Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Nadhani kuendelea kuvifunga hivi vyuo kwa week kadhaa na kisha kuvifungua ni kupoteza pesa za walipa kodi na wakati.

Wanafunzi need to know kwamba kugomba sio solution ya matatizo, na haijawai kuwa solution. I think hii tabia ya kugoma goma tume ilea wenyewe na sasa imekuwa jini mla watu inatumaliza sisi wenyewe.

Naamini kama tunataka hii tabia isijiludie basi serikali ichukue new action ambayo itakomesha huu mchezo. I can propose the harsh measurements ambayo kama serikali itachukua basi huu mchezo hautorudiwa tena.

Moja ya njia hizo ni kufukuza wanafunzi wote, kisha kufanya new vetting procidure ambayo itarudisha wachache wanaotaka kuwepo chuoni. Kisha kuandaa some kind of mechanism ambayo itakomesha hii tabia.

I am against kugoma, i believe on dialogue.
 
Nadhani kuendelea kuvifunga hivi vyuo kwa week kadhaa na kisha kuvifungua ni kupoteza pesa za walipa kodi na wakati.

Wanafunzi need to know kwamba kugomba sio solution ya matatizo, na haijawai kuwa solution. I think hii tabia ya kugoma goma tume ilea wenyewe na sasa imekuwa jini mla watu inatumaliza sisi wenyewe.

Naamini kama tunataka hii tabia isijiludie basi serikali ichukue new action ambayo itakomesha huu mchezo. I can propose the harsh measurements ambayo kama serikali itachukua basi huu mchezo hautorudiwa tena.

Moja ya njia hizo ni kufukuza wanafunzi wote, kisha kufanya new vetting procidure ambayo itarudisha wachache wanaotaka kuwepo chuoni. Kisha kuandaa some kind of mechanism ambayo itakomesha hii tabia.

I am against kugoma, i believe on dialogue.

I really doubt if you are well informed about the topic you are trying to discuss! Who perpetuates that kind of practice? Just do a bit of homework and you will reconcile your mind soon.

What happens if students can go without water in the hostels for 5 days, then abandons class for 3 hours and water starts to flow?? Harsh measures (as you propose) have never been a solution and can not help to silence people whose demands are right and justifiable. That's a kind of Ostrich trick,... to hide the eyes in the sand to avoid the enemy.
 
Wanasiasa msiongee vitu msivyokuwa na uhakika nao kuna tatizo katika database ya bodi ya mikopo ndio maana kuna vitu vinashindikana sio kwamba wanafunzi wamebaguliwa
 
Nadhani hata uwezo wakutafakali issue huna wale wale, wasomi ni wakorofi!!!......serikali nayo ifuate taratibu si ubabe kama unavypendekeza....chuo kikuu ni sehemu wanapotoka intellectuals, kama wachukia wasomi maofisini basi una tatizo zaidi
Ushirombo
Naomba tuongozane kutafakari haya yafuatayo kidogo,wasomi ninyi:
Nafikiri tumefika hapa tulipo kwa sababu sisi kama taifa tumepoteza MAADILI.

Maadili ya Taifa those days yalijengwa sana pale NATIONAL SERVICE.
Ule utaratibu ulisaidia sana kujenga yafuatayo:
1.NIDHAMU
2.MOYO WA UTAIFA
3.UKAKAMAVU WA KIFIKRA HATA WA KIMWILI.

Katika maisha lazima uwe mkakamavu hasa kifikra.

Huwezi leo ukaingia mkataba na serikali kuwa utalipa a certain remaining percentage ukakaa chuoni mwaka mzima then unakuja kesho unasema huwezi kulipa kile ulichoahidi kwenye mkataba wako na serikali.

Mikopo hiyo inatolewa kwa madaraja.

Kwangu mimi that is okay, kwani initially mikopo ilitolewa asilimia 100,lakini mahitaji na idadi ya wanafunzi mfano, 2002 tofauti na idadi ya 2007.Hicho kidogo itabidi mgawane,budget finyu (achana na habari za EPA,zitakufanya ushindwe kutafakari kwa mapana kwani kidogo unakimbilia oh EPA,oh ....SITISHA HIZO FIKRA KWA MUDA).

Tu my knowledge niwale walio perform vizuri wa madaraja ya juu watachangia kidogo.

Hiyo ni changamoto kuwa mnatakiwa ninyi vijana wa sasa msome zaidi ili muweze kufaulu na kuchangia kidogo.Hapo mimi sioni shida.

