Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Good Lord...!!
Story inazidi kusisimua walaqhi', hiyo habari ya mfupa uliosagwa mpaka moyo umeshtuka jamani kumbe hayo mambo yapo kweli..!?

Halafu boss wetu Lwanda kuna kaneno umekaweka mzee bila hata tafsida, imebidi tuanze kukemea pepo..!!
Kaneno gani bibie
 
Aiseeeh..!!
Kwa wanaoamini katika Mungu wa mbinguni, Muumba mbingu na nchi, kila mtokapo na muingiapo hakikisheni mmejifunika kwa damu ya Yesu, Ombeeni safari zenu, Ombeeni wapendwa wenu hakikisheni mnawaweka chini ya ulinzi wa Mungu siku zote, Maan' this sh** is so real..!
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 19

Inaendelea.............


Baada ya kuwa nimepata zile pesa niliona kwanza nianze ukarabati wa nyumba yetu hiyo ya hapo Nyegezi!
Mama yangu alikuwa na wasiwasi pesa ya ukarabati nimepata wapi!,Nilimwambia mama kuna mahali nimepata kazi ya kufundisha na hivyo ninalipwa vizuri!.
Basi kauli ile ilimtoa mama wasiwasi

Ile nyumba nilianza kuikarabati upya na kuanzia hapo kila nilipokuwa nikipata pesa kutokana na ajali zile nilizokuwa nikisababisha hapo mjini Mwanza na miji kama Geita na Magu,niliendelea kuisuka upya nyumba yetu na ikawa ya kisasa kabisa kama nyumba za matajiri!
Ulikuwa ukifika hapo nyumbani huwezi kuamini maana nyumba ilikuwa kama ya waziri fulani!
Nyumbani hawakutia shaka sana maana uwezo niliokuwa nao wasingeweza kufahamu zaidi!

Miaka nayo ilikuwa ikienda mbio na mimi pia niliendelea kufanya kafara!,Kuna siku nilishika mkono wangu huu uliokuwa na Irizi nikaanza kuongea "Mbona kafara natoa lakini bado napata pesa kidogo?"
Sauti ilinijibu kwamba muda wa kuwa tajiri haujawadia ila uko karibu!

Hiyo ilikuwa mwaka sasa wa 2013

Basi siku moja nikiwa Geto nilisikia sauti ikiniambia nielekee Mkoani Singida maeneo ya Sekenke ambako ilipaswa kuna watu wafe ili niweze kupata mali nyingi!
Asubuhi ya siku hiyo sikutaka kabisa kupoteza muda!,Kuna dawa nilizichanganya hapo ndani kwangu na nikatamka ya kwamba "Nahitaji kufika sekenke Singida"
Ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua!,Mpaka muda huu nilikuwa nishasema liwalo na liwe kama ni maji nishayavulia nguo sharti niyaoge!

Kwakuwa nilikuwa nina kiburi kwa wakati huo nilijiona kama hakuna wa kuniweza hapa duniani!
Nilipofika maeneo hayo ya Sekenke kuna gari ambayo nilielekezwa toka Mwanzo na ndani yake kuna abiria ambao walikuwa wakisakwa kwa udi na uvumba kutoka huko majini nilikotoka hivyo siku hiyo ilikuwa ndo Mwisho wao!

Basi kuna dawa niliitupa kwenye barabara na ile gari ilipofika yale maeneo ilipasuka tairi ya mbele na kukosa uelekeo hali iliyofanya kupiga mzinga wa maana!Kiukweli nilikuwa nina roho ya kikatili sana kwa wakati huo!,Nilikuwa sina huruma kabisa hata chembe!
Niliokuwa nina huruma nao ni ndugu zangu pamoja na mama yangu!
Baada ya ile gari kuwa imepata mzinga nilisogea pale na kukuta wale watu niliokuwa nimetageti wamebanwa na viti kwa chini,Nilifika nikawachinja kichawi na kuchukua damu zao!Pia nilichukua damu za abiria wengine waliokuwa wamekufa kwa wakati huo na nilihakikisha nawakausha kabisa wasiwe na damu hata tone!

