Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

MASWALI MAZURI, NAOMBA NIJARIBU KUJIBU.
Intro
Biblia sio kitabu, ni muunganiko wa vitabu. Havijaandikwa na Mungu personally bali vimeandakwa na wanadamu kwa maagizo na msaa wa Roho wa Mungu.
Kama kuna makosa yeyote ni makosa ya kiuandishi ya kibinadamu sio ya kimaana.
1. Kitabu cha mwanzo hakijaandikwa kwa kufauata mfululizo wa mfuatano wa matukio.
Kiliandikwa kwa mfumo wa flashback.
Ndio maana tukio la kuumbwa mwanga limezungumzima mara mbili, mara ya pili ameongezea kile ambacho alikuwa hajaandika.
Vile vile na swala la kuubwa kwa mimea limeandikwa kwa flashback, ndio maana imekuchanganya.
2. Mfumo wa Mungu ni kufanya kazi na wanadamu, ameumba wanadamu wawe washilika wake.
Sio kwamba Mungu hawezi kufanya vyote bali kuna sehemu anamuachia mwanadamu naye awe mshiliki katika kazi. Aliwaagiza wana Israel wapake damu kwenye milango sio kwa sababu hawezi kuona Bali nao washiliki katika ukombozi wao na alituma malaika kufanya hiyo kazi ya kupiga wamsri ambao pia ni viumbe.
Pia kupaka Damu ilikuwa ni unabii wa namna Yesu atakuja kumwaga damu yake kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu miaka maelfu baadae.
3. Mungu hakumuambia nabii Hosea azini bali alimuagiza aende kuoa mwanamke ambaye hatakuwa muaminifu kwake, ili ajifunze nini maana ya kusalitiwa na awafikishie ujumbe waisrael kwa uzito wake ( namna waisrael walikuwa wamemsaliti Mungu wao na kugeukia miungu mingine ni kama mwanamke aliyeolewa kumsaliti mume wake na kuanza kutembea na wanaume wengine).
NB. Mungu si kama mwanadamu bali Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake.
Hisia za binadamu za upendo, hasira, huzuni, huruma zimetokana naye kuwa mfano wa Mungu.
Huyo roho wa mungu anafanyaje makosa ya kiuandishi? Na kwanini mungu awe na hasira ili hali hiyo ni weakness ya mental judgement.
 
Mungu huyo, Aliumbaje binadamu wenye uwezo wa kuleta shida,uovu,ukatili na dhambi kwenye dunia yake?

Mungu huyo, Alishindwaje kuumba binadamu wasioweza kuleta shida, Uovu, ukatili na mabaya kwenye dunia yake?

Mungu huyo anaweza yote kweli?

Mungu huyo kama hapendi dhambi, uovu, ukatili na mabaya viwepo duniani, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na mambo haya?
Hapo tusingekuwa binadamu BALI NI MALAIKA SASA.
 
Kwa mujibu wa Biblia hata shetani alikuwa Malaika na akaweza kufanya uasi na uovu,

Sasa utasemaje kwamba malaika ni wakamilifu hawawezi kufanya uovu?
Shetani hakuwahi kuwa malaika.yeye aliumbwa na moto na malaika waliumbwa kwa nuru.ni vitu viwili tofauti
 
Inaonesha ni kwajinsi gani Ambavyo Elimu na sayansi haijakukomboa kwamambo ya fuatayo
1.kuwepo kwa contradiction Hakumaanishi kwamba Mungu hayuko
2.Msomi unae toa fact Kama Mungu hayupo na hiliali Ata Biblia yenyewe inaonekana hujawai kuisoma una sikia tu historia nta kwambia kwann unaonekana Biblia inaonekana hujawai kuisoma
3.Ww kiranga nawenzako woteee
Inaonekana kunashida kwenye akilizenu
Wote Mnajaribu kuingiza sayansi kwenye maswala ya Imani mna sahau kwamba Imani ni Imani tuuu
Na sayansi ni sayansi tuuuu

Nini maana ya Imani??
Ni kua na HAKIKA ya mambo YATSRAJIWAYO NI BAYANA YA MBAMBO YA SIO ONEKANA

