika dhana nzima ya kuchangia elimu ya juu na zaidi ya yote mfumo mzima wa utoaji wa mikopo umeharibika sana. Lakini tatizo kubwa zaidi liko katika serikali iliyoko madarakani.
a. Kwa miaka nenda rudi serikali imeshindwa kubuni na kutekeleza mfumo mzuri, wa usawa na wa haki wa kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu ya juu.
b. Serikali bado inafikiri ni "nchi iliyoendelea" ambapo elimu ya juu inatolewa kama nchi hizo badala ya kuona kuwa kama Taifa linataka kupiga hatua ni lazima tuwekeze kwenye elimu ya juu tena kwa makusudi.
c. Kwa nchi kama ya ya kwetu hatuwezi kuendesha vyuo vikuu kwa mtindo tunaofanya hivi sasa; kunahitajika mabadiliko makubwa ya kimtazamo na utendaji. Unapofikia serikali inawarudishwa vijana walioko Chuo Kikuu wakisomea shahada mbalimbali za sayansi ati kwa vile hawakujaza "fomu kwa usahihi" ujue umefika mahali pabaya. Hadi hivi sasa hakuna kiongozi yeyote Tanzania ambaye ameweza kukaa chini na kusema "hili ndilo tatizo, na options zetu ni hizi, na hivi ndivyo tutakavyofanya". Wote wanajaribu kulazimisha vitu alimradi waonekane wana nguvu. Hatutatui matatizo tunajaribu kuyafunika ili yasitutatize.
c. Wengine tulishapigia kelele bodi ya mikopo ilivyo corrupt na kuonesha mifano lukuki. Guess what? Watu wale wale walioboronga bado wapo pale pale wakiendelea kuboronga na wakizidiwa wanafunga vyuo.
Serikali haina lengo, nia, wala sababu ya kutatua suala la elimu ya juu. Hivyo ndivyo ilivyo. Mtazunguka tu lakini ukweli unabakia na serikali kuwa kwa karibu miaka 20 hakuna msomi aliyeweza kukaa chini na kusema "we have to solve this problem once and for all" na kila mwaka tutaendelea kuwa na hii migomo, tishio la serikali, chuo kufungwa/wanafunzi kufukuzwa, kufunguliwa, kusoma kidogo, migomo, tishio la serikali, chuo kufunguwa (wanafunzi kufukuzwa), kufunguliwa and and the stupid circle of stupidity - M.M. Original keep on spinning..