Nilipomaliza nilifanya fasta na kuondoka zangu na mara hiyo nikawa pale geto,Nilichukua kile kibuyu kama kawaida nikakiweka uvunguni!
Niliondoka zangu kuelekea kwa Bi mkubwa kuangalia maendeleo ya nyumba!
Nilipojiridhisha ya kwamba mambo ni mazuri nilirudi zangu tena geto!

Safari hii nilikuta kitandani kwangu kuna begi kubwa yale ya mgongoni ambayo watoto wa shule wanayowekaga madaftari nikakuta limejaa pesa!
Siku hiyo nilikuwa nina furaha sana maana sikuwahi kukamata pesa nyingi kiasi hicho!

Sasa nikaanza kuzihesabu pale nilipata kama milioni thelathini na tano pesa za kitanzania (35,000,000/=)
Niliondoka hapo geto kwangu kuelekea Igoma na lengo ilikuwa ni kutafuta eneo nianze ujenzi!
Kuna dalali nilimpata maeneo ya huko Igoma jamaa akaniambia viwanja vipo lakini kuna nyumba zipo zinauzwa!
Alipo niambia nyumba zipo zinauzwa wazo la kununua uwanja nikalitoa kichwani!,Nilimwambia anipeleke kwenye hizo nyumba anazozifahamu zinazouzwa.

Jamaa alipeleka kwenye nyumba ya kwanza ambayo ilikuwa ya kawaida!,Tuliendelea kutembelea zile nyumba ambazo zilikuwa zikiuzwa na kuna nyumba tulifika kiukweli niliipenda sana!
Jamaa aliniambia nimwachie namba ya simu na atakomuniketi na tajiri wa hiyo nyumba halafu atanijulisha!
Basi nilipoachana na yule dalali wazo lingime ambalo nilikuwa nalo ni kutafuta mwanamke wa kuishi naye ambaye niliambiwa atakuwa akibeba ujauzito wale watoto watakuwa wanatolewa kafara!,Yaani yule mwanamke ntakuwa ninaishi naye kwa kazi hiyo tu!
Na yeye hapaswi kuelewa kitu!

Sasa akilini mwangu niliwaza kwamba nataka nimchukue yule shemeji yangu aliyekuwa na nyodo niwe nampiga shipa na yeye awe kama mke wangu kwa kazi hiyo tu!
Kiukweli nilitaka nimkomoe maana alikuwa na nyodo sana!
Ila nilitaka kwanza nikiisha inunua hiyo nyumba na kuvuta usafiri ndo nifanyie kazi ilo suala!
Nilirudi geto na kukuta tena pesa zimejaa kwenye lile lile begi ambalo mara ya kwanza nilitoa zile pesa!,Japo hazikuwa nyingi kama za mara ya kwanza,Safari hii nilipozihesabu ilikuwa kama milioni 20,Hivyo ukijumlisha na zile za mara kwa za ilikuwa kama milioni hamsini na tano(55,000,000/=),Kiukweli nilipagawa sana!

Nakumbuka siku hiyo nilimpigia mama yangu simu nikamwambia "Mama nimekuagizia gari na wiki hii itakuwa inaingia"
Bi mkubwa aliniuliza "Mwanangu pesa unatoa wapi"?,Niliendelea kumdanganya kwamba nimechukua mkopo kwenye kituo nilichokuwa ninafanya kazi kwa wakati huo!
Ndani ya wiki hiyo nilienda kwenye Show room moja iliyoko karibu na kamanga fery(nisingependa kuitaja) nilitoa pesa cash nikamnunulia Bi mkubwa Murano mpya!
Sasa kwakuwa mimi ilipaswa nikaonane na yule dalali wa Igoma nilimpigia simu nikamwambia anapelekea gari yake!

Kuna dereva wa pale show room nilimpa namba ya Bi mkubwa ili akifika maeneo yale amwelekeze!
Nilipofika Igoma yule dalali alinikutaniaha na mmiliki wa ile nyumba na nikaongea nae jamaa akasema nimpe milioni 60,kwa wakati huo nilikuwa nimebaki kama na milioni 30 maana pesa nyingine nilimnunulia Bi mkubwa gari, siku iliyofuata nilimpelekea na nikamwambia pesa nyingine ningempa siku si nyingi!,Lile jumba lilikuwa la kisasa halafu zuri,hivyo nikaona litanifaa kwenye mambo yangu!

