Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Miili ya watu wawili na kichwa kimoja vimekutwa kwenye eneo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha Wilayani Mbarali mkoani Mbeya jana Jumatatu Aprili 27, 2021 huku vikiwa vimeharibika.
Taarifa za vifo hivyo zilitolewa na baadhi ya wanavijiji waliodai kukimbia askari wa wanyamapori waliokuwa wakiwafukuza katika hifadhi hiyo juzi.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Urlich Matei amethibitisha kukutwa kwa miili na kichwa hicho jana Jumatatu April 26, 2021 na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.
Akizungumza na Mwananchi leo April 27,2021 Matei amesema kuwa kwa sasa bado polisi wanandelea na ufuatiliaji wa tukio hilo ili kujua sababu ya vifo hivyo kama ni kutokana na maji ya mvua au mauaji.
"Polisi tangu jana wako huko tunaendelea kufuatilia sababu vya vifo hivyo kwani mvua zinaendelea kunyesha pamoja na kuendelea kutafuta watu wengine wanaosadikika kutoweka kwenye familia zao," amesema RPC Matei.
Awali Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Isisi ya kichama wilayani humo, Thobias Mjengwa ameiambia Mwanachi kwa njia ya simu kuwa mbali ya kupatikana kwa miili hiyo na kichwa bado kuna familia zinadai ndugu zao wanne kutoonekana kwa muda wa siku kadhaa.
"Mimi nimekwenda kushuhudia tukio hilo ni nilishiriki kuwatafuta watu ambao wanasadikika kupoteza maisha na tulianza kuwatafuta baada ya kupata taarifa za watu kukamatwa eneo la hifadhi nawaliofanikiwa kukimbia kutoka eneo la hifadhini,” amsema Mjengwa.