Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Uwepo wake una mkanganyiko Ndio ambayo hivyo anavyodai vtabu vyake havieleweki.

Tukasema anza kupitia moja baada ya nyingine uzitatue

Karibu mkuu.
huo mkanganyiko mnaousema hauwezi kusababisha kuwa mungu asiwepo.
Bila ya hata vitabu kwa kutumia akili tu unaweza kufikiri na kujiuliza DUNIA YA NANI?
 
huo mkanganyiko mnaousema hauwezi kusababisha kuwa mungu asiwepo.
Bila ya hata vitabu kwa kutumia akili tu unaweza kufikiri na kujiuliza DUNIA YA NANI?
Dunia ya “Nani” huoni kwamba hilo swali ulishalipatia majibu yako? Ina maana unafahamu Halafu unakuja kuuliza!

Wanasayansi wengi walikuja na theory nyingi zinazoendelea kufanyiwa tafiti.
Ila watu wengi wapo radhi kukubali kuambiwa hapo mwanzo mungu Aliumba mbingu na nchi.
Bila ya kuelezea aliumba vipi kwa madai ya kwamba yeye ni muweza wa yote!

Ndipo hapa tunapohoji huo uwezo wake wote upo wapi?
Kama sayansi bado haijajua chanzo cha wapi dunia ilipotokea hilo hali justify kwamba mungu yupo ina maana kwamba bado hatujui.

Thibitisha mungu mwenye uwezo wote Kwanini kitabu chake kiwe na mikanganyiko?
 
Thibisha kauli yako broo Ili uwe kafiri wa kwanza kuithibitishia Dunia kuwa Quran Ina maneno ya kutunga au uongo

Maana Qurani yenyewe inasema ndani yake hakuna maneno ya kutunga Wala ya uongo

Quran 2:2-
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu,
 

 
🚮🚮
 
Mungu hayupo kwa sababu mabaya yapo. Angekuwepo yasingekuwepo, pili kutojua kwanini ulimwengu upo hivi haithibitishi mungu yupo, kukimbilia jibu la kwamba mungu ndo katengeneza ulimwengu hivi ulivyo ni kutafuta psychological relief juu ya maswali yanayohitaji majibu yasiyokuwa na ukakasi.
Kusema atheism ni ugonjwa, nionyeshe mtu alielazwa hospital akipatiwa dozi ya atheism.
 
Achana na huyo Kisai hanaga hoja zozote zaidi ya kutetea uislamu.

Kisai ni muislamu mwenye itikadi kali sawa na magaidi ya Islamic state,
Al-Qeida, Al-shabaab na Boko Haram.

Ni sawa na kumwelewesha chizi
 
Kwani kusema ni kitabu kisichokuwa na shaka ndo uhalisi kwamba hakina shaka? Huyo mwandishi kaandika hivyo kujitengenezea ulinzi wa kutokuhojiwa ila ni kitabu chenye udhaifu wa hali ya juu. Upuuzi umejaa sana mule.

Upuuzi wa kwanza,
Kuna sehemu mwandishi anasema mbingu zinatetemeka na kutikisika pale ambapo Yesu anaitwa mwana wa Mungu. Huo ni uongo wa wazi, mbingu haiwezi kutikisika kwa jambo la namna hiyo.

Upuuzi wa pili,
Kuna sehemu panasema Mungu na malaika zake wanamsalia mtume.
Huo ni ujinga wa viwango vya PhD kuona Mungu nae anasali.

Niendelee au tujadili hayo kwanza?
 
Mungu hana haja ya kueleza aliumba vip dunia.kwani wakatiunabadilika kutoka shahawa kuwa binadamu alikwambia amekugeuza vipi?
 
