Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne



Ndo ushangae sasa First lady,,, na sio kwamba hwajai wanajua sana ila ndo ivo wakishatamalaki kwenye mshangingi yao, haya mambo mengine wanayaona madogo madogo

mapambano yanaendelea na ipo siku kitaeleweka tu....si umesikia huko mashariki ya mbali wanafunzi wa chuo kikuu walishamwondosha raisi madarakani?
 

kua na watu wengi si ndo vzr nguvu kazi inaongzeka na uzalishaji hali kadhalika????
 

First Lady
Sio lazima zifike siku tatu, hata nusu saa inatosha kufunga chuo endapo kuna hatari au usalama haupo. Siku tatu ni za 'kumba na kukaa chini' na si za 'kutupa mawe'
 
tanzania haiwezi kuwakopesha wanafunzi wote wa elimu ya juu.
mimi hapa kidogo napata tabu maana kama watu wanaweza kula hela zetu wanautajiri wa kupindukia majibu ni yakishenzi kuanzia mwanzo mpaka mwisho.. Unategemea nani atakaakimya na kuan=mini nchi haiwezi kulipia wote.... Viongozi wanautajiri wa kutisha halafu tuamini tu serikali haiwezi?????? Na tukiendelea kukaa kimya mabadiliko ya maendeleo yatakuja ln??? Nawaunga mkono watoto kwa mgomo!!!
 
Haya Tena... Nakumbuka Siku iliyozama na kupinduka Meli ya MV Bukoba, palikuwa na mgomo wa wanafunzi pale UD na siku hiyo tulikwenda mpaka ofisi ya Wizara ya Elimu ya Juu - pale mtaa wa Jamhuri. Jinsi yale maadamano ya AMANI yalivokuwa "contained" na polisi sitaweza kusahau!!!!!

Nadhani kufunga Chuo Kikuu kwasababu ya mgomo ni zaidi ya "divide and rule", yawezekana kuwa wale waliokuwa madaraka
- Ni waoga sana
- Ni wavivu wa kujadili na wasiojiamini
- Ni watu wenye jaziba (si wavumulivu)
- Ni watetezi wa "siasa" na watekelezaji wa "sera" za wakubwa wao
- Ni walevi wa madaraka kiasi cha kupoteza fahamu na kumbukumbu za walikotoke (Magembe and Co)
- Ni wabinafsi na wasiopenda maendeleo ya watoto wa wa-Tz wengine (watoto wa Wakubwa walio wnegi wanasoma inje ya inji)
- Ni vilaza
- List inaendelela

Siku moja watapinduliwa na hawa hawa wanaowaletea FFU kuwavurumisha na hiyo siku siyo mbali... Wale wataalamu wa Physics wanafundisha kuwa "ukivuta sana mpira ukapitiliza mpaka "elastic limit" matokeo yake ni kuwa mpira huo upata hali mpya ya kiumbo na uwa ume-under go "permanent strain"!

Hawa vijana wakifikia "permanent strain" siyo tu vyuoni hapatakalika bali hata mitaani hakutakalika! Tutakuwa tumewadilisha umbo na sura na natumaini na "intelect" na watakuwa .... MAJAMBAZI SUGU.... Ambao kwao kila kukicha watakuwa wanafikiria kulipiza kisasi kwa waliowasababishia wao kuwa na umbo na sura hizi na eventually tutakutana na "Laurent Nkunda" - "LIVE" mitaani kwetu Sinza!!!! WAIT and SEE
 
Sera ya kuchangia huduma - afya, elimu nk, ilianza 1992. Kwa afya, wanaochangia ni masikini tu wanaokwenda kutibiwa amana, temeke, na mwananyamala. Wakubwa wanaokwenda kutibiwa hata mafua ngambo wanalipiwa na kodi za wanyonge.

Haya, kama tangu 1992 kuna kuchangia elimu, ni wangapi waliomaliza vyuo vikuu tangu 1995 wameanza kulipia. Je hiyo sera ya kuchangia elimu tangu 1992 imebadilika kiasi gani kwa kiwango, madaraja ya kufaulu, na uwezo! Wa mwanafunzi nk.