Ninyi kama wasomi kaka mnaona utaratibu wa Mikopo hauko sawa, then kaeni mbrainstorm na kujua mfanye nini kuibadili hiyo sera na HAPO NDIPO USOMI NA TOFAUTI YENU itakapoonekana comparatively na sisi tulio huku mtaani.

Migomo ni tool fulani tu kati ya tool nyingi ambazo mnaweza kutumia kufikia malengo yenu.Inasikitisha mnapo ng'ang'ania tool hiyo hiyo tuu kila mnapo pata matatizo.
Matatizo katika maisha hayatatuliwi kwa tool moja tu vinginevyo mkija huku mtaani mtaadhirika wadogo zangu.

Nimechangia hili kwani siku ile wanafunzi wameagizwa kutoka pale Mabibo hostel,ilikuwa aibu tupu.Watoto wa kike hawana pa kwenda wengine hawana ndugu hapa mjini.Matokeo yake watu walipata wake za bure that evening.
FIKIRIA MTOTO HUYU WA KIKE ANACHUKULIWA NA KUWEKWA KINYUMBA HATA KWA SIKU TATU TU.UJAUZITO,UKIMWI NA HATA MAUAJI KUTOKANA NA KUFUMANIWA NA MABWANA AU WAUME ZA WATU.

Haya ni matatizo makubwa Ushi.

Si lengo langu kuzungumza na wewe ila nazungumza na wote ambao mnashabikia haya mambo pasipo kufikiri nini kitatokea kutokana na maamuzi fulanifulani mnayoamua katika maisha yenu.

Tazameni adhari za migomo yenu kwenye LABOUR MARKET.Mnasoma saa ngapi kama kila wakati mnagoma, chuo kinafungwa je hiyo PRODUCT kweli ya miaka mitatu au minne kweli ni ile DESIRED.

HATUKATAI DAINI HAKI,LAKINI KATIKA KUDAI HUKU MJITOFAUTISHE NA SISI WA HUKU MTAANI.

CHOOSE THE RIGHT TOOL.
 
leo hii wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu wa chuo kikuu cha ushirika moshi nao wamegoma.
Moto unakaribia nao kuwaka kwenye chuo kikuu cha JK cha udom!
 
Wanasiasa msiongee vitu msivyokuwa na uhakika nao kuna tatizo katika database ya bodi ya mikopo ndio maana kuna vitu vinashindikana sio kwamba wanafunzi wamebaguliwa

hayo matatizo unayoyasema ndiyo yamesababisha hiyo mikopo isitolewe kwa haki, na utambue kuwa ubaguzi ni hayo matokeo ya ubovu wa hiyo mitambo (kama hicho unachodai ni sahihi).na huo ubaguzi haushii kwenye Loan board kushindwa kutambua uwezo wa waombaji(means testing) bali pia kitendo cha kuwabagua wale waliopata "division one" (kwa wavulana) na div.one & two (wasichana) ndio wanapata mikopo pasipo kuzingatia kuwa kigezo cha msingi ni muombaji kuwa na udahili katika chuo cha elimu ya juu.

hao wanasiasa unaowasemea sijui ni akina nani, hebu fafanua hapo.Ni loan board?ni waziri?ni wanafunzi?ni wazazi/walezi?au wadau wa elimu???
 
Nadhani Prof Lipumba ameshakata mzizi wa fitina!
mwenyewe kasema na ni mwanauchumi mzuri tuu kwamba kama serikali ni kuwapa wanafunzi wote asilimia 100 then ni kitendi cha kuongeza bilioni 20 tuu kwenye bajeti yake ya wanafunzi wote wa vyuo.
Serikali haijakosa bilioni 20 ila wanasikia raha kuona migomo!
 
Sasa John malecela anavyosema serikali iwafanyie wanafunzi wapya udahili kwa sababu hawa waliopo hawajui umuhimu wa elimu sasa hao watakaodahiliwa wakigoma tena watadaili wengine gani tena?
Mind you huyu mtu aliyekuwa anataka kugombea urais 2005.
TANZANIA BILA VIONGOZI WAJINGA INAWEZEKANA!
 
Zitto, Nape wamvaa Maghembe




na Edward Kinabo



WAKATI walimu wakitarajia kuanza mgomo wao leo, huku baadhi ya vyuo vikuu vikiwa vimefungwa kutokana na migomo, kada machachari wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jumanne Maghembe, kuacha kutumia ubabe na badala yake kuwakalisha wadau wa elimu ili kupata ufumbuzi wa hatma ya elimu nchini.

