Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Wote tunajifunza hapa.

Wewe umejifunza nini mpaka sasa?
Dooh..kwakwel mimi namuamin Mungu na mkristo japo wa maghumashi. Ila kuna time huwa napata was was sana na vitu kwel huwa vinanipa was was sana kama Yupo maana dah!! Lakin kuna time pia kuna mambo yanayonifanya nirud kwenye msatari kujilazimisha kuamini neno la Mungu maana mambo mengine yameshanitokea na kama hayangekua maombi ya viongozi wa dini na walokole najua kabisa nisingetoboa.

Mfano hiv karibun mwanangu almanusura apate mental breakdown akawa kama anaongea vitu vya ajabu ghafla na nimehangaika nae mahospitalin hakupata nafuu mpaka tulipo amua kufuata MAOMBI na now he ia very more than fine. Ofcz alishapone and is back to school.

SASA HAPO MKUU NDIO HUWAGA NASEMA MUNGU YUPO
 
Inaonesha ni kwajinsi gani Ambavyo Elimu na sayansi haijakukomboa kwamambo ya fuatayo
1.kuwepo kwa contradiction Hakumaanishi kwamba Mungu hayuko
Thibitisha Mungu huyo yupo.
Na si mawazo yako ya kufikirika tu.
2.Msomi unae toa fact Kama Mungu hayupo na hiliali Ata Biblia yenyewe inaonekana hujawai kuisoma una sikia tu historia nta kwambia kwann unaonekana Biblia inaonekana hujawai kuisoma
Wewe ndio hujaisoma Biblia kwa fikra huru uka ielewa na kuipambanua vizuri.

Umesoma biblia kwa imani ya kuaminishwa kwamba chochote kile kilicho andikwa kwenye Biblia ni ukweli hata kama ni uongo na kina Contradictions.

Ndio maana una halalisha kusema pamoja na Contradiction zilizopo kwenye Biblia, Bado Biblia hiyo ni andiko la Mungu.

Kwa vile ndivyo ulivyo pumbazwa kukubali Uongo.

3.Ww kiranga nawenzako woteee
Inaonekana kunashida kwenye akilizenu
Wote Mnajaribu kuingiza sayansi kwenye maswala ya Imani mna sahau kwamba Imani ni Imani tuuu
Na sayansi ni sayansi tuuu
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika. Imani haina uthibitisho wowote ule wa kinacho aminiwa zaidi ya mawazo ya kufikirika tu, Imagination just an illusion.

Ndio maana hata uongo unaweza kuaminiwa kwamba ni ukweli kwenye imani.

Sayansi inaendana na uwepo wa facts, evidences, proves na Logic.

Nini maana ya Imani??
Ni kua na HAKIKA ya mambo YATSRAJIWAYO NI BAYANA YA MBAMBO YA SIO ONEKANA
Imani ni kutokuwa na UHAKIKA wa mambo.

Ndio maana imani haina uthibitisho wowote ule wa jambo lake zaidi ya hadithi hadithi tu za kutungwa na kusadikika.

Huwezi kusema una imani ya kwamba mwanzilishi wa Jamii forums ni Maxence Melo wakati tayari uthibitisho na uhakika wa kwamba jamii forum ilianzishwa na Maxence Melo upo.

Ukisha kuwa na Uhakika wa kitu fulani au jambo fulani, Huitaji imani ya kujua kwamba kitu hicho kipo.


Sasa ww umeambiwa Imani inahusu mambo Ambavyo hayoonekani alaf mtu Ana kwambia anataka proof za kisayansi kwenye maswala ya Imani
Mambo hayo ambayo hayaonekani ulifahamu vipi kwamba
haya onekani?

Ni mambo gani hayo yasiyo onekana?

Na unathibitisha vipi kwamba hayaonekani?
Mf.Mm binafsi nishawai kuumwa Sana kichwa lakin nikajiombea Mimi mwenyewe kwa Jina La YESU nikapona kwamda mfupi tuuu
Logical non sequitur.

Wagonjwa wangapi wame muomba yesu huyo na wana muomba yesu huyo awaponye maradhi na shida zao lakini Nothing happens.

Hakuna kinacho tokea, wana ishia kufa tu na wengine kuendelea kuteseka zaidi.

Unafikiri wagonjwa waliopo hospitalini muhimbili, Ocean road, KCMC, Bugando n.k Hawa muombi Yesu huyo awaponye magonjwa yao?

Mbona wagonjwa hao kutwa kucha wapo hospitalini kutibiwa halafu unadai yesu huyo anaponya?