Nadhani kuiga kwingi tutatufikisha pabaya. Tunawaiga wamerikani na waingereza wakati hali zetu za kiuchumi ni tofauti kabisa. Sijui prof. Maghembe alichangia kiasi gani hadi kupata phd! Nadiriki kusema watawala wetu wote, kuanzia rais wa nchi yetu, walisoma "bure". Sasa kwa nini wanakazania hii suala la kuchangia elimu wakati nchi ilipokuwa haija anza kuchimba madini elimu ilikuwa bure!!

Mungu atusaidie wadanganyika.

Macinkus
 
...kwamba kuna nguvu kubwa ya chama kimoja cha siasa ndio natamani kujua hapo!ufafanuzi tafadhali kwa mwenye taarifa
 
Alafu mnasema mnataka kushindana kitaaluma na wenzenu.Hawa jamaa sijui kama wanamalizaga silabasi zao na kama wanamaliza basi wanalipua ukilaza unaanzia hapo.

Nilisikia UDSM kipo Top 10 ya vyuo bora Afrika......!!!!
 
Alafu mnasema mnataka kushindana kitaaluma na wenzenu.Hawa jamaa sijui kama wanamalizaga silabasi zao na kama wanamaliza basi wanalipua ukilaza unaanzia hapo.

Nilisikia UDSM kipo Top 10 ya vyuo bora Afrika......!!!!

Kwa kufunga mara kwa mara kinachukua nambari 1!!! Na hichi si kitu cha kujivunia hata kidogo.
 
Unajua nchi hii ni kama kichwa cha mwendawazimu,bodi ya mikopo wakati imeanzishwa kwa mara ya kwanza intake iliyoingia wakati bodi hii ndiyo inaanza kazi waliwapatia wanafunzi mikopo ya elimu ya juu kwa 100% tena kwa sifa rahisi tu;ambayo ilikuwa kwa yeyyote aliyepata admission chuoni alikuwa anaruhusiwa kupata mkopo.Mimi nilikuwa katika chuo kimojawapo Dar es salaam.
Huwezi kuamini mpaka wanafunzi wa Diploma baadhi yao waliopenda kujilipua walipata mikopo,waliomaliza miaka mmoja mpaka miwili na walikuwa mitaani walipata pia.
Mwaka uliofuata tukaanza kuletewa tena hadi mpya halafu ngumu kueleweka;kama ilikuwa ni kufanya majaribio basi wangechukua vyuo viwili ama vitatu kwaajili ya pilot study kuliko ku-introduce kwa watu wote utaratibu ambao hauna uhakika nao.
Ninavyojua mimi katika kutumia elimu unapofanya kitu kama hiki hutakiwi kubahatisha;hivyo basi mamlaka husika ndani ya serikali zimefanya uzembe wa kupindukia;binafsi wahusika hawastahili hata chembe ya msamaha katika hili.
 
Unajua nchi hii ni kama kichwa cha mwendawazimu,bodi ya mikopo wakati imeanzishwa kwa mara ya kwanza intake iliyoingia wakati bodi hii ndiyo inaanza kazi waliwapatia wanafunzi mikopo ya elimu ya juu kwa 100% tena kwa sifa rahisi tu;ambayo ilikuwa kwa yeyyote aliyepata admission chuoni alikuwa anaruhusiwa kupata mkopo.Mimi nilikuwa katika chuo kimojawapo Dar es salaam.
Huwezi kuamini mpaka wanafunzi wa Diploma baadhi yao waliopenda kujilipua walipata mikopo,waliomaliza miaka mmoja mpaka miwili na walikuwa mitaani walipata pia.
Mwaka uliofuata tukaanza kuletewa tena hadithi mpya halafu ngumu kueleweka;kama ilikuwa ni kufanya majaribio basi wangechukua vyuo viwili ama vitatu kwaajili ya pilot study kuliko ku-introduce kwa watu wote utaratibu ambao hauna uhakika nao.
Ninavyojua mimi katika kutumia elimu unapofanya kitu kama hiki hutakiwi kubahatisha;hivyo basi mamlaka husika ndani ya serikali zimefanya uzembe wa kupindukia;binafsi wahusika hawastahili hata chembe ya msamaha katika hili.
 