Nape alisema hali hiyo ikiachwa iendelee, inaweza kuiweka pabaya CCM hasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Nape alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa maoni yake kuhusu mgomo wa walimu uliotarajiwa kuanza leo pamoja na kufungwa kwa vyuo vikuu kadhaa nchini kutokana na madai ya kupinga sera ya uchagiaji elimu ya juu.

Nape alisema anashangazwa na ubabe wa serikali katika kutatua tatizo hilo kwani kinachotakiwa ni waziri mwenye dhamana kutumia busara ya kukaa na wadau wa elimu ili kurekebisha kasoro iliyopo, vinginevyo CCM na Serikali yake inazidi kujiweka kwenye wakati mgumu zaidi.

“Kinacholalamikiwa hapa ni sera ya uchagiaji elimu juu ambayo lengo lake ni kuwasaidia Watanzania, sasa kama wenyewe wanalalamika maana yake kuna tatizo katika sera ya uchangiaji na ili kuiondoa kasoro hiyo waziri anapaswa kukaa na wadau wa elimu badala ya kutumia ubabe au kikimbilia mahakamani,” alisema Nape.

Mwanasiasa huyo ambaye siku za hivi karibuni alijikuta kwenye mzozo mzito na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), alisema anakerwa na tabia ya ubabe ya Maghembe na wizara yake ambayo alisema si dawa ya kukabiliana na migomo.

Kuhusu mgomo wa walimu, Nape alisema ni aibu kwa Serikali kukimbilia mahakamani kusaka suluhu kwani madai ya walimu ni ya muda mrefu na njia sahihi ni kuyalipa.

“Ni vizuri Waziri Maghembe akaangalia namna ya kuondoa tatizo hilo. Serikali kukimbilia mahakamani ni aibu na hata Serikakali ikipata haki, haina maana kwani walimu wataendelea kufanyakazi kwa shingo upande.

Nape alisisitiza kuwa hali hiyo ikiachwa iendelee, itakuwa mbaya kwa CCM kwani wanaolalamikia kutotendewa wengi ni wanachama CCM na ndio wapiga kura wao.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe alisema kitendo cha serikali, kushindwa kutatua migogoro ya wanafunzi na walimu ni kielelezo kuwa CCM imechoka na haina uwezo tena wa kuwaongoza Watanzania.

Zitto alisema hayo juzi wakati akitoa mada kuhusu hali ya uchumi nchini katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vya elimu juu vya Mkoa wa Iringa, lililofanyika katika Ukumbi wa Jumba la Maendeleo, mjini Iringa.

Mbele ya maelfu ya wanafunzi waliofurika katika kongamano hilo, Zitto alisema CCM imechoka kufikiri ndio maana kwa muda mrefu sasa imekuwa ikishughulikia matatizo ya migomo ya wanafunzi kwa kufunga vyuo na kuwatisha, njia ambazo hazitaweza kumaliza matatizo yaliyopo.

“Tunaiambia serikali, huwezi kutatua matatizo ya uchangiaji wa elimu ya juu kwa kufunga vyuo. Huwezi kutatua migogoro ya elimu ya juu kwa kutishia wanafunzi. Matatizo ya elimu ya juu yatatuliwe kwa njia ya majadiliano na si mazungumzo kati ya serikali na wanafunzi pekee, yanapaswa kuwa mazungumzo yatakayoshirikisha jamii nzima….jamii nzima ikae na iamue jinsi gani ya kugharamia elimu ya juu,” alisema Zitto.

Zitto alitumia fursa hiyo kujibu tuhuma zinazotolewa na viongozi wa serikali na wa CCM kwamba CHADEMA imekuwa ikitumia viongozi na makada wake, kuchochea migomo katika vyuo hivyo.

Alisema CHADEMA haijawachochea wanafunzi wagome na haiwezi kufanya hivyo lakini inaunga mkono juhudi zote za kundi lolote linapodai haki zao, kama walimu na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanavyodai haki zao.

Alisema chama chake kinatetea zote haki za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini kwani kimejengwa na kuimarishwa na vuguvugu la wasomi wa vyuo vikuu na wanaharakati mbalimbali nchini, akiwemo yeye mwenyewe na viongozi wengine.

