Mkuu Mimi naona unajikanganya tu bado, na bado hujanijibu maswali yangu tafakuri, kua ni KIPI HASWA kimekufanya ulete hii stori hapa, suala la kudhibitisha najua huwezi kudhibitisha hayo mambo ambayo unaaminisha umma kua yapo upande wa pili, wewe kama ulikua CHUMBA A na ukahamia CHUMBA B, kuna ulazima gani wa wewe kuongelea yaliyokua yanafanywa CHUMBA A pasipo na UDHIBITISHO uliotukuka na zaidi ambayo unayasema yanaleta taswira mbaya kwa WAAMINIO wa CHUMBA A uliowaacha, narudia kuasema nilichokiandika hapa hakikunyimi wewe kuendelea na HADITHI yako lakini nimekuta jambo ambalo imenipasa kulitolea maelezo huu UNAFIKI na UONGO.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Nimekufuatilia saana mkuuu na nimekuelewa
Tatizo lililopo hujaelewa alikuwa upande gani?
Yeye alikuwa upande wawachawi (WACHAWI)
HUKO AMETOKA KATAFUTA UPANDE ANAOHISI NI SEHEMU SAHIHI.
Sidhani kama alikuwa huko unakokusema. Lakini kama unautetea upande huo aliotoka wawachawi uko sahihi, kama sivyo kuna pahala hujamuelewa.
Mleta mada wetu na wewe unataka kukosea sehemu moja tuu.
kuwanyima watu uhuru wa kubisha na kutafakari.
Unapotoa ushuhuda huu mzito amini kabisaa wewe ni kama babu anaesimulia wajukuu kwa kuwa yeye kaona mengi hivyo maswali na mitizamo yao haviepukiki. Kuna watakao kubali kuna watakao kataa
Amini usiamini mleta maada huu ni ushuhuda mkubwa kuwahi kutokea kwenye uso wa dunia hii ya mchana
Wewe unaweza ona ni kitu cha kawaida lakini sio hivyo.
Huenda hata huu ushuhuda wewe unauchukulia kiwepesi lakini amini ni mzito mnoo kubebeka ndio maana watu wameamua kuufanya burudani lakini undani wake ni mzito mnoo kwa watu wetu hawa kuwez kuubeba ki uhalisia
Tambua unafanya kitu kikubwa mnoo lakini usikoseee kujiruhusu kulazimisha kiwe chepesi kuaminika
Huenda ikachukua hata miaka 1000 watakaokuja humu jf na kupitia vitabu vyako naamini na penyewe hawataamini
Itawalazimisha kufanya tafiti ili kujiridhisha kama hichi kiumbe kinachoitwa wewe kilikuwepo.
Kwa wakristo huenda huu ushuhuda ukaja kutumika hata huko mbinguni kama nukuu ya kuwahukumu wakristo walioshupaza mashingo yao
Haya maswali anayouliza huyu ndugu ambao mnaona kama anakashifu, muamini ni maswali yanayoishi na sio ya kizazi hiki ni ya kizazi ambacho hakitabahatika kukushuhudia, hivyo unapomjibu yeye fanya kama miaka mingi saana akija mtu kujiuliza hili swali kama ungekuwepo ungemjibu vipi?
Akija mtu akitoa mitizamo kama ya huyu kama ungebahatika kuwepo ungemjibu vipi?
Na haya yooote anayoyafanya huyu ndugu endapo ukafanikiwa kufika mbinguni kama ilivyomatarijio yako ukapata nafasi ukiwa huko kumuona mja wa mwenyezi Mungu akijiuliza haya anayojiuliza huyu nadhani utakuwa unatamani asogee mbele alikute hili swali na hizi hoja ulizomjibu huyu hapo ndipo utasikia malaika wanakuimbia nyimbo na kushangilia huku wakimtukuza bwana kwa kuwahi kuweka kiumbe kama wewe
Tambua Mungu kakupitisha huko si kwa mipango yako ni kwa matumizi yake ili Nuru ing'ae gizani. Na hili ni deni jitahidi umtumikie Mnyazi Mungu kupitia hili alilokutendea kama mja wake
Usikosee kugeuza ushuhuda huu kuwa ni mali yako usikosee kabisaaa wewe ni chombo ulietumika kuandalia ushuhuda huu.
Whyme na wengine tafadhari embu chambueni hili kwa manufaa ya kizazi cha mbele pia msimnyime haki zake za kuwa binadamu na anamapungufu yake.
Ushuhuda huu si kwa ajiri ya dini moja zote zinahusika
Dini gani inapenda haya? Hakuna.
Ushauri
Pesa utakayoipata kupitia ushuhuda huu wa Mnyazi Mungu mrudishie mwenyewe kwa kugharamia ueneaji wa huu ushuhuda vinginevyo utataka kumkufuru