...kwamba kuna nguvu kubwa ya chama kimoja cha siasa ndio natamani kujua hapo!ufafanuzi tafadhali kwa mwenye taarifa

hakuna chama chochote cha siasa kinachogharimia migomo chuo kikuu. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wanatumia kisingizio hiki kwa muda mrefu ili kuweka sura na mtu wa kulaumu kwenye migomo ya wanafunzi chuo kikuu.
 

Kama kuna maelefu au mamilioni hawalalamiki inawahusu nini wanafunzi wa UDSM?? Suala la mtu kulalamika anapoonewa ni lake binafsi na halifungamani na matatizo ya mtu mwingine.

Lakini kutokana na mchango wako hapo juu napata shida kukuelewa na kwa ufupi nasikia hasira sana. Nashawishika kuwa wewe na watu wenye mawazo kama hayo hawakupitia vyuo vyetu hivi karibuni! Kama kweli ungekuwa umepita Mlimani au chuo kingine cha umma katika miaka 10-15 iliyopita usingetoa mawazo kama hayo.

Kwanza, kazi ya kutoa huduma za jamii ni ya serikali. Ni wajibu wake na siyo ombi! Serikali inalazimika kutoa elimu (basic) na matibabu n.k kwa wananchi wake. Na wajibu wa wananchi ni kulipa kodi. Nukta. Sasa hapa kodi tunalipa (labda wale ambao hawalipi) na kwa hiyo ni wajibu wa serikali kutoa elimu kwa wananchi wake. Pale ambapo serikali haina uwezo na wananchi wanaona kuwa kweli serikali haina uwezo basi wanaweza kuchangia. Kwa hapo kila mtu atakuwa anaridhika kuwa serikali haina huwezo ila pia haina matumizi mengine ya kipuuzi, kama vile magari ya gharama. Kwa nini wasiidai serikali yao iwape elimu kama wanaona serikali inafanya matumizi ya gharama kubwa yasiyo ya lazima??

Pili, sina hakika kama tunajua jinsi bodi ya mikopo inavyofanya kazi. Wanafunzi wameomba kukopeshwa 100% na si kupewa elimu ya bure. Na kama serikali inataka kutoa pungufu ya 100% basi iwe na vigezo vya msingi. Huu utaratibu wa kishenzi wanaotumia sasa hakuna mtu anaweza kuulewa na pia hauvumiliki. Na hapa watu wanaona kuwa wakubwa hawajali kwa sababu watoto wao wanasoma nje. Kwa wanafunzi, ni afadhali chuo kifungwe kuliko kufanyiwa usanii. Kuna kosa gani hapo? Kwanza wangeweza hata kukichoma chuo moto tukose sote! Nisingewalaumu kwa hilo.

Tatu, toka mwanzo sera ya elimu ililenga kuwanufaisha zaidi watoto wa masikini kwa kuwataka watu wenye uwezo walipie zaidi elimu ya watoto wao. Kwa hiyo hakuna mtu anayedai wote wasomeshwe bure ingawa ni haki yao kikatiba kupewa elimu na serikali yao. Kinachoonekana sasa, hii sera inawakomoa zaidi watoto wa masikini ambao hata kulipa 20% hawawezi. Katika hili sijui kama kuna hoja ya kuitete hii sera. Pia kwa watu wanaofuatilia, wanafunzi waliipinga toka siku inaanzishwa kwamba italeta ubaguzi na imekuwa hivyo toka siku ya kwanza ya utekelezaji wake!

Nne, migomo kwa vyuo vyetu ndiyo lugha pekee ambayo watawala wanaisikia, kuielewa na kuiitikia. Hakuna lugha nyingine. Wale ambao wamepitia vyuo wanalijua hili. Kwa mtu ambaye hajui hali na jinsi vyuo vinavyoendeshwa aulize tu. Sidhani kama JF ni uwanja wa kutoa maoni ambayo yanafanana kama hotuba wa Waziri J4 au Msemaji wa wizara (press secretary).
Hata hivyo kama wizara au msemaji wake anataka kutoa tamko alete tu kama thread inayojitegemea na si kuchomekea kwenye thread zetu ambapo tunatumia muda mwingi na akili zetu kutoa maoni yenye lengo la kujenga nchi yetu!
 