Sasa ww umeambiwa Imani inahusu mambo Ambavyo hayoonekani alaf mtu Ana kwambia anataka proof za kisayansi kwenye maswala ya Imani

Mf.Mm binafsi nishawai kuumwa Sana kichwa lakin nikajiombea Mimi mwenyewe kwa Jina La YESU nikapona kwamda mfupi tuuu

Haya Sasa niambie ni prove kwamba ni Mungu kaniponya Kama sayansi inavyotaka (sayansi ina taka proof za kibinadamu)
Tunaweza hata tukatumia miaka 100 na usielewe ilikuaje kuaje nikapona

Kwaufupi Jueni kutifautisha kwamba
Sayansi inahitaji PROOF
ILA
DINI inahitaji IMANI
4.Acheni uvivu wa fikra kupenda kutafuniwa vya Google na watu wengine(nakuona kilakitu unamtaja kiranga wakati kiranga ni mtu Kama ww yemwenyewe biblia hajawai kuhisoma na Kama anasoma Ana soma Kama Phyisics )

Mngekua mnasoma Biblia msingekua mna muulizia Mungu Jamii forum Eti mtu akuthibitishie Mungu yupo alaf Unakesha ukifanya mambo yako mengine

Mungu alisema kwamba

Mtafuteni Mungu maadam anapatikana

Mungu anatafutwa nakatoa ahadi ya kupatikana Kama mtu ata mtafuta kwa uaminifu

Msichojua nyie nikwamba Wapo watu wengi ambao wanasikia sauti ya Mungu Wanaona Maonoo wakiwa wamefumba machoo kwasababu hao watu Wana mtafuta Mungu kwa kufunga,kuomba na Kijitakasa dhambi zao

Ata Wana wa Israel walipo sema kwamba kwann Mungu aongee na Musa tuu. Walitaka kumuona waka ambiwa wajitakasee Kwanza ndo Mungu ashuke aongee nao

SASA NYIE ENDELEENI HIVYO HIVYO HATA KANISANI HAMTAKI KWENDA ALAF MNATAKA KUMUONA MUNGU GOOGLE NA JAMII FORUMS

5.BIBLIA IMEANDIKWA KWA KISWAHILI LAKINI JUA KUTOFAUTISHA KUSOMA BIBLIA NA VITABU VINGINE KAMA PHYSICS N.K

Biblia ni kitabu kinacho changanya Sana Kama utatumia akili zako binafsi ,Bila ya ROHO MTAKATIFU
Uwezi kuelewa sawa sawa Biblia

Mtataka tena tusibitishe ROHO MTAKATIFU YUPO EHH( Kama vile anaonekana )
Sasa nyie endeleeni ku Google tu na kusikiliza wazungu alaf tuuone Kama mtamuona

Mf.kwanin Biblia sio Kama VITABU VINGINE

Yesu mara ya Kwanza alikua na wanafunzi zaidi ya 70+ LAKINI sikumoja aliwaambia ya kwamba
"Mtu atakaye nifuata awe tayari kuula Mwiliwangu na Damu yangu"
Wengi wawana funzi wake hawakuelewa Yesu kamaanisha Nini wakaondoka wengi wakabaki wachache tuu ikiwemo wale 12

LAKINI katika historia ya YESU hatuajaona sehemu ambayo wanafunzi walio bakia walikula mwili wa Yesu

Biblia IMEANDIKWA kwa mafumbo ambayo kwaakili ya kawaida Bila ROHO MTAKATIFU haiwezekani kuifumbua

In short
ACHENI KUSOMA BIBLIA KAMA MLIVYOSOMA PHYISICS NA MATHEMATICS

6..UJUI BIBLIA KWASABAU
Unashanga sifa ya Mungu ya KUSAHU
Kama ungekua msomaji wa Biblia usinge shangaa Mungu maranyingi alikua anawaambia Wana wa Israel kwamba ATA YASAHAU MAKOSA YAO
Ata MAKOSA yako ukiyatubu Leo Mungu ata yasahau

HASIRA
Mungu anazaidi ya HASIRA tena Ni MOTO ULAO
Mungu HASIRA anayo Kama nako huamini kawaulize Sodoma na Gomora wata kudada vulia Haswa

