Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Na wewe kutokujua kwako Dunia imekuwepo vipi, Sio Sababu ya kusema kwamba Dunia iliumbwa na Mungu.

Wewe, Sema hujui dunia imekuwepo vipi, sio kuhalalisha uongo uongo wa kwamba Mungu ndiye Muumbaji wa dunia ilhali huna uthibitisho.
Tunamjua mungu kupitia vitabu vyake,lete mwingine anayedai kuwa dunia ni yake tofauti na mungu
 
Kuna ulazima upi wa kwamba Akili zimetoka mahali fulani?

Huko akili zilipotoka, na kwenyewe kulitoka wapi?

Kuambiwa hata uongo unaweza kuambiwa.

Kuambiwa kuna Mungu hakuthibitishi kwamba Mungu yupo, ni maneno tu ya kuhadithiwa.

Thibitisha Mungu yupo na si maneno ya kuambiwa au mawazo yako ya kufikirika tu.
Kumbe wewe unaamini akili unazo ila haujui zinatoka wapi.ILA KUAMINI MUNGU HAUTAKI SABABU HAUJUI KATOKA WAPI.sasa kwanini usiamini kuwa hakuna AKILI
 
Thibitisha kauli Yako ukishindwa ichunge
Biblia ni kitabu kinachoelezea historia ya mambo ya zamani, sina hakika kama yote yaliyoandikwa mule yalikuwepo kweli ila kuna mambo mengine ukisoma tu yanaonekana ni uongo wa waziwazi. Quran ukiisoma utaona kwamba mwandishi wake alikuwa ameisoma vizuri biblia na akahisi ina makosa na kutaka kuyarekebisha ndipo akaharibu kabisa. Quran ni kitabu kilichojaa stori za kujitungia tu, kama we hulioni hilo tambua kwamba una ufikiriaji mdogo sana.
 
Wakuu habari zenu?binafsi nimekuwa nikifuatilia mijadala mingi sana kuhusu mikanganyiko(contradiction) katika vitabu vya dini.

Nimekuwa nikifatilia nyuzi nyingi za kiranga kuhusu kupinga uwepo wa mungu, tukitoa mihemko tukajenga hoja kwa mantiki (logical) character ya mungu mwenye nguvu zote, mwenye upendo wote na ajuaye yote hayupo na haiwezi kufit kwenye mizani ya mantiki.

Nimekuwa nikisoma Biblia na imekuwa ikijikanganya yenyewe na bado ikidai kwamba mungu huwa hakosei. Leo nitaonyesha baadhi ya mikanganyiko hiyo ambayo hata kiranga amekuwa akiiweka.hizi ni baadhi ya verse zenye mikanganyo👇

Mwanzo 1:3-5 BHN
Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.

Mwanzo 1:14 BHN
Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka

Mwanzo 1:11-13 BHN
Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu.

Mwanzo 2:4-9 BHN
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia, Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima. Hata hivyo, maji yalitoka ardhini yakainywesha ardhi yote. Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai. Kisha Mwenyezi-Mungu akapanda bustani huko Edeni,

Mwanzo 1:26-27 BHN
Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. Hapa mungu aliumba mwanamume na mwamke.

Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.

(Mbele kidogo mungu anaumba mwanaume)utaona jinsi gani anavyosahau kurekodi matukio katika mtiririko ulio sahihi.

Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.

Mwanzo 6:6 BHN
Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake

Hesabu 23:19 BHN
Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize?

Kutoka 12:13 BHN
Basi, ile damu itakuwa ishara yenu ya kuonesha nyumba mtakamokuwa. Nami nitakapoiona hiyo damu, nitawapita nyinyi, na hamtapatwa na dhara lolote wakati nitakapoipiga nchi ya Misri.

Mithali 15:3 SRUV
Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.

( kwenye kutoka mungu wa kiyahudi anatoa maagizo wapake damu kwenye vizingiti vya milango ili asije kujichanganya, lakini mungu huyo huyo anajinasibu katika mithali macho yake yapo kila mahali)

Kutoka 20:14 BHN
“Usizini.

HOSEA 1:2
2 Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.