Alafu mnasema mnataka kushindana kitaaluma na wenzenu.Hawa jamaa sijui kama wanamalizaga silabasi zao na kama wanamaliza basi wanalipua ukilaza unaanzia hapo.

Nilisikia UDSM kipo Top 10 ya vyuo bora Afrika......!!!!

Pamoja na matatizo yote haya, wanafunzi wa chuo kikuu wanamaliza syllabus na most of them ni very smart.
 

Nani kakwambia wanamkopa mtu? Unaweza kutofautisha serikali na mtu?? Mtu gani katika nchi hii anakusanya kodi za wananchi?? Please soma maoni yangu katika jibu kwa Masanja.
You don't have to say anything if you are not well informed about the issue. Just read others' views or ask. Ignorance is not an offence.
I just can't stand some direct mispresentation and malice on very clear issues!
 
Kwa mtazamo wangu,
Mi naona swala la kuchangia si baya, shida ni ule ubaguzi unao fanywa na bodi ya mikopo! Pale ambapo mapacha ambao wote ni yatima mmoja anapata mkopo asilimia 100 mwingine asilimia 40, Pale ambapo mtoto wa kigogo mkopo wake ni asilimia mia moja wakati wa kalimanzira ni asilimia 40!

Lakini pia hoja nyingine ni kwamba ili uweze kupima uwezo wa mwanafunzi kwa level ya chuo kikuu, lazima wote wawe katika mazingira sawa. Yaani wana uhakika wa kula kwenda darasani na mahitaji ya muhimu bila kuwa na msongo wowote juu ya upatikanaji wa vitu hivyo, kitendo cha kuwapa wengine asilimia 40, na kuwalazimu kutumia hela yao ya kula kulipa karo na kuishi kwa kunywa uji, unakuwa tayari umeondoa dhana nzima ya mazingira sawa!

Kwa msingi huu, mi naona bora wote wakopeshwe asilimia mia moja ili kulinda msingi huo.

Cha kushangaza wengine tulio maliza siku za nyuma bodi ilisha anza kusanya marejesho ya mikopo, hizo je zinapelekwa wapi? ama ndo zinaishia mikononi mwa wajanja au nazo hazina mwenyewe? (EPA type)
Pili bodi wana uzembe wa kufatiliwa wadaiwa wengine, kwani inashangaza watu mpo ofisi mmoja, na wote mlikopeshwa, mmoja anakatwa mwingine wala!

Mwisho hilo swala la kusema kuna nguvu ya chama cha siasa ni uongo mkubwa!, madai ya vijana ni ya msingi, hii sera, na hasa utekelezaji wake chini ya watendaji dhaifu wa bodi ya mikopo ni ya KIBAGUZI na hakika ni ya kiuonevu kwa watoto wa masikini.
 
Pamoja na matatizo yote haya, wanafunzi wa chuo kikuu wanamaliza syllabus na most of them ni very smart.
Wanalipua na wawako smart wanapigwa vikumbo na vijana wa Uganda na Kenya.Au kukariri mavitabu makubwa makubwa kilo 20 ndio kuwa smart?
 
Hakuna kundi hatari na lisilotabirika katika nchi yoyote kama wanafunzi wa elimu ya juu. Na hakuna watu ambao wanatakiwa kudhibitiwa, kugawanywa na kukwaza inavyowezekana kama kundi hilo. Kama nchi yoyote inautawala wa kimabavu, wa kiimla au unachezea sheria na Katiba ni kwa manufaa ya watawala mara zote kudhibiti mwamko katika elimu ya juu.

Hii ni kweli Ulaya, Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali, Marekani, na hata Afrika ya Kusini.

