Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mkuu@LwandaMagere hili jina lina kisa chake ujue, nakumbuka kipindi nasoma kenya primary tulipewa hadithi za lwandamagere jinsi alivyokuwa mbabe na mpiganaji hatari wa kabila lake la wajaluo. Kilichomuondoa ni mwanamke aliyemuoa ambaye alitaka kujua siri ya nguvu zake ndipo lwanda akamwambia ukichoma kivuli changu nami ntapoteza nguvu zangu.
 
MKASA WA PILI -Sehemu ya 45.


Inaendelea.............



Sasa kuna wikiendi moja nikiwa nimepumzika nyumbani,yule jamaa aliyenipeleka Kasulu alinipigia simu akaniambia yupo njiani anakuja Mwanza,akasema atakapofika inabidi tuonane!,nilimwambia mimi nitakuwepo tu nyumbani kwangu akifika aniambie nikamchukue!.Basi baada ya masaa kadhaa jamaa alifika,nilimtuma dereva wangu aende akamchukue kule stendi.Jamaa alipofika hapo nyumbani alianza kushangaa sana namna nilivyokuwa nimepiga hatua ya kimaisha tofauti na mwanzo tulivyoachana!.

Jamaa aliniambia "Aisee kaka unatisha mzee,kaka hii yote ni mali yako?".

Jamaa aliendelea kuuliza huku akishangaa maisha yale ya kifahari niliyokuwa nikiishi.Sasa kwakuwa sikutaka kabisa mke wangu aelewe mambo yaliyokuwa yakiendelea nilimwmbia jamaa "Usijali kaka ngoja tule halafu tutoke kidogo tukapunge upepo mahali fulani".

Basi baada ya kuwa tumemaliza kula nilimchukua jamaa mpaka maeneo fulani ya Kirumba ambayo mara zote nilipendelea kwenda kupumzika.

Jamaa akaanza kuniambia "Eeh kaka nipe stori ndugu yangu mambo yaliendaje,maana baada ya kukuacha kule mimi nilirudi zangu sikufahamu kilichoendelea".

Nilimwambia "Wewe acha tu kaka mambo si mepesi kama nilivyokuwa nikidhani maana nilipitia mambo mengi sana ila namshukuru Mungu kanisimamia mpaka hatua hii".

Jamaa akaniuliza "Kwani kaka ulifanyaje mpaka kufikia hapa,tafadhali nieleze ili na mimi niangalie cha kufanya kaka".

Nilimwambia "Kaka uliponiacha Mnyegera yule mama aliniagiza kwenda Kongo na huko ndiko nilipopata dawa ya biashara na hatimaye namshukuru Mungu imenipa matokeo".

Nilimwambia huku nikifahamu kabisa ninamdanganya ila sikuwa na namna,sikutaka kabisa aelewe kilichokuwa kinanipatia pesa wakati huo.

Jamaa aliendelea kuniuliza "Kwahiyo kaka ulianzisha biashara?".

Nilimjibu "Ndiyo kaka nilianzisha biashara".

Jamaa aliniuliza "Lakini mbona imeenda fasta sana"?.

Jamaa alikuwa akiuliza maswali kana kwamba ana mashaka na wasiwasi kuhusu utajiri wangu,nilijua lazima awe na mashaka maana ule utajiri uliinuka ghafla sana.

Nilimwambia "Ndiyo ile dawa kaka imefanya haya maajabu".

Jamaa aliendelea kusema "yaani kaka ningejua na mimi tungeenda wote,mimi nilienda tu kuchukua dawa ya kinga hatimaye hata kazi yenyewe sikuendelea nayo".

Baada ya maongezi ya muda mrefu nilimwambia nitampatia pesa afanye mtaji ili aisaidie familia yake,wakati huo zile nilikuwa nikizitumia pia hata kwenye biashara,hii ni baada ya Malikia kuniambia nizifanyie maendeleo sikuwa na mashaka tena maana nilijua hata kama ingeharibika huko mbeleni mimi nisingehusika kwa wakati huo!.