“CHADEMA ni chaguo la watu makini, ni chaguo la wanaharakati. Aliyewahi kuwa rais wa Serikali ya wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar-es-Salaam (Daruso) mwaka 1998/1999, Kitila Mkumbo, ni mwanachama wetu hai. Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Daruso mwaka 2005/2006, John Mrema, ndiye Mkurugenzi wetu wa sasa wa Bunge na Halmashauri. Aliyewahi kuwa Rais wa serikali ya wanafunzi chuo cha teknolojia Dar-es-Salaam, Msafiri Mtemelwa, ndiye Mkurugenzi wetu wa kampeni na uchaguzi. Aliyewahi kuwa Rais wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Dadi Igogo, ndiye afisa mwandamizi wa kurugenzi ya mafunzo.

Wapo wengi sana …..mimi mwenyewe pia nilikuwa Katibu Mkuu wa Daruso. Ndiyo maana serikali inaweweseka,” alisema Zitto na kushangiliwa.

Alisema baada ya vyuo kufungwa, serikali inaweza kuwarudisha baadhi tu ya wanafunzi waliogoma huku wengine wakitolewa mhanga kwa kufukuzwa kabisa na kuwataka wanafunzi hao kutokubali kuwagawanyika na waendelee kupigania haki yao kwa pamoja.

“Msisikitike chuo kufungwa, msisikitike kurudi nyumbani…….nendeni mkawaelimishe watu kuhusu kile mnachokisimamia. Wala msijali kwamba mnachokipigania hakitatokea sasa……mnachokipigania kama si ninyi basi kitakuja kuwanufaisha wadogo zenu. Kina Nyerere na Bibi Titi wasingepigania uhuru mapema tusingeupata mapema…..tungepata uhuru hata kama Nyerere na Bibi Titi wasingepigania, lakini tungechelewa,” alisema Zitto.

Alisema iwapo serikali itapanga mambo yake vema, inaweza kumudu kutoa mikopo ya asilimia 100 kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu nchini kutokana na kasi nzuri ya ukuaji wa uchumi.

“Huko nyuma wakati wa Nyerere, serikali iliweza kuwalipa walimu na kugharamia gharama zote masomo. Iliwasomesha watu bure kuanzia elimu ya msingi hadi elimu ya juu wakati ambapo ukuaji wa uchumi ulikuwa chini sana . Leo wakati kasi ya ukuaji uchumi ni nzuri serikali inasema haina fedha.

Akizungumzia hali ya uchumi nchini, Zitto alisema unakua kwa wastani wa asilimia 5.6 ambacho ni kiwango kikubwa kabisa kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, na inatarajiwa mwaka huu utakuwa kwa asilimia 7.2.

Hata hivyo alisema ukuaji huo umeshindwa kuwaondolea watu umaskini kwa sababu unachangiwa sana na ukuaji wa sekta ya madini, mawasiliano na ujenzi, ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na uborekaji wa maisha ya watu.

Akitoa mfano katika sekta ya mawasiliano, alisema wakati makampuni ya simu ya vodacom, zain na tigo yanajiingizia mabilioni ya fedha kwa siku, hakuna kampuni ya simu hata moja nchini inayolipa kodi ya mapato kwa serikali.

“Chukua mfano wa Zain yenye wateja karibu milioni 3. Kwa huduma yao ya xtreme tu inajiingizia bilioni 3 kila siku. Tigo yenye wateja milioni 2, pigia hesabu wateja milioni moja tu, kwa huduma yake ya ‘xtreme’, kwa siku inajiingizia bilioni 1. Vodacom yenye wateja wengi, ina wateja milioni 5, kwa huduma yake ya chizika, kwa siku inajiingizia bilioni 4. Piga kwa mwezi, kwa mwaka ni sh ngapi…… Lakini hakuna kampuni hata moja ya simu inayolipa kodi ya mapato. Serikali ingekusanya kodi ya mapato kwenye kampuni hizi…..isingeshindwa kuwapa mikopo ya asilimia 100,” alisema Zitto.

Akigusia sekta ya madini, alisema serikali haikufikiria vema katika kunufaika na uwekezaji unaofanyika kwenye sekta hiyo kwani ililenga kupata pesa kutokana na mrabaha tu ilhali kuna njia nyingine ambazo serikali ingeweza kujipatia mapato kutokana na madini, ikiwemo kutoza kodi kwa makampuni ya uchimbaji, kuingia ubia na makampuni hayo na kuhakikisha kuwa kunakuwa na uhusiano kati ya ukuaji wa sekta moja na nyingine.

