changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Nakumbuka na sifa akapewa kwamba kwa Gamond kila mchezaji atapata nafasi uwanjani. Wakawahesabu wachezaji wote wameshacheza kasoro Msheri tu. Sifa akapewa za kutosha kuwa kikosi ni kipana Gamond ni bingwa wa rotation. Mechi ya Ihefu ikabadili upepo, Yanga alipofungwa mashabiki wakalalamikia uwepo wa akina Mauya na Sureboy, nk kuwa kocha alikosea kufanya rotation katika mechi ngumu kama ile ya away. Mashabiki wakalalamika, kocha akajifunza kutumia silaha zake zile zile anazoamini ili apate matokeo.Mashabiki siku zote hawaeleweki wanataka nini
Kipindi mnapigwa na Ihefu unakumbuka lawama zilikuwa kuhusu nini?
Wengi mlimshukia Kocha kwa kufanya rotation ya kikosi kwa kuwaweka benchi wachezaji wenu mnao wapenda.
Leo kocha anaweka hao wachezaji wenu mnao wapenda ambao mna amini ndio mhimili wa timu lakini bado mnakuja tena kumpa lawama kwanini hachezeshi wale wachezaji ambao hamkuwataka kwenye mechi ya Ihefu.
Hao ndio Gongowazi
Kocha inawezekana akawa ni muumini mzuri wa rotation, na akili yake pengine ilikuwa inadhani wachezaji wote wa Yanga wanashabihiana kwa uwezo na ubora ila aliyaona kwenye ile mechi akapata funzo.