Basi niliondoka kuelekea kwa Bi mkubwa na alifurahi sana maana sasa aliishi maisha kam mtu!
Kwakuwa hakujua kuendesha gari ilibidi nimtafutie dereva na nikawa namlipa kila mwezi!

Siku ziliendelea kusonga na siku moja nilielekea mkoani shinyanga kupiga tukio la kafara kama kawaida!



Itaendelea..............
Duh hii ngoma hatari! So kipindi unapiga hayo matukio na kazi za tuition na kule shule ulipokuwa unafundisha ulikuwa unaendelea au we ulikuwa unazunguka kupiga matukio tu!!
Kama ulikuwa unaendelea walimu wenzako hawakuhoji maendeleo yako ya ghafla??
 
Hivi kuna sehemu ulisema ukikosea masharti ukafanya mapenzi hyo ndo inakua adhabu yako kufanya mapenzi mpaka mwisho wa maisha yako??[emoji848][emoji848]

Hao madem ndo umesema wazuriii??

Hahahahaa ww jamaa unatala uende then ukosee mashart ili ufanye nao maisha yote sababu wazuri[emoji1787][emoji1787]
 
Kwa sasa nikiingia jf kitu cha kwanza kufungua huu uzi.Hii ni zaidi ya Elimu na nilichoamini kwamba Mungu ni mwema na anasamehe na kusahau kabisa na maandiko yanasema dhambi zako ata ziwe za aina gani na hata ziwe nyekundu kama damu ukiomba msamaha na atazisafisha na kuwa nyeupe.Mfano umeiba na ukajutia na kumuomba msamaha yeye anasahau na kusamehe kwa maana hakumbuki Kama ulifanya kosa Hilo na ndio maana ata yule mwizi msalabani alipoomba msamaha alisamehewa palepale

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
PILI - Sehemu ya 18


Inaendelea.............


Asubuhi kulipokucha nilijianda na nilimuaga Mzee Nchibaronda na kuondoka!
Yule Mzee Nchibaronda nilimwachia shilingi laki moja ile ya kitanzania pamoja na kiasi kidogo nilichokuwa nacho cha faranga!

Mzee usiku alikuwa ameniambia kwamba siku nitakayofanikiwa inabidi nirudi kumpa shukurani maana shukurani huwa ni lazima!

Kwakuwa wakati huo nilikuwa nina uwezo wa ajabu kutokana na ile irizi niliyowekewa mkononi kuna jambo nilifanya pale si la kawaida!,Nilitamka ya kwamba "Ninataka muda huu niwe ziwa Tanganyika",na kweli nilijikuta nipo ziwani kwa upande wa kongo!.
Kiukweli nilijiona kama nina bahati kuliko binadamu wote walioko kwenye hii sayari ya dunia!
Nilitembea hapo ufukweni kuelekea kaskazini mwa Congo na muda si mrefu nilifika pale kwenye Bandari ya Kalemii!,Bado nilikuwa sielewi ule uwezo wa kutembea kwa haraka ulitoka wapi lakini yawezekana ilikuwa ile Irizi ya malikia!

Nilipofika pale Bandarini nilikuta Boti nyingi za kisasa na niliuliza pale boti inaelekea kigoma nikaonyeshwa!,nipofika kwenye hiyo boti nilipanda na kuingia ndani na hakuna aliyeweza kuniuliza kuhusu nauli maana nilikuwa ninatamka tu na inakuwa!
Huu mtindo wa kusafiri bila nauli ndo yalikuwa maisha yangu siku zote tangu nilipotoka huko chini ya maji!
Ile boti haikuchukua muda sana ilianza safari kuelekea kigoma na masaa kadhaa ikawa imetia nanga bandari ya kigoma!