Biblia imejimwambafai yenyewe kwamba ni perfect na haina madhaifu? Hiyo relation haiendani na biblia na ni kuikosea biblia hadhi yake. Hao waandishi wa habari unaowasema walikuwa na roho mtakatifu kama waandishi wa kwenye bible?
That's what you are saying. Hebu onyesha hayo madhaifu unayosema kama hayaendani na mfano nilioutoa na je umejibu maswali niliyouliza? Kitu nilichotaka kukuonyesha ni kwamba Biblia imeandikwa kwa lengo fulani na iliyowalenga hawana shida nayo kwa sababu wanaelewa ni nini kinachozungumzwa. Wale wasio walengwa kama wewe ndiyo wanaoona shida. Na kila kitu kiko hivyo. Wale wanaohusika hawaoni shida, lakini wasiohusika ndio wa kwanza kuwaambia wahusika kwamba kuna shida. Wewe unaweza ukawa na utaratibu wako wa kula nyumbani na wanafamilia wote wanaufahamu na hawana shida na huo utaratibu. Lakini majirani wanaweza wakaanza kusema "siku hizi familia X ina shida ya chakula hata wameweka utaratibu wa kula usio wa kawaida." Je, shida inakuwa kwako na familia yako au ni hao wanaosema kuna shida? Hata Biblia ni hivyo. Ina maudhui ambayo mtu anayesoma kama kitabu cha historia atapata shida kuielewa kwa sababu haikuandikwa kwa lugha ya historia (chronology of events in time). Sasa kuna watu wanaisoma na kulazimisha isomwe kama kitabu cha historia. Yaani kwamba kulikuwa na location fulani hapa duniani inaitwa "bustani ya Edeni" na humo Mungu alimfinyanga Adamu na kisha akampulizia hewa, akawa hai. Kisha Mungu akamletea usingizi wa pono na alipokuwa amelala, Mungu akanyofoa baadhi ya mbavu (na of course Adamu alibaki anavuja damu nyingi na huenda alienda hospitali kutibiwa) na kisha akamtengeneza Eva (Hawa). Na kabla ya haya yote Mungu alikuwa ameshaumba ulimwengu kwa siku 5 na kisha Mungu ndipo alipomfinyanga Adamu siku ya 6 na Mungu akawa amechoka na siku ya 7 akapumzika. Sasa ukisoma Biblia kwa mtindo huo, lazima utapata shida. Lakini sehemu mbalimbali Biblia imeandikwa "na haya yameandikwa ili mpate kuamini". Ikiwa na maana kwamba unasoma Biblia siyo kama historia, bali kwa macho ya imani. Ukisoma Biblia kwa macho ya imani, ina maana utasoma 'narrative' na kupata "funzo fulani" (ujumbe) unaomhusu mtu anayeisoma kwa macho ya imani. Je, wewe unasoma Biblia kama historia au kitabu cha imani ambacho masimulizi yake ni tofauti na kusoma historia Shaka Zulu, au vita vya majimaji au vita vikuu vya dunia? Je, unasomaje wewe? Hata fizikia huwezi kuisoma kama historia au hesabu na lazima usome hayo masomo kwa mantiki hiyo au kwa lengo lililokusudiwa na siyo unavyotaka wewe usome.
 
Kusema tu mungu alichoka siku ya saba akapumzika,akastarehe tayari ni mkanganyiko, inakuaje mungu nae anachoka hadi anapumzika kama binadamu?
 

Mkuu kwa mujibu wa Bibilia “maneno matakatifu ya Mungu” Bibilia ni kwaajili ya watu wote duniani

Sasa unaposema Bibilia ni kwaajili ya walengwa fulani unamaanisha nini?

Kumbe kuna wengine Bibilia haiwahusu na wanaketa kiherehere kuhoji?
 
Kusema tu mungu alichoka siku ya saba akapumzika,akastarehe tayari ni mkanganyiko, inakuaje mungu nae anachoka hadi anapumzika kama binadamu?
Siyo kwamba mimi ndivyo ninavyoamini. Nimeandika jinsi wewe unavyosoma Biblia na ku'miss' the point. Yaani unasoma unachanganya mambo na badala ya kuona kwamba umechanganya unaona Biblia ndiyo iliyochanganya. Ndicho nilichotaka kukuonyesha na naona hujanielewa pia. Shida iko hapo.
 
huo mkanganyiko mnaousema hauwezi kusababisha kuwa mungu asiwepo.
Bila ya hata vitabu kwa kutumia akili tu unaweza kufikiri na kujiuliza DUNIA YA NANI?

No body knows
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…