Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Acha kuleta nuksi mkuu siyo maneno mazuri yakuongea hayo unaweza kuchukuliwa hatua Kali na jamuhuri ili fundisho kwa watu wengine

Hahaha, we jamaa una hasira kama vile story umeilipia.

Bahati mbaya leo episodes hakuna, LwandaMagere anajiandaa kuangalia team yake inavyochapwa na Man City. Na akishafungwa itabidi mpaka maumivu yapoe ndo aje tena.
 
Hauko serius wewe!!! Juhudi zako pekee zitakupandisha cheo kazini. Mungu pekee ndo anaweza kukukinga na watu wabaya na wala sio nguvu za Giza. Embu kasome tena ulichoandika mzee.

Mimi ni wale vijana ambao umri wetu ni 30+ hivyo ninaelewa vizuri sana ninachokiandika alafu mkuu naomba ukae ukijua kwamba hizi ni imani na imani ni jambo pana sana na ndio maana mtoa mada kama ulimfatilia neno kwa neno amerudia rudia kwa kusema hii dunia ni pana sana kuna mengi ambayo hatuyajui na inawezekana mpk tunaingia kaburini tusiyajue sasa wewe endelea kuamini hicho unachokiamini(kwa imani yako)na mimi nitasimama kwa ninachokiamini kwa imani yangu huko kwa yesu tutakutana baadae.
 
Alooooooooooooo
 
Kuna mtu bado namtafuta

Akisema hivi hazipiti dakika 15
 
Mkuu sema tu kuwa unataka namba ya yule bibi Kasulu usiongee sana

ukimfata jamaa pm kwa kutaka msaada wa mawasiliano ya yule mama ili tupate kinga bado kuna ubaya mpaka tuogopane kiasi hicho?
Ina maana humuamini Mungu mpaka utake kinga ya shetani? 😁😁 Hufiki mbali asee afu pia hutaweza masharti.
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 19.


Inaendelea.............



Baada ya kuwa nimepata zile pesa niliona kwanza nianze ukarabati wa nyumba yetu hiyo ya Nyegezi.Mama yangu alikuwa na wasiwasi kuhusu zile pesa ya kwamba nilikuwa nimezipata wapi!,nilimwambia mama kuna mahali nilikuwa nimepata kazi ya kufundisha,hivyo nilikuwa ninalipwa vizuri,kauli ile ilimtoa mama yangu wasiwasi.

Ile nyumba nilianza kuikarabati upya na kuanzia hapo kila nilipokuwa nikipata pesa kutokana na ajali zile nilizokuwa nikisababisha hapo mjini Mwanza na miji mingine,niliendelea kuisuka upya nyumba yetu ikawa ya kisasa kabisa kama nyumba za matajiri wengine.Ulikuwa ukifika hapo nyumbani huwezi kuamini kama ile nyumba walikuwa wakikaa watu wa kawaida,maana ilibadilika sana ikawa kama nyumba za vigogo wa kiserikali.Nyumbani hawakutia shaka sana maana nilifanya usiri mkubwa sana,hivyo isingekuwa rahisi kufahamu chochote.Siku zilikuwa zikienda mbio na mimi pia niliendelea kutoa kafara!,Kuna siku niliushika mkono wangu uliyokuwa na irizi nikaanza kuongea "Mbona kafara natoa lakini bado napata pesa kidogo?".

Nilisikia sauti ikinijibu kwamba "muda wa kuwa tajiri haujawadia ila uko karibu!".

Kafara na matendo mabaya hayo nilianza kuyafanya mwaka wa 2013.Basi siku moja mwisho wa mwezi nikiwa geto kwangu nilisikia sauti ikiniambia nielekee mkoani Singida eneo la Sekenke ambako ilipaswa kuna watu wafe ili niweze kupata mali nyingi!.Asubuhi ya siku hiyo sikutaka kabisa kupoteza muda,Kuna dawa nilizichanganya hapo ndani kwangu na nilipomaliza nilitamka ya kwamba "Nahitaji kufika sekenke Singida muda huu".

Ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua nikajikuta nipo eneo la tukio.Nilipofika maeneo hayo ya Sekenke kuna gari ambayo nilielekezwa toka mwanzo,ndani yake kulikuwa kuna abiria ambao walikuwa wakisakwa kwa udi na uvumba kutoka huko majini nilikotoka,hivyo siku hiyo ilikuwa ndiyo mwisho wao!.Basi kuna dawa niliitupa katikati ya barabara,ile gari ilipofika yale maeneo nilipoweka ile dawa,gurudumu la mbele lilipasuka ndipo ilianza kukosa uelekeo hali iliyofanya kupata ajali mbaya sana!,Kiukweli nilikuwa nina roho ya kikatili sana kwa wakati huo!,nilikuwa sina huruma hata chembe.Baada ya ile gari kuwa imepata ajali,nilisogea na kukuta wale watu niliyokuwa nimewatageti wamebanwa na viti kwa chini,Nilianza kuwachinja kichawi na kuchukua damu zao!,Pia nilichukua damu za abiria wengine waliyokuwa wamekufa kwa wakati huo,nilihakikisha nawakausha kabisa wasiwe na damu hata tone!.Nilipomaliza nilifanya haraka na kuondoka zangu hilo eneo,nilipofika geto kama kawaida kile kibuyu nilikiweka chini ya uvungu,sikutaka kushinda hapo geto,hivyo niliondoka nikaelekea Nyegezi kwa mama kuangalia maendeleo ya nyumba.Nilipojiridhisha ya kwamba mambo ni mazuri nilirudi zangu tena geto.