Nilipofika kigoma nilijaribu kumtafuta yule jamaa wa Mwanza kwenye simu lakini alikuwa hapatikani,Baada ya kumkosa jamaa nilijaribu kumtafuta mama na alipopatikana tulisalimiana na akaniambia wao wanaendelea vizuri!,Mama aliniuliza "Kwani ukowapi wewe?,mbona hujaja nyumbani takribani wiki mbili?"
Nilimwambia mama "Nitakuja kesho maana nilikuwa bize kuna kazi nilikuwa naifanya"
Baada ya mazungumzo na mama nilielekea hapo kigoma nikatafuta hotel kwa ajili ya kupata msosi!

Baadae nilitafuta hotel maeneo ya hapo kigoma kwa ajili ya kupumzika ili kesho nianze safari ya kuelekea Mwanza!
Usiku huo nilikuwa nawaza namna nitakavyokuwa tajiri na namna ya kufanya watu wasigundue utajiri wangu kuwa niwa kishirikina!
Kulipokucha Asubuhi nilielekea kupanda basi lililokuwa linaelekea Mwanza na kama kawaida nilipanda bure sikuweza kulipa nauli!

Wakati huo mrume ndago nilikuwa nina jeuri na kiburi kisichokuwa na mfano,maana niliona mimi ndiyo mimi na kwamba hakuna mbwa yeyote wa kunibabaisha!,
Kama kawaida Mwanza tuliingia mida ya usiku!
Nilipofika hapo stendi ya Nyegezi nilipanda bodaboda mpaka Geto kwangu!,Kwakuwa ile nyumba tuliyokuwa tumepanga ilikuwa na geti niligonga na kuna jamaa mmoja alikuja kunifungulia!
"Mwanangu mambo vp",jamaa alinisalimia,nkamwambia" poa kaka"
"Ulikuwa wapi kaka maana nilijaribu kukuulizia lakini kila mtu hakuwa na jibu"jamaa aliendelea kuniuliza!
Nilimwambia "Nilisafiri kidogo kaka,siunajua tena utafutaji?"

Basi nilielekea chumbani kwa yule jamaa ambaye tulienda nae kasulu maana nilikuwa nimempa funguo zangu anitunzie!,Nilijaribu kugonga akafungua lakini ilikuwa sura ngeni machoni kwangu!
Alikuwa mwanamke na mimi nilidhani uenda angekuwa mwanamke wa jamaa lakini kumbe kulikuwa na mpangaji mpya kwenye hicho chumba!
Nilimuuliza "Vp jamaa kalala",Yule dada aliniambia "jamaa yupi"?,Aliendelea kuniambia yeye hapo kahamia ana kama wiki mbili hivi!.
Nilimuomba samahani sana maana nilijua uenda ni mwanamke wa jamaa na nkamwambia hapo mwenye chumba alichohamia kulikuwa na mpangaji ambaye nilimwachia funguo za chumbani kwangu maana mimi nilikuwa nimesafiri!

Yule dada aliniambia nijaribu kuwauliza wapangaji wengine maana yeye hafaamu kitu chochote!

Nilienda kumgongea yule jamaa aliyenifungulia nikijaribu kumuulizia labda jamaa atakuwa kamwachia funguo!,Jamaa akasema "Hapana sikuachiwa funguo"

Kuna jamaa mmoja yeye shughuli zake zilikuwa za viwandani huko Igoma na uenda nadhani jamaa ndo alimwachia funguo!
Niliona isiwe taabu sana!,Nilielekea chumbani kwangu na niligusa kile kitasa kwa mkono wa kushoto ulokuwa na ile irizi na ukafunguka nikaingia ndani!
Kiukweli sikutaka mtu yeyote lile tukio alione na ndo maana nilijaribu kuutafuta ufunguo wangu na kwakuwa ilishakuwa usiku sikuwa na namna ingawa hakuna aliyeona nafanya nini!
Asubuhi jamaa alipokuja kutoka shift huko kiwandani alishangaa kunikuta nafanya usafi ndani kwangu!

"Aisee mambo vp"?,Umerudi lini"?,yalikuwa ni maswali aliyoniuliza,Nilimjibu nimefika jana usiku!
"Ulikuwa na funguo nyingine nini!,maana jamaa aliniachia funguo zako",Nilimwambia "Ndiyo nilikuwa na funguo moja maana hii niliyompa

Mlume ndago twende kazi
Mwenzio anajiita
mRume ndago
 
Back
Top Bottom