JuIzi kati mwaka mpya nimeenda Arusha, nimechukua room pahala, bei ilikuwa 45,,, ni hotel ya kawaida tu sema wana bei sana sijui shida nini au ndo mji wa kitalii ! Kufika room mwenzangu akaenda kujimwagia, yeye ndo mwenyeji wangu kwa hio hali ya hewa ameizoea,,, Nikaingia mimi kuoga, dah kumbe maji ya moto hayatoki , nadhan mfumo ulikuwa mmbovu, reception wakati nasainishwa hiki kipengele niliuliza, ! Nikaenda kumvaa yule dada mbona maji moto hamna na mmetaka hela nyingi ? Ooh saamahani sijui bla bla kibao, nikamwambia nibadilishe room akagoma, basi rudisha hela kiasi napo akagoma, nikawa mkali hadi akamuita mlinzi ! wapuuzi wale, wakanirudishia 15 !