Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Bado haujajibu swali ulitaka dunia iweje na binadamu tuweje ili ndo uamini kuwa mungu yupo
Unaamini vipi kitu hakipo, na hicho ambacho ngozi nyeupe kakuletea kina mashaka na kinajichanganya Sana, yaani ni kiumbe Fulani katili sana
 
Ndio maana nilikuuliza unakubali mungu wako ni perfect ila hajaumba viumbe perfect? Yaani kitu unachokiita perfect kimeshindwa kuunda kitu perfect huo uperfect unatokea wapi?
 
Kwa mantiki hiyo ya uhuru wa kujichagulia. Kwanini basi uchawi , uganga wa jadi, kupiga ramli,arbotion kunakatazwa na dini ndo ionekane ni spesho,kwamba watu wana uhuru wa kujichagulia na si hivo vingine?
 
Kama ana uwezo wa kuona dhambi utakazofanya ukiwa duniani na bado akakuumba halafu baada kifo ukaenda motoni, maana yake Mungu/Allah alimuumba ili akuchome Moto, maana toka anakuumba alijua mwisho wako ni motoni
Mungu alituumba ili tuje TUMUABUDU.na si vinginevyo
 
Kwa hyo unataka kusema hakuna binadamu wa kwanza?
Binadamu wa kwanza Hayupo.

Ndio maana Duniani kuna binadamu wenye rangi tofauti na DNA 🧬 tofauti.

Binadamu tuna Genes tofauti.

Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wahindi weusi, wahindi weupe n.k na tuko na utofauti mkubwa sana wa miili yetu kwenye ku adapt mazingira na mifumo yake.

Sasa huwezi kusema kwamba kuna binadamu wa kwanza kwenye dunia iliyo jaa binadamu wengi wenye utofauti.

Kama binadamu wa kwanza angekuwepo, Binadamu wote tungekuwa wa aina moja tu kufuata Genes za huyo Binadamu wa kwanza.
 
Kama Mungu aliumba binadamu wote tuje tumwabudu na si vinginevyo, Mbona sisi Atheists hatumwabudu?

Au Mungu huyo haku tuumba?

Au sisi Atheists au mimi infropreneur sio binadamu?
Sasa kama unakaza future unataka akushikie bakora?si utakufa utakwenda kuonana nae
 
Sasa binadamu tumetoka wapi?
 
Kama Mungu aliumba binadamu wote tuje tumwabudu na si vinginevyo, Mbona sisi Atheists hatumwabudu?

Au Mungu huyo haku tuumba?

Au sisi Atheists au mimi infropreneur sio binadamu?
Ukishakubali wewe ni binadamu afu ukapinga uwepo wa abrahamac god unakuwa unafanya contradiction. Nje ya propaganda za abrahamac god hakuna binadamu bali kuna watu.According to abrahamac fairy tales Adamu ni binadamu wa kwanza na waliofuata nyuma yake wanaitwa binadamu.
 
Kwa mantiki hiyo ya uhuru wa kujichagulia. Kwanini basi uchawi , uganga wa jadi, kupiga ramli kunakatazwa na dini ndo ionekane ni spesho,kwamba watu wana uhuru wa kujichagulia na si hivo vingine?
Wewe unaipinga dini, kwa nini unaifanya dini bado iwe dira yako? Kwa nini unaiga inachofanya dini wakati wewe unataka kutoka kwenye dunia ya dini?

Kwa nini unaicopy dini kwamba dini inapinga wasioamini, na wewe ambaye huamini unapinga dini?

Huoni mpaka hapo unakuwa bado unaifanya dini ikupangie maisha yako, badala ya kujitungia mfumo mwingine wa maisha?

Watu wengine tuliotoka kwenye dini hatusumbuliwi na waamini dini. Tunawaachia uhuru wao kwenye imani, ingawa tukija kwenye facts tuna wa set straight.

Kuhusu swali lako, wachawi, waganga wa jadi, kupiga ramli zote hizo ni imani tu, na as long as hawamdhuru mtu, waachiwe tu watimize imani zao, na hivyo ndivyo mtu asiyeamini dini kama mimi anatimiza uhuru wa kuamini wa kila mtu.

Watu wa dini wana haki ya kusema kwamba dini zao haziruhusu mambo hayo, and that is OK. There is nothing special in that. Ila, wewe ukianza kuwaonea gele watu wa dini kwa nini wanaweka mipango yao hivyo, wewe ndiye unawapa u special.

Wewe unaweza kuanzisha jamii yako ya wasioamini, ikasema kwamba waganga wa kienyeji ni watu muhimu katika research za madawa ya asili, hatuwabagui. Tutawa upgrade wafanye mambo kileo na kisayansi zaidi. Umeondoa ubspecial wa watu wa dini hapo. Waganga wa kienyeji kibao watasema hebu tumsikilize huyu mtu hatubagui kama dini zinavyotubagua.
 
Dini ni wizi mtupu!!
 
Mimi najua wasio na imani ndo wanaenda motoni. Swali hilo nimekuuliza kutokana na wewe kusema imani haikupeleki mbinguni kwaio nataka nisikie upande wako,Labda una sifa zingine unazozijua ambazo mimi sizijui
na hakuna sehemu nimesema najua kila kitu.
Miongoni mwa sifa soma waebrania 12:14

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Sasa binadamu tumetoka wapi?
Binafsi naweza kusema kwamba,

Binadamu hatuja tokea popote pale.

Binadamu tulikuwepo, tupo na tutaendelea kuwepo.

Kama binadamu hatukuwepo duniani halafu ghafla bin vuuh! tukawepo,
Je huko tulipokuwepo kabla ya kuwepo duniani Kulitoka wapi?

Au kabla ya Mungu kuumba mbingu na Dunia alikuwa wapi?
Na huko alikokuwa kulitoka wapi?

Mkuu hapo kutakuwa na mtiririko wa maswali yasiyo na mwisho wa kila kitu kilitoka wapi?

Hata chanzo, cha chanzo, cha chanzo cha chanzo, cha ulimwengu either ni mungu au anything else, kitakuwa kimetoka wapi?

Hatuwezi kujua tusicho kijua, ila tuna punguza tusivyo vijua kwa kujifunza kadiri muda unavyokwenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…