“Wakati serikali imekuwa ikitegemea kutoza mrabaha wa asilimia 3 ambao hata ukipandishwa hauwezi kuzidi asilimia 12, kwa kipindi cha miaka 10, imekuwa pia ikitoa misamaha ya kodi kwa makampuni ya madini ili yaweze kujiagizia mafuta kwa ajili ya kuzalisha umeme kwenye machimbo yao, ” alisema Zitto.

Alisema matokeo ya kufanya hivyo ni serikali kujikuta imesamehe jumla ya dola milioni 32 kwa makampuni hayo, huku yenyewe ikipata dola milioni 25 tu kutokana na kutoza mrabaha huo wa asilimia 3, wakati ingeweza kuepuka hasara hiyo kwa kuhakikisha kwamba shirika la Umeme (TANESCO) linasambaza umeme katika migodi yote nchini.

Aliongeza kuwa kama serikali isingesamehe kodi kwa makampuni ya uchimbaji wa mafuta pekee kwa mwaka 2006 tu, basi ingeweza kulipa deni la bilioni 16 inalodaiwa na walimu ikiwa ni malimbikizo ya mafao yao .

Alisema chanzo cha serikali kushindwa kuwalipa walimu ni kuyanufaisha makampuni hayo ya madini ambayo ni ya matajiri kwa kuyasemehe kodi, ambayo kama ingekusanywa ingeweza kuepusha mgomo unatarajiwa kuanza kesho Jumatatu.

Alisisitiza kwamba serikali ya CCM imechoka na haiwezi tena kuwaondolea Watanzania umaskini kwani imesahau kujenga uchumi wa vijijini kwa kushindwa kukuza sekta ya kilimo na kujenga miundo mbinu vijijini, hali iliyosababisha kujengeka kwa mataifa mawili ndani ya taifa moja, moja likiwa la matajiri waliyopo mijini na jingine taifa la maskini ambao wapo vijijini.

Katika kongamano hilo, ambalo pia lilijadili rasimu sifuri ya sera ya vijana ya CHADEMA, iliyowasilishwa na Dadi Igogo na Danda Juju, zaidi ya washiriki 200 walijiunga na CHADEMA, huku wawili kati yao wakiwa wamerejesha kadi za CCM.

Kongamano hilo lilikuwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanafunzi duniani ambapo mwaka jana chama hicho kilifanya maadhimisho kama hayo katika ukumbi wa DDC jijini Dar-es-Salaam.
 
Ni jambo la aibu sana kuona matatizo yaliyokuwepo miaka nenda rudi yanashindwa kutafutiwa ufumbuzi, yaani hii ndo inaitwa "kufanya mambo kwa staili ile ile halafu utegemee matokeo tofauti", chukulia mfano mfano suala la mikopo ya wanafunzi nimeambiwa kwamba hata mwaka huu kuna wanafunzi wamezidishiwa mkopo kuliko kiasi walichoomba.
sasa mtu unajiuliza umakini upo wapi?, yaani Wizara ya Elimu imeshindwa kutoa tenda itengenezewe software makini ya kuhakiki data zake!!. hili ni jambo la ajabu kabisa
 
Zitto, Nape wamvaa Maghembe

"Tunaiambia serikali, huwezi kutatua matatizo ya uchangiaji wa elimu ya juu kwa kufunga vyuo. Huwezi kutatua migogoro ya elimu ya juu kwa kutishia wanafunzi. Matatizo ya elimu ya juu yatatuliwe kwa njia ya majadiliano na si mazungumzo kati ya serikali na wanafunzi pekee, yanapaswa kuwa mazungumzo yatakayoshirikisha jamii nzima….jamii nzima ikae na iamue jinsi gani ya kugharamia elimu ya juu,"

"Msisikitike chuo kufungwa, msisikitike kurudi nyumbani…….nendeni mkawaelimishe watu kuhusu kile mnachokisimamia. Wala msijali kwamba mnachokipigania hakitatokea sasa……mnachokipigania kama si ninyi basi kitakuja kuwanufaisha wadogo zenu. Kina Nyerere na Bibi Titi wasingepigania uhuru mapema tusingeupata mapema…..tungepata uhuru hata kama Nyerere na Bibi Titi wasingepigania, lakini tungechelewa," alisema Zitto.

Alisema iwapo serikali itapanga mambo yake vema, inaweza kumudu kutoa mikopo ya asilimia 100 kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu nchini kutokana na kasi nzuri ya ukuaji wa uchumi.

