Miili ya watu 20 yakutwa katika Jangwa Nchini Libya

Wakati wa Ghadafi yaliwahi kutokea haya??
 
Dikteta/udikteta ni mtu au kikundi cha watu wanaotawala nchi bila kufungwa na katiba ya ya nchi. Dikteta ni kiongozi ambaye kauli yake, hulka zake na matamanio yake vinaweza kuwa sheria, sera au mipango ya serikali wakati wowote bila kujali katiba, sheria , miongozo na tamaduni za muda mrefu zilizokubalika katika nchi husika.
Hivi dikteta Ni nani!?
 
Nikijibu vibaya ntakula ban ngoja nitulie tu
Alikua dikteta ndio..niulize lini aliitisha uchaguzi mkuu wa libya..alijiona Mungu mtu kuwa yeye ndio yeye hakuna zaidi Libya ona alioipeleka nchi yeye ndio wa kwanza kulaumiwa katika hili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana ju ya Gadafi na utawala wake .

Viongozi wengi wa ukanda wa Afrika wanapenda Sana madalaka na wakiyapata inakuwa ruba ,hawataki kuachia madalaka.

Wananchi wa Libya walihitaji mabadiliko ya kiutawala na usawa wa kunufaika na lasilimali za nchi ya Libya kwa watu wote.

Hata hivyo Gadafi hakutaka katakata kuachia madalaka licha ya mda wake KIKATIBA kuisha na kuungaunga katiba ili aendelee kuwa rais taklibani miaka 42 akiwa mamlakani mpaka alipo pinduliwa na kuuawa, kwani wananchi walikuwa hawajui ni lini Gadafi ataachia madalaka na kukabidhi wengine.

Hata hivyo taarifa zingine zilidai kwamba alitaka kurithisha utawala huo kwa mwanaye , kwani kuanzia jeshini ilionekana hivyo hivyo .

Vilevile kulikuwa na visa vingi vya walinzi wake kutakiwa kimapenzi kwa nguvu bila ridhaa yao ( ubakaji) ambapo Gadafi na wanawe waliwafanyia ubakaji huo .

Kabla ya miaka 42 Gadafi alipaswa kuachia madalaka kwa wengine , kwani kitendo cha kiutawala Libya kwa mkono wa chuma mds wote huo kiliwafanya wananchi wamchoke na ikwa ni fursa kwa wazungu kupenyeza ushawishi wao ili kumdondosha mamlakani.

Viongozi wa Africa wawe makini Sana ju ya kuifuata katiba zilizo waingiza madalakani na sio kuanza kuzipinda ili ziwasaidie kuendelea kutawala mataifa yao ni mtego mkubwa.
 
Waache wafe hata wote ilihali walihusika na mauaji ya Kanali M. Gaddafi.
 
Ukiwa kiongozi ongoza kwa muda mfupi kisha ondoka waachie wamchague mwingine, (George Washington).

Kama Mungu tu aliyewaumba na kuwaweka kwenye dunia yake ndio wanamuasi sasa wewe ni nani utake kutawala milele?

Siku ile Gaddafi anauwawa hakukuwa na mmarekani hata moja kwenye tukio, Gaddafi aliuliwa na Walibya wenzake na kama wangekuwa wanampenda sana ule uasi usingekuwepo hivyo watu acheni unafiki.

Gaddafi alipofikia alikuwa amewachosha wananchi wake, huo ndio ukweli, hayo mengine ni porojo tu za wafia dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…