WIVU
Kama ungekua onasoma Biblia usinge shangaa WIVU wa Mungu

Maana yeye ni Mungu mwenye WIVU


Mwambie na Kiranga Jueni kutifautisha kati ya Imani na Sayansi

(+)kanisani unaitwa Msalaba

(+) Shule inaitwa jumlisha

NB.Huu usiwe ugomvi Tuna eleweshana tuu

Nakama kunasehemu nimekosea kuandika Bahati mbaya
msije mkaleta visingizio

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Pamoja na hayo uliyosema, sasa kwanini kitabu kinachomwelezea mungu mwenyewe na ambacho kakiandika yeye mwenyewe kupitia watu kinajikontradict?kwanini aruhusu jambo hilo? Vilevile huyo mungu akili na uwezo wake havichunguziki kwa ukubwa wake, sasa kwanini awe na wivu na hasira vitu vinavyoashiria imperfection?
 
Kwanini wafanye uovu na kwanini kuna uovu? Ilishindikanaje mungu kuumba watu wasiofanya uovu?
Kwahiyo mkuu ulitaka uumbwe kama Malaika maana Malaika ndio hawafanyi uovu

Binadamu amewwkewa njia mbili njia ya mema na njia ya uovu na amepewa nafsi na akili ya kuchagua atakacho

Na amewwkewa moto na pepo pia amepewa nafsi na akili Ili achague anakotaka kuenda
 
First things first.

Mimi sijadili imani, najadili ukweli.

Imani una haki ya kuwa nayo yoyote. Ya ukweli au ya uongo.

Hii ni haki yako ya kikatiba, ni haki ya utu wako ipo katuka Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Na nimesema mara nyingi hapa, mimi siamini uwepo wa Mungu wala dini, lakini natetea haki za watu wote kuamini wanavyotaka, na haki zao za kuamini wanavyotaka zikiingiliwa, nitazitetea.

Kwanza kabisa naomba tuelewane hapo kwamba kuna tofauti kati ya kujadili imani na kutafuta ukweli.

Imani ni haki ya kikatiba ya kila mtu, haina haja ya kuithibitisha, ukweli ndio unathibitishwa.

Ninapohoji uwepo wa Mungu, siongelei suala la imani, naongelea suala la kutafuta ukweli.

Umeelewa hapo?
Napinga uwepo wa imani na dini cause zinatuletea majanga na uharibifu mwingi, mfano vita vya kidini, degrade human thinking capacity. In short mambo ya imani na dini should perish from this world.
 
Msio amini uwepo wa Mungu mnajichagulia njia ya "KIPUMBAVU SANA" ... Haya fanya Mungu hayuko, inakuongezea nini au kukupunguzia nini zaidi ya KUJIFANYA MJUAJI SANA ( unasoma biblia ili utafute makosa)
Naita njia ya kipumbavu kwa sababu moja tuu . Ikitokea mimi ninae Muamini Mungu nikifa nikienda niendako nikikuta uwepo wake ni poa tuu . Na nikienda nikakuta hamna uwepo wake ni poa tuu SIKOSI CHOCHOTE .. ila wewe umejichagulia chaguo moja tuu lisilo na ulazima kulichagua zaidi ya kujifanya mjuaji ...haya umekufa ukae kumkuta UTAJITETEA AJE [emoji1787][emoji1787][emoji1787] jibu utakua nalo wewe .

ILA YOTE KWA YOTE NYIE MSIO MUAMINI MUNGU, MUNGU NDIE ANAE WAPENDA ZAIDI ...
Mkuu,
Jadili hoja acha kelele Kama chizi aliyeona jalala jipya!
Karibu tujadili kwa staha.
 
Shetani hakuwahi kuwa malaika.yeye aliumbwa na moto
Kwa hiyo Mungu aliumba shetani?

Unaona sasa Mungu huyo alivyo mkatili? 😆

Yani Mungu anaumba Shetani wa kuleta uovu duniani halafu anataka tutende mema..!!

Niki kwambia kwamba, Maandiko ya kidini ni Hadithi za kutungwa ndio kama hivi sasa.

na malaika waliumbwa kwa nuru.ni vitu viwili tofauti
 
Dooh..kwakwel mimi namuamin Mungu na mkristo japo wa maghumashi. Ila kuna time huwa napata was was sana na vitu kwel huwa vinanipa was was sana kama Yupo maana dah!! Lakin kuna time pia kuna mambo yanayonifanya nirud kwenye msatari kujilazimisha kuamini neno la Mungu maana mambo mengine yameshanitokea na kama hayangekua maombi ya viongozi wa dini na walokole najua kabisa nisingetoboa.