I love it

..........Hata hivyo alisema ukuaji huo umeshindwa kuwaondolea watu umaskini kwa sababu unachangiwa sana na ukuaji wa sekta ya madini, mawasiliano na ujenzi, ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na uborekaji wa maisha ya watu.

Akitoa mfano katika sekta ya mawasiliano, alisema wakati makampuni ya simu ya vodacom, zain na tigo yanajiingizia mabilioni ya fedha kwa siku, hakuna kampuni ya simu hata moja nchini inayolipa kodi ya mapato kwa serikali.

"Chukua mfano wa Zain yenye wateja karibu milioni 3. Kwa huduma yao ya xtreme tu inajiingizia bilioni 3 kila siku. Tigo yenye wateja milioni 2, pigia hesabu wateja milioni moja tu, kwa huduma yake ya ‘xtreme', kwa siku inajiingizia bilioni 1. Vodacom yenye wateja wengi, ina wateja milioni 5, kwa huduma yake ya chizika, kwa siku inajiingizia bilioni 4. Piga kwa mwezi, kwa mwaka ni sh ngapi…… Lakini hakuna kampuni hata moja ya simu inayolipa kodi ya mapato. Serikali ingekusanya kodi ya mapato kwenye kampuni hizi…..isingeshindwa kuwapa mikopo ya asilimia 100," alisema Zitto.

Akigusia sekta ya madini, alisema serikali haikufikiria vema katika kunufaika na uwekezaji unaofanyika kwenye sekta hiyo kwani ililenga kupata pesa kutokana na mrabaha tu ilhali kuna njia nyingine ambazo serikali ingeweza kujipatia mapato kutokana na madini, ikiwemo kutoza kodi kwa makampuni ya uchimbaji, kuingia ubia na makampuni hayo na kuhakikisha kuwa kunakuwa na uhusiano kati ya ukuaji wa sekta moja na nyingine.

"Wakati serikali imekuwa ikitegemea kutoza mrabaha wa asilimia 3 ambao hata ukipandishwa hauwezi kuzidi asilimia 12, kwa kipindi cha miaka 10, imekuwa pia ikitoa misamaha ya kodi kwa makampuni ya madini ili yaweze kujiagizia mafuta kwa ajili ya kuzalisha umeme kwenye machimbo yao, " alisema Zitto.

Alisema matokeo ya kufanya hivyo ni serikali kujikuta imesamehe jumla ya dola milioni 32 kwa makampuni hayo, huku yenyewe ikipata dola milioni 25 tu kutokana na kutoza mrabaha huo wa asilimia 3, wakati ingeweza kuepuka hasara hiyo kwa kuhakikisha kwamba shirika la Umeme (TANESCO) linasambaza umeme katika migodi yote nchini.

I like it..
 
NAOMBA turudi nyuma hatua moja na kuanza kuangalia mikataba na migodi ya wachimba dhahabu hapa nchini.

Je, tukiongeza hivi ni mrabaha au mrahaba toka asilimia 3 hadi 10 tutashindwa kweli kuwalipa wanafunzi wote asilimia 100.

Je, tukipunguza gharama kubwa za serikali ambazo zinadidimiza uchumi badala ya kusaidia kukuza uchumi kwa kuwa na magari simpo na sio mashangingi na serikali kukwepa kubeba mzigo wa spea pati, petroli na dizeli kwa kuwauzia wakuu magari hayo tutashindwa kuokoa fedha za kuwatendea haki vijana wetu?

Hivi kila wizara, idara, wilaya na mkoa ukiwa na mkakati wa kiuchumi na kuwa na visheni na misheni ya kujikwamua na 'kuaccelerate' kiuchumi tutashinwa kweli kuingiza mapato ya kutosha kuwalipia watoto wetu wote wenye uwezo na nia ya kusoma.

Hivi hizo scholarship nyie hapo WIZARA ya ELIMU mnazoziiba na kuwapa watoto wenu mngezilipia zisingepatikana hela za kujazia mapengo?

Hivi maduka ya Mlimani Millenium Village na kwingineko Tanzania yangetuajiri kwa masaa nasi tungekosa pesa za kujazia kujisomesha.

Tatizo ni kwamba nyie mlioko serikalini mmejisahau, sera hamna na jipya la mazuri hamna ila ni watu wa shari tu na mnaopenda kutumia nguvu na mabavu pale isipostahili.