Tunaweza kuwalaumu hawa vijana n.k lakini ukweli utabakia pale pale ambapo sisi wengine tumeuimba miaka nenda rudi, kuwa kuna tatizo katika dhana nzima ya kuchangia elimu ya juu na zaidi ya yote mfumo mzima wa utoaji wa mikopo umeharibika sana. Lakini tatizo kubwa zaidi liko katika serikali iliyoko madarakani.

a. Kwa miaka nenda rudi serikali imeshindwa kubuni na kutekeleza mfumo mzuri, wa usawa na wa haki wa kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu ya juu.

b. Serikali bado inafikiri ni "nchi iliyoendelea" ambapo elimu ya juu inatolewa kama nchi hizo badala ya kuona kuwa kama Taifa linataka kupiga hatua ni lazima tuwekeze kwenye elimu ya juu tena kwa makusudi.

c. Kwa nchi kama ya ya kwetu hatuwezi kuendesha vyuo vikuu kwa mtindo tunaofanya hivi sasa; kunahitajika mabadiliko makubwa ya kimtazamo na utendaji. Unapofikia serikali inawarudishwa vijana walioko Chuo Kikuu wakisomea shahada mbalimbali za sayansi ati kwa vile hawakujaza "fomu kwa usahihi" ujue umefika mahali pabaya. Hadi hivi sasa hakuna kiongozi yeyote Tanzania ambaye ameweza kukaa chini na kusema "hili ndilo tatizo, na options zetu ni hizi, na hivi ndivyo tutakavyofanya". Wote wanajaribu kulazimisha vitu alimradi waonekane wana nguvu. Hatutatui matatizo tunajaribu kuyafunika ili yasitutatize.

c. Wengine tulishapigia kelele bodi ya mikopo ilivyo corrupt na kuonesha mifano lukuki. Guess what? Watu wale wale walioboronga bado wapo pale pale wakiendelea kuboronga na wakizidiwa wanafunga vyuo.

Serikali haina lengo, nia, wala sababu ya kutatua suala la elimu ya juu. Hivyo ndivyo ilivyo. Mtazunguka tu lakini ukweli unabakia na serikali kuwa kwa karibu miaka 20 hakuna msomi aliyeweza kukaa chini na kusema "we have to solve this problem once and for all" na kila mwaka tutaendelea kuwa na hii migomo, tishio la serikali, chuo kufungwa/wanafunzi kufukuzwa, kufunguliwa, kusoma kidogo, migomo, tishio la serikali, chuo kufunguwa (wanafunzi kufukuzwa), kufunguliwa and and the stupid circle of stupidity - M.M. Original keep on spinning..
 

Mzee Mwanakijiji,

Naelekea kukubaliana nawe hapo kwenye bold. Kuanzia ule mgomo wa kupinga mapendekezo ya uchangiaji wa elimu ya juu wa mwaka 1992, kila muda fulani ukipita, wanafunzi wamekuwa wanaieleza serikali kuwa bado watanzania ambao unemployment rate ni zaidi ya asilimia 50 hawana uwezo wa kulipia mamilioni kwa ajili ya elimu ya juu.

Hali imekuwa ile ile kwa muda sasa, mwaka 2000 nikiwa mlimani, mgomo wa wanafunzi ulikuwa na almost madai yale yale ya mwaka 1992, miaka minane baada ya 2000 (miaka 16 baada ya mgomo wa mwaka 1992), wanafunzi wa mlimani wanagomea mambo yaleyale.

Ninamshauri rafiki yangu Prof Mukandala atafute njia mbadala ya kudeal na hii migomo ya wanafunzi. Suala la ubabe halielekei kumaliza hali hii. Mwaka 1992 kuna murra alifukuzwa mlimani kwa mgomo na maisha yake yakaharibiwa for ever. Mwaka 2000 mimi na kina Zitto tulifukuzwa shule na baadhi yetu maisha yalibadilishwa forever. Mwaka 2008 kuna murra mwingine atafukuzwa chuoni na story itaendelea kuwa ile ile na utatuzi wa hili tatizo utakuwa mbali sana.

Prof Mukandala, please and please. Njia ya kufukuza na kunyanyasa wale wanaoitwa "instigators" wa migomo imeonekana kutomaliza suala la migomo kwa sasa. Tafuteni njia nyingine ya kutatua suala la gharama za elimu ya juu nchini.

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…