Mfano hiv karibun mwanangu almanusura apate mental breakdown akawa kama anaongea vitu vya ajabu ghafla na nimehangaika nae mahospitalin hakupata nafuu mpaka tulipo amua kufuata MAOMBI na now he ia very more than fine. Ofcz alishapone and is back to school.

SASA HAPO MKUU NDIO HUWAGA NASEMA MUNGU YUPO
Kuwa na mental disorder na kutibiwa kisaikolojia haithibitishi mungu yupo.
 
Unakubaliana nami mungu Perfect hayupo?
Siwezi kubaliana na wewe, hiyo Ni imani yako, na nami nina imani yangu, na imani yangu inanihakikishia kuwa Mungu yupo na nimeona akinitendea mambo mengi hivyo Nina ujasiri wa kusema Mungu yupo, sijui kuhusu imani yako
 
Siwezi kubaliana na wewe, hiyo Ni imani yako, na nami nina imani yangu, na imani yangu inanihakikishia kuwa Mungu yupo na nimeona akinitendea mambo mengi hivyo Nina ujasiri wa kusema Mungu yupo, sijui kuhusu imani yako
Hujajibu swali mpaka sasa,
Unakubaliana nami mungu perfect hayupo?
 
Napinga uwepo wa imani na dini cause zinatuletea majanga na uharibifu mwingi, mfano vita vya kidini, degrade human thinking capacity. In short mambo ya imani na dini should perish from this world.
Hapo sasa kuna nuance kubwa kati ya kupinga uwepo wa dini/imani na kusema dini/imani zinapotosha ukweli.

Ukisema unapinga uwepo wa dini na imani, ni kama unataka kupiga marufuku imani/dini.

Dini ukiipiga marufuku, ndiyo unaipaisha umuhimu wake. Watu watakuita mpinga dini uliyetabiriwa, watasema huo ni utabiri unatimia. Matokeo yake utazidisha wafuasi wa hiyo dini.

Dini inapingwa kwa kuonesha isivyo kwenye ukweli, kuachiwa iwe huru, lakini kuelimisha watu kuhusu ukweli. Elimu ndiyo itawaongoza watu kujua mapungufu ya dini.

Kimsingi, uhuru wa kuabudu kwa dini/imani yoyote ni upande mmoja wa shilingi ambayo kwa upande mwingine ina uhuru wa kutoamini. Hata kwenye katiba nyingi na Universal Declaration if Human Rights, uhuru wa kuabudu unajumuishwa na uhuru wa kutoabudu.

Kwa hivyo, ukiruhusu dini zipigwe marufuku, kwa sababu zinalemaza uwezo wa watu kufikiri, kimsingi utakuwa pia umefungua mlango wa watu wasioamini kulazimishwa waamini, uhuru wa kuamini na kutoamini ni uhuru mmoja huo huo, kifalsafa, huwezi ku promote kuzipiga marufuku dini bila ya wewe usiyeamini kuhatarisha uhuru wako wa kutoamini dini.

Kwa falsafa hii, mimi napenda sana watu wawe na uhuru wa kuamini mpaka wao wenyewe wagundue kuwa imani hizi ni kamba tu. Na hata wasipogundua, ni sawa tu, ni haki zao za kikatiba na za kibinadamu.

Sitaki kumuondoa mtu kwenye imani yake kwa lazima, kwa sababu tu mimi nafikiri dini zinalemaza watu, au hata kama kweli dini zinalemaza watu, wakiamua kulemaa, ni haki yao.

After all, watu wana haki ya kuchagua maisha ya kulemaa akili, kama hicho ndicho kitu muhimu kwao.

Unajua kuwa kuna watu wanapenda uongo mtamu, kuliko ukweli mchungu.

Sasa, watu kama hao, wakichagua kuamini uongo mtamu wa dini, wewe ukawalazimisha waondoke kwenye uongo mtamu ukawapa ukweli mchungu kinyume na wanavyotaka wao, utakuwa umewakosea, umewaingikia kwenye uhuru wao.
 