Mwinyi alisema yeye angalau alikuwa kichuguu nyie sijui tuwaite nani jamani???
 
Ushauri:

Serikali ibadilishe utaratibu na kusimamisha ufadhili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu binafsi kisha itowe mikopo ya 100% kwa vyuo vikuu vya umma.

Karibu kila mwaka kuna chuo kikuu kipya kinaanzishwa nchini. Serikali haiwezi kumudu kutoa ufadhili kwa vyuo vikuu vyote kwa 100%.

Wasioweza kushindana katika vyuo vikuu vya umma wajisomeshe wenyewe kwa njia wanazojua.
 
na dit, chuo cha uhandisi jijini dar es salaam kilichopo morogoro rd, nacho kimefungwa leo kwa muda usiojulikana. wanafunzi wameagizwa kuondoka ifikapo saa 11.00 jioni ya leo.
kufukuzwa kwao kunatokana na mgomo uliodumu kwa siku tatu. taarifa iliyo tolewa kwa redio ya mlimani na ofisa habari wa chuo hicho imethibisha wanafunzi wote wamekwisha ondoka.

mwendo ndio huo. tutafika tuendako.

macinkus
 
Ushirombo
Naomba tuongozane kutafakari haya yafuatayo kidogo,wasomi ninyi:
Nafikiri tumefika hapa tulipo kwa sababu sisi kama taifa tumepoteza MAADILI.

Maadili ya Taifa those days yalijengwa sana pale NATIONAL SERVICE.
Ule utaratibu ulisaidia sana kujenga yafuatayo:
1.NIDHAMU
2.MOYO WA UTAIFA
3.UKAKAMAVU WA KIFIKRA HATA WA KIMWILI
.

mkuu hapo umechemka vibaya sana.hakuna hata chembe ya ukweli katika maoni yako.kumbuka kuwa hawa watu waliosfhikiria nafasi nyeti serikalini na mashirika ya umma ndio hao waliopita huko JKT, lakini ndio hao hao wanaoongoza kwa ufisadi, ndio hao hao wanaoongoza kwa rushwa, ndio hao hao wanaosaini mikataba mibovu kila siku.ndio hao hao wanaowaleta richmonduli, IPTL,songas n.k. ndio hao hao wanaojigawia kiwira coal mine bure, wanogawia makaburu bure benki yetu ya NBC, ndio hao waliolitoa shirika letu la reli(TRC) kwa magabacholi wa TRL, hao hao ndio wameua ATC na viwanda na mashirika kede kede, mengine utajaza mwenyewe.
hao hao ndio wanasomesha watoto wao nje ya nchi na kusahau kabisa kuwa watanzania wengine nao wanahitaji elimu bora.hao hao ndio wanaotunga sera zisizozingatia hali halisi za watanzania walio wengi ambao ni maskini.
halafu unataka kutuambia eti sisi JKT itasaidia sijui mambo gani????
kajipange upya mkuu hapo hakuna kitu!!!
 
WaTanzania msishangilie sana ,kwa upande wangu naona huu si wakati wa walimu na wanafunzi kugoma,kama ,hivi sasa uchumi wa Dunia nzima umeanguka tena umeanguka vibaya sana,hawa wanaogoma naona hawayajui hayo japo ni walimu na wanafunzi ,wana ufahamu mdogo wa hali inavyokwenda ,ni jana tu nchi za Ulaya na Marekani zimatangaza kutokuwa na fedha za kuwahudumia wanafunzi ,hebu fikirieni jambo hilo.
Inawezekana Serikali ya Kikwete ilijipanga vizuri kumaliza matatizo na walitoa ahadi lakini kabla hawajaanza kuhudumia na kutimiza ahadi ,mambo ya kibenki duniani yakaharibika na sidhani kama hayakutugusa hapa Tanzania,hivyo hata kama kuna feza ilitengwa kwa ajili ya kulipa na kuhudumia wanafunzi ,fedha hiyo ilibidi isimamishwe kwanza na pengine kwa muda fulani ,haiwezekani kabisa Serikali ikatumia fedha wakati kuna machafuko ya kifedha au Uchumi katika Dunia na tahadhari zimeshatolewa kila kona.

Moja ya tahadhari ni Matumizi holela ya fedha ambayo yanaweza kupelekea serikali kushindwa na kuangushwa au kusababisha matatizo ya njaa na mifarakano ya kulipa mishahara.