Nakwambia hivi, Yesu huyo hawezi kuponya chochote kile kwa vile Hayupo.
Haya Sasa niambie ni prove kwamba ni Mungu kaniponya Kama sayansi inavyotaka (sayansi ina taka proof za kibinadamu)
Mungu huyo angekuwa anaponya wagonjwa Kusingekuwa na haja ya kutibiwa hospitalini au kumeza dawa ili upone.
Mungu huyo anatafutwa kwani amepotea?

Mungu huyo amejifichia ni nini hadi atafutwe?
Mungu anatafutwa nakatoa ahadi ya kupatikana Kama mtu ata mtafuta kwa uaminifu
Mungu huyo hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Biblia ni andiko moja la kipumbavu sana lililo jaa Contradiction nyingi sana.
 
Sawa.

Una haki ya kuamini unavyotaka. Hii ni haki yako ya kikatiba. Ni haki ya utu. Ipo katika Universal Declaration if Human Rights.

Kwa hiyo, ikiwa unachoamini ni sahihi, au si sahihi, kweli au uongo, kuamini unavyotaka ni haki yako.

Kwa hivyo, hilo nataka kulipigia mstari, kwamba sina nia ya kujadili imani yako.

Ninachoongelea hapa ni ukweli, ambao huu haujaishia kwenye imani yako.

Mtoto kupata mental breakdown halafu kuombewa na kupona hakudhihirishi Mungu yupo, inawezekana hapo kuna aina fulani ya psychological relief/Placebo effect inapatikana kwa kuamini Mungu yupo na kuombewa.

Kwenye sayansi wanasayansi wakitengeneza dawa mpya, huwa wanaifanyia testing kwa ma group, group moja la wagonjwa linapewa dawa, group lingine halipewi dawa, linaweza kupewa vidonge tu ambavyo si dawa, wanaangalia ma group haya, watu gani waliopewa dawa watapona wangapi, na pia, wale ambao hawajapeea dawa, wamepeea vidonge tu (lakini hawajaambiwa kuwa vidonge hivyo si dawa). Hii ni katika kupima, ile dawa inafanya kazi kivipi.

Mara nyingi wanaonankuwa, kuna watu wanapona kwa imani tu, yani wamepewa vidonge tu visivyokuwa na dawa, lakini hawajaambiwa vidonge havina dawa, na wanapona kwa kuamini kuwa wamepewa dawa.

Hii inaitwa placebo effect.

Kwa hivyo, hata kwenye kuombewa, especially kwenye mental breakdown, mtu anaweza kupona kwa kuombeea, kwa placebo effect tu, na hilo halithibitishi Mungu yupo.
 
DINI ni hadithi za kutumgwa
Lakin

Unaamini BigBang theory
Aliyekwambia na amini Bing theory ni nani?

Mimi siamini kwenye kuamini, Sina imani yeyote ile.

Mimi siamini kwenye theory yeyote ile ya kidini wala kisayansi inayo sema kwamba Dunia iliumbwa.

Dunia haina mwanzo wala mwisho, Dunia ipo siku zote. Dunia haijawahi kutokuwepo kisha ikawepo.

Dunia haijawahi kuumbwa.
Unaamini zamani Binadamu tulikua Sokwee

Dhaaah
Binadamu hajawahi kuwa sokwe huu ni Uongo.
Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Sasa hizo shida anazileta mungu au binadamu ndo tunazileta kwa mikono yetu?
Mungu huyo, Aliumbaje binadamu wenye uwezo wa kuleta shida,uovu,ukatili na dhambi kwenye dunia yake?

Mungu huyo, Alishindwaje kuumba binadamu wasioweza kuleta shida, Uovu, ukatili na mabaya kwenye dunia yake?

Mungu huyo anaweza yote kweli?

Mungu huyo kama hapendi dhambi, uovu, ukatili na mabaya viwepo duniani, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na mambo haya?
 
Out of topic! Jikite katika mada.
 