Safari hii niliporudi geto nilikuta kitandani kwangu kuna begi kubwa yale ya mgongoni ambayo watoto wa shule wanayowekaga madaftari nikakuta limejaa pesa,siku hiyo nilikuwa nina furaha sana maana sikuwahi kukamata pesa nyingi kiasi hicho!.Sasa nikaanza kuzihesabu pale nilipata milioni 35 pesa za kitanzania.Niliondoka hapo geto kwangu kuelekea Igoma,lengo langu ilikuwa ni kutafuta eneo ili nianze ujenzi wa nyumba,Kuna dalali nilimpata maeneo ya huko Igoma akaniambia viwanja vipo lakini kulikuwa kuna nyumba zinauzwa.Aliponiambia nyumba zipo zinauzwa,wazo la kununua uwanja nikalitoa kichwani!,nilimwambia anipeleke kwenye hizo nyumba zinazouzwa ili niangalie ambayo ningeipenda ninunue.

Jamaa alinipeleka kwenye nyumba ya kwanza ambayo ilikuwa ya kawaida!,tuliendelea kutembelea zile nyumba ambazo zilikuwa zikiuzwa huko Igoma,kuna nyumba tulifika kiukweli niliipenda sana,huyo dalali aliniambia nimwachie namba ya simu ili atakapo wasiliana na tajiri wa hiyo nyumba angenijulisha.Basi nilipoachana na yule dalali wazo lingine ambalo nilikuwa nalo ni kutafuta mwanamke wa kuishi naye ambaye niliambiwa atakuwa akibeba ujauzito ili watoto watakao zaliwa,wawe wanatolewa kafara!.Sasa akilini mwangu niliwaza kwamba nataka nimchukue yule shemeji yangu aliyekuwa na dharau na nyodo ili aifanye hiyo kazi.Lengo langu lilikuwa ni kumkomoa tu ili dharau na nyodo alizokuwa nazo zimtoke.Nilitaka kwanza nikiisha inunua hiyo nyumba na kuvuta usafiri ndiyo nifanyie kazi ilo suala!.

Nilirudi geto na kukuta tena pesa zimejaa kwenye lile lile begi ambalo mara ya kwanza nilitoa zile pesa!,japo hazikuwa nyingi kama za mara ya kwanza,safari hii nilipozihesabu ilikuwa milioni 20,hivyo ukijumlisha na zile za mara kwanza ilikuwa jumla milioni 55,Kiukweli nilipagawa sana!.Nakumbuka siku hiyo nilimpigia mama yangu simu nikamwambia "Mama nimekuagizia gari wiki hii itakuwa inaingia".

Mama aliniuliza "Mwanangu pesa unatoa wapi?".

Niliendelea kumdanganya " hapo shuleni ninapofundisha walitupatia fursa ya mkopo ndiyo nami nimechukua mkopo mama".

Ndani ya wiki hiyo nilienda kwenye Yadi ya magari iliyokuwa karibu na kamanga fery(nisingependa kuitaja) nilitoa pesa keshi nikamnunulia mama yangu gari mpya aina ya Murano.Sasa kwakuwa ilipaswa nikaonane na yule dalali wa Igoma nilimpigia simu mama nikamwambia anapelekewa gari yake.Kuna dereva wa pale Yadi nilimpa namba ya mama ili akifika maeneo ya Nyegezi ampigie.Nilipofika Igoma yule dalali alinikutanisha na mmiliki wa ile nyumba nikaongea naye,jamaa akasema nimpematie milioni 60 ili aniuzie ile nyumba,kwa wakati huo nilikuwa nimebaki na milioni 30 maana pesa nyingine nilimnunulia mama gari,siku iliyofuata nilimpelekea hiyo hela nikamwambia pesa nyingine ningempa siku si nyingi!,lile jumba lilikuwa la kisasa halafu zuri,hivyo nikaona lingenifaa kwenye mambo yangu ya kafara.

Nakumbuka mama yangu alifurahi sana baada ya kumnunulia gari maana aliishi maisha kama mtu sasa!.Kwakuwa hakujua kuendesha gari ilibidi nimtafutie dereva ambaye nilikuwa namlipa kila mwezi.

Siku ziliendelea kusonga sana,siku moja nilielekea mkoani Shinyanga kupiga tukio la kafara kama kawaida!.



Itaendelea.................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…