Kwa upande wangu naona serikali kwa wakati huu haitambembeleza sana mwalimu au mwananfunzi kwani serikali kwa sasa ipo kwenye matatizo ya kiuchumi ,ambayo yameikumba dunia na ipo kwenye tahadhari , ikiwa kuna Nchi au makampuni yanapunguza wafanyakazi ,hivyo kwa haya yetu serikali itaona bora kila mmoja ashike njia arudi kwao na hapo itakuwa imejinasua katika kulipa mishahara na posho.

Si ajabu kwa serikali yetu au zetu zikawatimua wote na kuanza upya hali ya kiuchumi itakaporejea.
 
Kuna taarifa nimesikia kuwa chuo cha muhimbili hali si shwali mwenye full data atupatie.
 
NAOMBA turudi nyuma hatua moja na kuanza kuangalia mikataba na migodi ya wachimba dhahabu hapa nchini.

Je, tukiongeza hivi ni mrabaha au mrahaba toka asilimia 3 hadi 10 tutashindwa kweli kuwalipa wanafunzi wote asilimia 100.

Je, tukipunguza gharama kubwa za serikali ambazo zinadidimiza uchumi badala ya kusaidia kukuza uchumi kwa kuwa na magari simpo na sio mashangingi na serikali kukwepa kubeba mzigo wa spea pati, petroli na dizeli kwa kuwauzia wakuu magari hayo tutashindwa kuokoa fedha za kuwatendea haki vijana wetu?

Hivi kila wizara, idara, wilaya na mkoa ukiwa na mkakati wa kiuchumi na kuwa na visheni na misheni ya kujikwamua na 'kuaccelerate' kiuchumi tutashinwa kweli kuingiza mapato ya kutosha kuwalipia watoto wetu wote wenye uwezo na nia ya kusoma.

Hivi hizo scholarship nyie hapo WIZARA ya ELIMU mnazoziiba na kuwapa watoto wenu mngezilipia zisingepatikana hela za kujazia mapengo?

Hivi maduka ya Mlimani Millenium Village na kwingineko Tanzania yangetuajiri kwa masaa nasi tungekosa pesa za kujazia kujisomesha.

Tatizo ni kwamba nyie mlioko serikalini mmejisahau, sera hamna na jipya la mazuri hamna ila ni watu wa shari tu na mnaopenda kutumia nguvu na mabavu pale isipostahili.

Mwinyi alisema yeye angalau alikuwa kichuguu nyie sijui tuwaite nani jamani???

,,,,,,inachekesha lakini inahuzunisha sana hii,hivi nchi hii TUTAFIKA kweli,Manake mijitu kazi ya kuongoza nchi hii imeshindwa,lakini ajabu ndio yameng'ang'aniaaa!!!!,aaah ,kwani aliwadanganya nani kwamba nyie mnaong'ang'ania kuongoza nchi hii ni ya kwenu DAIMA??,muungwana ukipewa mke na humuwezi,unatoa nafasi kwa wengine wanaomuweza bwana,tushachoka????
 
Watanzania wenzangu mimi kwa mawazo yangu na kama Mtanzania nilio nje naweza kusema kwa uhakika kwamba siasa zinarudisha Tanzania nyuma sana. Mijadala mingi kwa sasa ni malumbano kuliko jinsi ya Kutatua matatizo. Zitto kwa mfano ni kijana mwenye akili na mawazo mengi lakini mambo mengi anayozungumzia ni siasa tu kwa mfano. Zitto alikuja huku marekani akaongea na Watanzania kuhuzu mambo muhimu ya nchi lakini aliporudi Tanzania hakuwaita waandishi wa habari kuzungungumzia vitu vizuri alivyojifunza USA badala yake alirudi kupiga porojo. Watanzania wa nje tunaomba tuhusishwa na mijadala ya maendeleo kidogo kuliko kulumbana kila siku. Je zitto Bill yako ya elimu iko wapi? ahadi zako za kuelimisha Watanzania kuhusu mchango wa Watanzania walio nje umeishia wapi? Ikuwapi plan ya kuhakikisha Zambia, zaire, burundi na rwanda wanatumia bandari?. Hakuna plan badala yake tuna jadili migomo bila kuwa na suluhu, ukweli ni kwamba Tanzania ni masikini na badala ya kulumbana tueleze mawazo yetu ya kutoka kwenye umasikini?? Zitto hawezi hata kujibu emails lakini anamuda wa kulumbana huku??? nashangaa sana.
 
Back
Top Bottom