Karibuni tujadili bila kashfa tujadiliane, hizi ni baadhi ya mikanganyiko iliyopo katika biblia.

Kwanini mungu mkamilifu kitabu chake kiwe na mikanganyiko kiasi hiki?

Mungu anasifa zote za binadamu anasahau, anabadili mawazo yake, ana hasira, Ana wivu, katili, na tabia zingine nyingi za kibinadamu.

" Uelewa mdogo wa wanafunzi ndo unaoleta kikanganyiko na kusababisha wao kutoelewa somo la chemistry na kufeli, ila somo la chemistry halina shida"

Uliza kama hujui, uache ujuaji kukufuru mambo usiyoyajua.
 
Kumbe wewe unaamini akili unazo ila haujui zinatoka wapi.ILA KUAMINI MUNGU HAUTAKI SABABU HAUJUI KATOKA WAPI.sasa kwanini usiamini kuwa hakuna AKILI
Akili ni nini?

Unaweza kuthibitisha kwamba una Akili?
 
Tunamjua mungu kupitia vitabu vyake,lete mwingine anayedai kuwa dunia ni yake tofauti na mungu
Mungu ni nini?

Leta uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Mwambie huyo Mungu aje hapa athibitishe kwamba hii dunia ni yake.

Sio unatetea fictional character asiye kuwepo.
 
Mungu ni nini?

Leta uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Mwambie huyo Mungu aje hapa athibitishe kwamba hii dunia ni yake.

Sio unatetea fictional character asiye kuwepo.
unataka mpaka aje nyumbani kwako akwambie yeye ndo mungu?.kwani wazazi wako wakati wanataka kukuzaa walikwambia wanataka kukuzaa?
 
" Uelewa mdogo wa wanafunzi ndo unaoleta kikanganyiko na kusababisha wao kutoelewa somo la chemistry na kufeli, ila somo la chemistry halina shida"

Uliza kama hujui, uache ujuaji kukufuru mambo usiyoyajua.
Jikite katika hoja
Karibu sana.
 
unataka mpaka aje nyumbani kwako akwambie yeye ndo mungu?.kwani wazazi wako wakati wanataka kukuzaa walikwambia wanataka kukuzaa?
Hakuna mtu anayetaka mungu aje nyumbani kwake, hukuwahi kuelewa kabisa! Na hii inashangaza.

Embu tafuta sehemu mtu anasema tunahitaji kumuona mungu aje nyumbani kwetu,

Jikite katika mada uliomba mistari mungu akiua watu umepewa lakini bado hakuna ulilojibu.

Jikite katika mada mkuu karibu sana.
 
Maandiko yote ya kidini ni Hadithi za kutungwa sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.

Mungu hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Dhana ya uwepo wa Mungu mwema, mkamilifu, mwenye kujua yote, muweza wa vyote na mwenye upendo na huruma Kwenye Dunia iliyojaa uovu, ukatili, uasi, mabaya na shida za kila aina ni uthibitisho kwamba Mungu huyo Hayupo.

Mungu mkamilifu, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na uovu?

Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba Binadamu wema tu wasio na uwezo wa kutenda dhambi, ukatili na ubaya?

Mungu mwenye kujua yote, Hakujua kwamba uovu, ukatili na mabaya yatakuja kuwepo duniani ayadhibiti mapema?

If God wanted us in Heaven Why he created us on Earth?

Mungu huyo, Alishindwaje kutuumba tukiwa mbinguni directly kama alitaka tuwe Mbinguni?

God is a fictional character invented by religion to scam people.

Religion convinced people that there's an invisible man beyond the sky who watches everything.

Human beings created God through assumptions Based on things beyond their imaginations.

God doesn't EXIST.

Kila mtu huzaliwa Atheist hata wewe ulizaliwa Atheist mpaka pale ulipo aminishwa kwamba kuna invisible creature beyond the sky anaitwa Mungu.

Hizi ni fiction stories za kurithishwa.
Wewe umejuaje kama Mungu hayupo ?

Tuambie imekuwaje hii Dunia ikawa hivi ilivyo ? Kama hujui hili, unapata wapi uhalali wa kudai ya kuwa Mungu hayupo ?

