Mijadala haipo kwa ajili wananchi - wanakula hela zetu tu

Mijadala haipo kwa ajili wananchi - wanakula hela zetu tu

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Hata siku moja hutasikia kamwe kuna Mpango au Bajeti imepingwa na imesababisha mjadala mzito na wenye manufaa kwa wananchi.
Jana usiku nikaamua kufuatilia kilivyokuwa kipindi cha bunge - yaani kupitisha Bajeti - nilicheka sana sana yaani (kwa sauti ya Mtumishi Magembe).

Yaani alianza Shangazi - akaongea urojo rojo tu na kuleta ushabiki wa Simba. Ndugai akaingilia kuwa eti ile ni klabu kubwa - basi tu Mo yaani eti Mo ikaoenekeana hata ile kutofuata taratibu za ushindani wa kibiashara (acha michezo) ati anaonewa yaaaaaaani. Basi hoja ya Bwana wa Mlalo ikavuma - na clips nyingi zikatembea jana na akaonekana ni kati ya wabunge wa maana. Kiuhalisia hana hata maana huyu jamaa ni ujanja ujanja tu na ndiyo maana Jimbo lake limelala zii kwa maendeleo kama jina la jimbo lenyewe lilivyo. Acha mjanja aendelee kuliongoza.

Mara akafuata Bulaya - jana alionekana kazeeka kweli halafu hakuwa karibu na Swaiba wake Mdee. Akajitutumua na issue ya kikokotoo - kwa kuwa alisababisha yule mama wa SSRA akatumbuliwa mwaka 2018 basi Bulaya ndiyo kaona hiyo ndiyo kick kwake. Huyu haelewi kitu - yeye anataka tu wastaafu walipwe vizuri - hajui kuwa ile fomula ya PSPF ndiyo iliyosababisha na inayoendelea kusababisha Mfuko wa PSSSF kufa. Hajui kuwa Serikali haijaajiri vya kutosha kwa muda mrefu ukilinganisha na wanaostaafu. Hebu atumie hata akili kidogo tu. Yule mama wa SSRA alitengeneza fomula nzuri ambayo iliimarisha pensheni ya kila mwezi na kupunguza ya mkupuo.

Jenister Mhagama jana kakiri hilo na inavyoonyesha itarudi fomula ya yule yule mama. Sasa ikirudi hapo tutasema Bulaya kashinda? Yaani nchi yetu imekuwa ya vipi sijui - tunawakosoa hadi wasomi ambao wana nia ya dhati kabisa kusaidia jamii yao. Huyo mama siku hiyo pale Ikulu ninakumbka kabisa Mwendazake alimwambia "too academic".

Yaaani yaaani yaaani mie ninasema kabisa bila kurudisha ile fomula ya yule mama huo Mfuko lazima kitaumana tu (backfire hiyo). Na hapo ndipo uonevu aliofanyiwa huyo mama utaonekena wazi lakini hakuna atakayeaibika kwa kuwa kishaenda zake Mbinguni kwa Mungu.

Porojo ingine ikaja ya yule mama ati anasema waume zetu wa siku hizi hamna mbegu za kiume. Akatoa mfano wa anapotoka mume wangu kule Iringa akataja na Ruvuma kwa Mhagama. Mhagama naye akakubali ila akasema pia sababu ingine ni ulevi. Yaaaani ukfikiri kwa undani utagundua kuwa hakukuwa kabisa na mjadla ambao ulikuwa detailed wa kujadili Bajeti kama Bajeti.

Ndiyo maana kwa sasa hata kuzipata hizo nyaraka za Bajeti imekuwa kazi kwelikweli. Yaani tunawamiss sana akina Zitto na Mnyika ambao angalau walikuwa wakisema details. Hawa sasa ni wachumia tumbo tu. Hamna kitu pale. Ndiyo maana ninamsititiza mume wangu tuendelee tu kufuga nguruwe asigombee hata udiwani!
 
Ni ujinga mtupu unaoendelea kwenye jengo lile. Sioni mwenye akili ya kutegemewa.
 
Kama eneo gani sasa? Labda kule kwa Kessy!
Eneo la kukubali kutumika, kukubali kudanganywa kwa mambo ambayo hatupaswi kudanganywa, kujifanya hatuna akili na hatuwezi kutumia akili zetu ipasavyo etc. Haya nina uhakika nayo.
 
Eneo la kukubali kutumika, kukubali kudanganywa kwa mambo ambayo hatupaswi kudanganywa, kujifanya hatuna akili na hatuwezi kutumia akili zetu ipasavyo etc. Haya nina uhakika nayo.
Mfano?
 
Back
Top Bottom