Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Na wewe kutokujua kwako Dunia imekuwepo vipi, Sio Sababu ya kusema kwamba Dunia iliumbwa na Mungu.

Wewe, Sema hujui dunia imekuwepo vipi, sio kuhalalisha uongo uongo wa kwamba Mungu ndiye Muumbaji wa dunia ilhali huna uthibitisho.
Tunamjua mungu kupitia vitabu vyake,lete mwingine anayedai kuwa dunia ni yake tofauti na mungu
 
Kumbe wewe unaamini akili unazo ila haujui zinatoka wapi.ILA KUAMINI MUNGU HAUTAKI SABABU HAUJUI KATOKA WAPI.sasa kwanini usiamini kuwa hakuna AKILI
 
Thibitisha kauli Yako ukishindwa ichunge
Biblia ni kitabu kinachoelezea historia ya mambo ya zamani, sina hakika kama yote yaliyoandikwa mule yalikuwepo kweli ila kuna mambo mengine ukisoma tu yanaonekana ni uongo wa waziwazi. Quran ukiisoma utaona kwamba mwandishi wake alikuwa ameisoma vizuri biblia na akahisi ina makosa na kutaka kuyarekebisha ndipo akaharibu kabisa. Quran ni kitabu kilichojaa stori za kujitungia tu, kama we hulioni hilo tambua kwamba una ufikiriaji mdogo sana.
 
" Uelewa mdogo wa wanafunzi ndo unaoleta kikanganyiko na kusababisha wao kutoelewa somo la chemistry na kufeli, ila somo la chemistry halina shida"

Uliza kama hujui, uache ujuaji kukufuru mambo usiyoyajua.
 
Kumbe wewe unaamini akili unazo ila haujui zinatoka wapi.ILA KUAMINI MUNGU HAUTAKI SABABU HAUJUI KATOKA WAPI.sasa kwanini usiamini kuwa hakuna AKILI
Akili ni nini?

Unaweza kuthibitisha kwamba una Akili?
 
Tunamjua mungu kupitia vitabu vyake,lete mwingine anayedai kuwa dunia ni yake tofauti na mungu
Mungu ni nini?

Leta uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Mwambie huyo Mungu aje hapa athibitishe kwamba hii dunia ni yake.

Sio unatetea fictional character asiye kuwepo.
 
Mungu ni nini?

Leta uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Mwambie huyo Mungu aje hapa athibitishe kwamba hii dunia ni yake.

Sio unatetea fictional character asiye kuwepo.
unataka mpaka aje nyumbani kwako akwambie yeye ndo mungu?.kwani wazazi wako wakati wanataka kukuzaa walikwambia wanataka kukuzaa?
 
" Uelewa mdogo wa wanafunzi ndo unaoleta kikanganyiko na kusababisha wao kutoelewa somo la chemistry na kufeli, ila somo la chemistry halina shida"

Uliza kama hujui, uache ujuaji kukufuru mambo usiyoyajua.
Jikite katika hoja
Karibu sana.
 
unataka mpaka aje nyumbani kwako akwambie yeye ndo mungu?.kwani wazazi wako wakati wanataka kukuzaa walikwambia wanataka kukuzaa?
Hakuna mtu anayetaka mungu aje nyumbani kwake, hukuwahi kuelewa kabisa! Na hii inashangaza.

Embu tafuta sehemu mtu anasema tunahitaji kumuona mungu aje nyumbani kwetu,

Jikite katika mada uliomba mistari mungu akiua watu umepewa lakini bado hakuna ulilojibu.

Jikite katika mada mkuu karibu sana.
 
Wewe umejuaje kama Mungu hayupo ?

Tuambie imekuwaje hii Dunia ikawa hivi ilivyo ? Kama hujui hili, unapata wapi uhalali wa kudai ya kuwa Mungu hayupo ?

Nukta ya pili, umejuaje kama kila mtu amezaliwa ni Atheist ? Hujui kama Atheism ni ugonjwa wa akili ?

Unaposema maandiko ya kidini ni hadithi za kutunga, tunaomba ushahidi huo utuambie nani ametunga hizi habari, hasa jikite katika kuelezea Qur'an.

Nukta ya tatu, kila mtu anazaliwa akiwa Muislamu.
 
Mungu ni nini?

Leta uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Mwambie huyo Mungu aje hapa athibitishe kwamba hii dunia ni yake.

Sio unatetea fictional character asiye kuwepo.
Kwanini mnapenda kurudia maswali ambayo mshajibiwa ?

Kwanini unatumia kiulizi Cha "nini ?" juu ya kitu chenye maarifa, nguvu, hekima, ujuzi ? Swali lako la uongo

Uwepo wako wewe ni uthibitisho ya kuwa Mungu yupo.

Mungu haamrishwi sababu yeye amejitosheleza, haulizwi kwa analo lifanya, Wala hana haja ya kuja sababu kila kitu amekiweka wazi na hakuna kitu chenye ushahidi mkubwa katika uwepo wake kuzidi uwepo wa Mungu, yaani hata uwepo wako wewe hapo ulipo hauzidi ushahidi wa uwepo wa Mungu.

Thibitisha ya kuwa Mungu ni fictional Character na utuambie nani wa kwanza kumtunga Mungu ?
 
Mkuu,
Unathibitisha vipi kila mtu kazaliwa muislamu?
Angalia nafsi yako, kila mtu anazaliwa katika kumkiri Allah, ndio maana Leo ukienda kwa mtu ambaye hana habari zozote kuhusu Mungu, na akili yake haijaingizwa uchafu ukimuuliza Mungu yuko wapi lazima atakuonyesha yuko juu. Hili ni umbile ambalo kila mwanadamu ameumbiwa kwako.

Kwa minajili hiyo tunasema ni Muislamu sababu anakuwa ameumbwa katika umbile la kujisalimisha na kumkiri Allah.
 
Akili ni nini?

Unaweza kuthibitisha kwamba una Akili?
Akili ni uwezo alio pewa mja au nguvu aliyo nayo mja inayo mzuia kufanya mabaya au kukosea. Yaani kwa lugha nyepesi ni kizuizi.

Naam naweza kuthibitisha ya kuwa akili ninayo.

Wewe unaweza kuthibitisha ya kuwa Mungu hayupo ? Kama unaweza thibitisha.
 
Nafikiri ungejikita katika mada mkuu.

Tumeweka mistari yenye mikanganyiko Hapo juu.
Unaweza ukaondoa contradiction hizo

Karibu sana.
 
Rudia comment ya niliyemjibu,uisome vizuri.anataka uthibitisho gani wa kuwa mungu yupo.kama sio kwenye vitabu vyake na vile vinavyoviona duniani?au anataka aende nyumbani kwake amgongee mlango amwambie mimi ndo mungu?
 
Uwepo wake una mkanganyiko Ndio ambayo hivyo anavyodai vtabu vyake havieleweki.

Tukasema anza kupitia moja baada ya nyingine uzitatue

Karibu mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…