Ilibidi nimuulize "kwahiyo unadhani nikikupa kiasi gani kitatosha wewe kuanzisha biashara?.

Jamaa aliniambia "Kaka kuna biashara za vipodozi nizifanye,nataka nifungue duka pale kakola maana kuna uhitaji mkubwa sana".

Nilimuuliza "Kwahiyo unadhani kiasi gani kitatosha?".

Aliendelea kuniambia "Yaani kaka mimi nikipata milioni 10 tu itanitosha,hata kama ni mahakamani tukahandikishane nitakurudishia,maana hesabu nilizo piga mpaka kufungua duka niwe nafata mzigo Uganda itanigharimu kama milioni 8,hivyo ndiyo maana nasema ningepata milioni 10 ingenisaidia sana".

Kwakuwa jamaa alinisaidia sana kunitoa Mwanza mpaka Kasulu niliona jamaa alinisaidia sana mpaka mimi kuheshimika kwa wakati huo hivyo nilimwambia kwamba nitampatia hizo pesa na sitaki anirudishie,nilitaka yeye aende akapambane na maisha ili atimize ndoto zake.Wakati huo suala la pesa lilikuwa haliniumizi akili kabisa maana kila mwezi ulikuwa unaingia mzigo wa kutosha.Basi baada ya kumpatia ile hela aliyohitaji,jamaa hakutaka kupoteza muda,alinambia inapaswa akapambane na angenijulisha kila lililoendelea kwa wakati huo,nilimwambia kama angehitaji msaada wa kifedha basi asisite kuniambia ningemsaidia!.

Sasa nakumbuka siku moja nikiwa nimelala chumbani kwangu,mke wangu alikuwa ameenda kazini,kama kawaida nilipata ndoto ambayo ilikuwa ni ileile niliyoiota siku kadhaa zilizokuwa zimepita,ile ndoto ilinitaka nielekee eneo moja ambalo nilikuwa silifahamu ili nikatoe kafara,nililiona lilelile lori la mafuta na ile costa,sasa kwakuwa ilikuwa mwisho wa mwezi sikutaka kabisa kuipuuza ile ndoto maana nisingejiongeza ilikuwa inakula kwangu.Niliamka kitandani ikabidi nielekee kule kwenye kile chumba cha siri kujiandaa kuelekea hilo eneo nililokuwa nimeonyeshwa ndotoni,niliingia ndani ya kile chumba cha siri nikachukua zana zangu za kazi,nilihakikisha pia ile pembe siku hiyo siiachi kwasababu sehemu niliyokuwa naelekea nilikuwa siifahamu vizuri,hivyo niliona ingenisaidia katika mapambano hata kama ningekuta kuna vizuizi vya kishirikina.Kabla ya kuondoka nilijaribu kuyatazama yale magari yote mawili kishirikina,yaani ile Costa pamoja na lile lori lililokuwa limebeba mafuta,lengo langu ilikuwa ni kuangalia uwezo waliyokuwa nao abiria wa magari yote mawili,nilipotazama kwa makini nikaona wote waliyokuwa kwenye hayo magari mawili walikuwa weupe na wepesi kama karatasi,hakukuwa na mtu mwenye uwezo ndani ya hayo magari ambaye angenizuia nisitoe kafara,ndipo niliushika mkono wangu wa kushoto uliyokuwa na irizi na kutamka kama kawaida ya kwamba inapaswa muda huo niwe katika hilo eneo lililokusudiwa.

Kufumba na kufumbua nilijikuta nipo kando kando ya barabara katika hilo eneo,sasa kumbe hilo eneo ilikuwa ni kijiji kimoja kinaitwa Mulowo,na barabara niliyosimama kando ilikuwa ni barabara kuu ya kutoka Mbeya kueleka Tunduma,sasa ilibidi niyatazame yale magari kishirikina ili kuona yalikuwa umbali gani,baada ya kuyatazama na kuona kwamba hayakuwa mbali sana ilibidi nisogee pembeni kuyasubiri, baada ya muda wa nusu saa kwa mbali nililiona lile lori nililoliona ndotoni likiwa linakuja kutoka Mbeya kuelekea Tunduma na ile Costa pia ilikuwa inakuja kutoka Tunduma kuelekea Mbeya,basi nilisogea kuelekea katikati ya barabara kuanza kuweka dawa za tego,safari hii nilitaka asibaki mtu hata mmoja kwenye ile kafara hata kama kungekuwa na mende au nzi kwenye hayo magari nilitaka wateketee kabisa!.