Nukta ya pili, umejuaje kama kila mtu amezaliwa ni Atheist ? Hujui kama Atheism ni ugonjwa wa akili ?

Unaposema maandiko ya kidini ni hadithi za kutunga, tunaomba ushahidi huo utuambie nani ametunga hizi habari, hasa jikite katika kuelezea Qur'an.

Nukta ya tatu, kila mtu anazaliwa akiwa Muislamu.
 
Mungu ni nini?

Leta uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Mwambie huyo Mungu aje hapa athibitishe kwamba hii dunia ni yake.

Sio unatetea fictional character asiye kuwepo.
Kwanini mnapenda kurudia maswali ambayo mshajibiwa ?

Kwanini unatumia kiulizi Cha "nini ?" juu ya kitu chenye maarifa, nguvu, hekima, ujuzi ? Swali lako la uongo

Uwepo wako wewe ni uthibitisho ya kuwa Mungu yupo.

Mungu haamrishwi sababu yeye amejitosheleza, haulizwi kwa analo lifanya, Wala hana haja ya kuja sababu kila kitu amekiweka wazi na hakuna kitu chenye ushahidi mkubwa katika uwepo wake kuzidi uwepo wa Mungu, yaani hata uwepo wako wewe hapo ulipo hauzidi ushahidi wa uwepo wa Mungu.

Thibitisha ya kuwa Mungu ni fictional Character na utuambie nani wa kwanza kumtunga Mungu ?
 
Mkuu,
Unathibitisha vipi kila mtu kazaliwa muislamu?
Angalia nafsi yako, kila mtu anazaliwa katika kumkiri Allah, ndio maana Leo ukienda kwa mtu ambaye hana habari zozote kuhusu Mungu, na akili yake haijaingizwa uchafu ukimuuliza Mungu yuko wapi lazima atakuonyesha yuko juu. Hili ni umbile ambalo kila mwanadamu ameumbiwa kwako.

Kwa minajili hiyo tunasema ni Muislamu sababu anakuwa ameumbwa katika umbile la kujisalimisha na kumkiri Allah.
 
Akili ni nini?

Unaweza kuthibitisha kwamba una Akili?
Akili ni uwezo alio pewa mja au nguvu aliyo nayo mja inayo mzuia kufanya mabaya au kukosea. Yaani kwa lugha nyepesi ni kizuizi.

Naam naweza kuthibitisha ya kuwa akili ninayo.

Wewe unaweza kuthibitisha ya kuwa Mungu hayupo ? Kama unaweza thibitisha.
 
Angalia nafsi yako, kila mtu anazaliwa katika kumkiri Allah, ndio maana Leo ukienda kwa mtu ambaye hana habari zozote kuhusu Mungu, na akili yake haijaingizwa uchafu ukimuuliza Mungu yuko wapi lazima atakuonyesha yuko juu. Hili ni umbile ambalo kila mwanadamu ameumbiwa kwako.

Kwa minajili hiyo tunasema ni Muislamu sababu anakuwa ameumbwa katika umbile la kujisalimisha na kumkiri Allah.
Nafikiri ungejikita katika mada mkuu.

Tumeweka mistari yenye mikanganyiko Hapo juu.
Unaweza ukaondoa contradiction hizo

Karibu sana.
 
Hakuna mtu anayetaka mungu aje nyumbani kwake, hukuwahi kuelewa kabisa! Na hii inashangaza.

Embu tafuta sehemu mtu anasema tunahitaji kumuona mungu aje nyumbani kwetu,

Jikite katika mada uliomba mistari mungu akiua watu umepewa lakini bado hakuna ulilojibu.

Jikite katika mada mkuu karibu sana.
Rudia comment ya niliyemjibu,uisome vizuri.anataka uthibitisho gani wa kuwa mungu yupo.kama sio kwenye vitabu vyake na vile vinavyoviona duniani?au anataka aende nyumbani kwake amgongee mlango amwambie mimi ndo mungu?
 
Uwepo wake una mkanganyiko Ndio ambayo hivyo anavyodai vtabu vyake havieleweki.

Tukasema anza kupitia moja baada ya nyingine uzitatue

Karibu mkuu.
 
Back
Top Bottom