Wewe nani aliyekuambia bibilia ni kitabu kisicho na Makosa?

Wakati nabii wa Mungu Yeremia anasema Bibilia imechakachuliwa

Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
Kama imechakachuliwa, huyo roho mtakatifu tunaeambiwa ndo alikuwa anawaongoza waandishi alikuwa anafanya kazi gani?
 
Nikusibitishie Mungu kama yupoo

Haya Niki kwambia kwamba nimeugua nikapona kwakujiombea nikapona utasema ni psychological relief
Je..kwamtu ambaye yupo kwenye coma state ambaye kaombewa kapona naye utasema ana psychological relief?

Kumbuka Mungu hamna mwanadamu katika hali ya ubinadamu anaye weza kumuonaaa

Alaf pia Unatakiwa kujua kutifautisha kiswahili Cha Biblia na kiswahili Cha kibantuu



PILI

Sijakubali kwamba Biblia ina Contradiction kama ulivyo sema
Kusoma kwenu Biblia mkizitegemea akilizenu wenyewe ndo kuna sababisha kuona kwamba Kuna Contradiction

Tena nyie sio watu wa Kwanza kuona kwamba Biblia ina Contradiction nimesha kutolea mfano wa Yesu
Kilichotokea na wanafunzi wake

TATU
IMANI nimekuandikia ni kua na Hakika.....ni bayana ya mambo yasio onekana

Cja kuelewa una niambia msingi wa Imani ni kutokua na uhakika

Ukitaka dfn soma waebrania 12:1

NNE

Imani na Sayansi nimesha kuandikia ni vitu viwilitofauti

Mtu anaye ingiza DINI kwenye Sayansi hasa matibabu ataishia vibaya

Na hivyo hivyo mtu anaye changanya sayansi ya evidence na DINI hawezi kuelewa chochote

Jua kutifautisha kati ya DINI na Imani
Maana nakuona Bado unachanganya sayansi na IMANI

TANO
Kuponywa na Mungu Kuna depends na many factors kama sio mtu wa DINI huwezi kuelewa utaishia kubisha vitu usivyo jua tuuuu

Namaswali kama haya yanasibitisha ni kiasigani Biblia hujui kabisaaa

Miongoni mwa factors ni kiwango chaimani ya mtuuu binafsi

Kw mfano mtu Kama ww ukiombewa huwezi kuponaa ng'oooo

SITA

Ett una ulizaa

Mungu anatafutwa kwani hanekani?

Nimecheka sannaaa Yann ina onesha jinsi gani Biblia huijuiiii....
Unajua kumtafuta Mungu kwa Tochiii Auuu[emoji1][emoji1]

We bado sanaaa kwenye bible hujui ata jinsi ya kumtafuta Mungu alaf una sema Mungu. Hayupo

Yan mfano mtu hajui kufanya swali la Logarithms yupo darasa la saba alaf anakwambi swali Hilo halifanyikii
Mtakesha apooo

Sina maana kwamba weee ni darasa la saba mfanoo tuuuu rafiki

Mfano mwengine

Waislam Wana sema ss tuna kufuru tunaposema yesu ni mwana wa Mungu
Wana dai Mungu hazai

Wakati ss tunaposema mwana wa Mungu hatuu maanishi Mungu anapata Mimba na ana zaa

##SHIDA KUBWA WEWE HUJUI KUTOFAUTISHA MISAMIATI YA KIBIBLIA NA KUIWEKA KATIKA MAAANA ##

Anaposema kutafuta katika bible hamaanishi mtu kapoteaaa

Jua Kwanza MISAMIATI ya KIBIBLIA vizur friend

Jiulize kwann Kuna makanisa mengi kwasababu watu wenginhawajui kuisoma Biblia....


Me sio mtumiaji mzoefu Sana ndomana nimeshindwa kuweka picha zaaswali.yako
Natumaini umeelewa It

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Adam ,Musa, ibrahimu, yakobo, walimwona mungu unasemaje mungu haonekani kwa macho ya mwili? Contradiction zipo nyingi tu ila we ndo huzioni maana unasoma biblia kishabiki.
 
Back
Top Bottom