Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo


Ongeza SAME, Kilimanjaro
 
Kuna vumbi la Mbeya hasa pale mabatini utakoma alafu kuna bonus ya kimbunga unaweza kuona bati hilo lipo hewani mpk litue lishachinja watu
 
Kwa morombo, Moshono, Lengijave, Kisongo, Ngaramtoni na Chekereni. Hizo sehemu sio poa
Mbele ya Lengijave, panaitwa Oldonyosambu, huko watu washarudi mavumbini kabla ya hata ya kufa. Kuna vumbi narudia tena KUNA VUMBI. Robo tatu ya vumbi la dunia liko huko. Kuna wakati unatembea ukijiangalia chini ujioni yaani unatembea lakini miguu yako huioni imezama kwa vumbi.
 
Nasikia Dodoma kila sehemu wametandaza lami kwa hio hakuna vumbi kabisa
Dodoma ipi yenye lami kote?[emoji3526][emoji3526][emoji3526]unapajua mpwayungu wewe?makanda?Manda?Fufu?chipogolo?Kuna balaa huko asehhh...Dodoma Kuna Vumbi baya sana Sijapata kuliona
 
+Morogoro
alafu Dodoma gani kuna vumbi jekundu? Wilaya wa kondoa huko labda ila dom mjin mbona nimezunguka sijaona vumbi jekundu au mtaa gani?
Sio jekundu la kahawia unapauka balaa , Dodoma Ina vumbi mi nshazunguka vijiji vya huko achaa kunatisha mweee
 
Ila dodoma nyie kuna upepo na baridi sijawahi ona. Bahati nzuri nilifikia area D sikuona hata vumbi sikupata bahati ya kutembea kwa miguu ila baridi na upepo watu wa dodoma mtakuwa mmepauka balaa.
Dodoma kunapausha sana yaani huku napaka Vaseline, Glycerin,lotion Ndo natoka na Bado kukatika miguu Ndo usiseme besti ..Kuna Hali ya hewa mbaya mnooo
 
Niko Dodoma juzi nkaenda Arusha nkasahau Sweta sikupata shida ila nimerudi Jana Ile kuingia tu dodoma Pale Machame Lile baridi na upepo nkasema Dodoma nuksi Jamani

Halafu hawajui Geography hao Sehemu ya Jangwa Usiku Ina baridi sana mchana Kuna kua na jua upepo..Dodoma Kuna baridi na upepo
 
Dodoma ipi yenye lami kote?[emoji3526][emoji3526][emoji3526]unapajua mpwayungu wewe?makanda?Manda?Fufu?chipogolo?Kuna balaa huko asehhh...Dodoma Kuna Vumbi baya sana Sijapata kuliona
Acha kujitoa ufahamu umesoma title ya thread au umekurupuka kutokana na chukizako+wivu kwa Dodoma.Kinachozungumziwa ni miji sio mikoa.Sikuzote huwa unakua negative kuhusu Dom wewe mdada.Sijui walikukosea nini watu wa huko ....sijawahi kuona ukicomment chochote positive kuhusu Dom.
 
Dodoma ipi yenye lami kote?[emoji3526][emoji3526][emoji3526]unapajua mpwayungu wewe?makanda?Manda?Fufu?chipogolo?Kuna balaa huko asehhh...Dodoma Kuna Vumbi baya sana Sijapata kuliona
Acha kutaja vijijini huko,kwa jinsi hiyo hakuna kijiji nchi hii kisicho na vumbi,ukiondoa vile vya mikoa ya pwani ambako ardhi yake ni ya kichanga,hapa tunazungumzia urban,Dodoma kwa sasa pako vizuri sana ukilinganisha na miaka 20 iliyopita...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…