Sasa wakati nimemaliza kuweka ile dawa ya tego pale katikati ya barabara,mara ghafla niliona upepo mkali sana kama kimbunga,ule upepo ulinisomba mpaka kwenye shamba moja ambalo halikuwa mbali sana na ilipokuwa barabara,ile kutazama vizuri nikawaona wanawake wawili wakiwa uchi kama walivyozaliwa,mmoja alikuwa akining'inia angani na mwingine alikuwa amesimama kando ya barabara huku akiniangalia kwa hasira!.

Yule aliyekuwa akining'inia angani akaniuliza "Wewe umekuja kufanya nini hapa,uelewi kwamba hii si himaya yako?".

Nilinyanyuka pale chini kujaribu kuwasogelea ili nilianzishe vurumai lakini sikuweza kupiga hatua hata moja.

Yule mwenzie akaniambia "Aliyekutuma leo kakudanganya,leo tunaanza na wewe ili tukakukaange tukule nyama".

Kiukweli nilisposikia ile kauli ya kuliwa nyama,jasho likaanza kunitoka japo hakukuwa na jua!.Sasa kwa wakati huo yale magari niliyokusudia kuyatoa kafara yalikuwa yameshapita eneo la tukio nilipokuwa nimeweka lile tego,nilitambua wale wachawi walikuwa wametegua lile tego ili nisipate kitu,kiukweli wale wachawi walinizidishia hasira kiasi kwamba macho yalibadilika,nilikasirika mpaka macho yakawa mekundu kama damu,kitu kilichofanya nikasirike ni kile kitendo cha kuondoa lile tego ambalo tayari lilinikosesha damu ya kafara kwenye zile gari ukizingatia ilikuwa tarehe ya mwisho ya kutoa kafara,pia niliwaza kama ningekosa ile kafara ni nini kingenikuta maana Malikia asingenielewa kwasababu uwezo wote alikuwa amenipatia,pia alishanionya kwamba nisije rudia tena kosa nililokuwa nimelifanya kule bungu,mkoani Pwani.Nilitambua kabisa lazima ningepata adhabu maana yale magari tayari yalikuwa yameshapita lile eneo la tukio bila kupata madhara yoyote,na chanzo cha hayo yote walikuwa hao wachawi wawili.

Basi niliukamata mkono wangu uliyokuwa na irizi nikauamrisha ya kwamba nataka nipige hatua kutoka nilipokuwa nimetupwa na kile kimbunga ili niweze kusogea barabarani.Pale pale nilianza kusonga barabarani,wale wachawi baada ya kuona naelekea barabarani walianza vituko tena,walianza kutimua vumbi lile eneo kiasi kwamba kukawa kama uwanja wa vita,Kiukweli nilikuwa nimejaa sana hasira,sasa kwakuwa waliweza kutegua lile tego wakanidharau wakaona sikuwa na uwezo wa kuwafanya chochote!.Nilipoona vumbi limezidi nilichukua ile pembe nikainyoosha kwenye lile vumbi hatimaye likakoma.


Itaendelea..................
 
Aiseee[emoji134][emoji134]
Kweli ulizunguka sehemu nyingi..hadi Mlowo toka Mwanza[emoji119][emoji119][emoji119]


Hiyo pembe haikuweza kukuonyesha hali ya anga unayoenda ikoje?
 
Mkuuuu Mimi nataka kujua KWA mwezi ukiingia kwenye begi unakuta kama kiasi gani cha pesaaaa
 
Mkuu umesahau waganga walivyo na mbwembwe?
 
Vyuma vimeuma .!
 
Hapa lazima patakuwa Iwambi kama unaenda Mbalizi au Senjele kutoka Tunduma kuja Mbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…