Ata mm nilishawai kupataga was was Kama ww Sana Sana tunaposoma masomo ya sayansi alaf ukutane na mwalimu ambaye aamin Mungu yupo maneno yake yaneweza kukufanya usiamini Mungu yupo

Ila ashukuriwe MUNGU muweza wa yote ambaye

Kanifundisha kujua kutifautisha Sayansi na Mambo mengine ya kidunia na IMANI

Sasa naweza kutifautisha kwamba DINI ukiingiza kwenye sayansi Sana utaona Wana sayansi waongo
Napia Sayansi ukiingiza kwenye DINI utaona DINI kama DINI

Mambo ya DINI yanafanyika kwa IMANI mf kuponywa kwa IMANI n.k

Sayansi haijui Imani inajia vitendo tuu
Kwamba mtu akimeza dawa itafanya hiv na hiv (mechanism of action) haijui imani

## Mimi mtu asije akanidanganya Mungu hayupo


Atapia nikikumbuka nikiwa na miaka 9 tuu nilishawai kumuombea mtu mwenye mapepo kwa Jina la YESU akaanguka na kupiga makelele wakati huo nilikua na iga tu wa chungaji

Alaf Leo mtu ambaye hata kusoma Biblia ajawai Wala ajui aniambie Mungu hayupooo

Napata wakati mgumu kwell

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Ndomanaaaaa...

Tunge kesha hapa kumbe mdawote tunanabishana nawatu ambaoo hawaamini chochote mpaka sayansi haiamini

Sasa rafiki kama Hauamini chochote unataka kujua Mtu tena Akuaminishe Mungu yupooo

Kwaakilizako inawezekana kwell

Kumfundisha Bubu kuongeaa

Kumbe mwenzetu Imani Hunaa
Alaf tena Hauamini Mungu yupoo

MAMBI YA DINI YANA HITAJI IMANI RAFIKI
kama hata Imani ya kuamini mambo ya sayansi haunaa

Sembuse kuamini kitu USICHOKIONA

DINI yake Imani
Imani kumbe mwenzetu Hunaa
Alaf unataka mtu akusibitishie Mungu yupo dhuuuu...

Mungu hanekani kwa machooo hivi Wala hashikiki

Ndo utamwaminiii....atakama mtu akusibitishie apaaa



Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.

Makosa yaliyofanywa na binadamu wenzako katika bibilia wewe unamsingizia Mungu?

Ndio maana Mungu amekupa akili nyingi kuliko viumbe wote aliyowaumba Ili uweze kutumia akili yako kukabiliana na changamoto ndogondogo kama hizo

Ila hapo inaonekana hao waliyoichakachua bibilia wanakuli kukuzidi wewe maana wameweka maneno Yao wakakuambia haya yote ni Maneno ya Mungu na wewe umekubali inamaana wewe ni kilaza
 
Jikite katika hoja nimeweka mistari hapo juu anasema hivi baadae anabadilika.

Jibu hoja mkuu
Karibu sana.
 
Ndio maana nakwambia hivi, Mungu huyo Hayupo katika uhalisia ila katika dhana ya kufikirika tu.
 
Human beings created God through assumptions Based on things beyond their imaginations.
Hii kitu kama ina ukweli lakini nikifikiria kuhusu ulimwengu wa giza yaani wachawi,waganga,majini, mapepo n.k Najikuta na rudi Kuamini Mungu Yupo.
 
Jikite katika hoja nimeweka mistari hapo juu anasema hivi baadae anabadilika.

Jibu hoja mkuu
Karibu sana.
Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.

Waliobadisha hayo mandiko Hadi yanajichanganya ni watu sio Mungu
 
Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.

Waliobadisha hayo mandiko Hadi yanajichanganya ni watu sio Mungu
Mungu karuhusu kitabu chake kichezewe? Ina maana kazidiwa akili?

Madai ya biblia ni kitabu kisicho na makosa huwa yanatoka wapi na unadai wapo waliobadilisha?
 
Mungu karuhusu kitabu chake kichezewe? Ina maana kazidiwa akili?

Madai ya biblia ni kitabu kisicho na makosa huwa yanatoka wapi na unadai wapo waliobadilisha?

Wewe nani aliyekuambia bibilia ni kitabu kisicho na Makosa?

Wakati nabii wa Mungu Yeremia anasema Bibilia imechakachuliwa

Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
 
Afadhali umekuwa mkweli,
unakubaliana nami kwamba mungu si mwenye nguvu zote?

Mkuu karibu bado kuna mikanganyiko mingi ambayo inahitaji ufafanuzi
 
Human beings created God through assumptions Based on things beyond their imaginations.
Hii kitu kama ina ukweli lakini nikifikiria kuhusu ulimwengu wa giza yaani wachawi,waganga,majini, mapepo n.k Najikuta na rudi Kuamini Mungu Yupo.
Mkuu wewe kama wewe ushawahi kuona, ku experience na kuthibitisha uwepo wa ulimwengu wa giza,wachawi, mapepo na majini?

Au una amini kwenye story za kuambiwa na kusikia sikia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…