MKASA WA PILI - Sehemu ya 19
Inaendelea.............
Baada ya kuwa nimepata zile pesa niliona kwanza nianze ukarabati wa nyumba yetu hiyo ya hapo Nyegezi!
Mama yangu alikuwa na wasiwasi pesa ya ukarabati nimepata wapi!,Nilimwambia mama kuna mahali nimepata kazi ya kufundisha na hivyo ninalipwa vizuri!.
Basi kauli ile ilimtoa mama wasiwasi
Ile nyumba nilianza kuikarabati upya na kuanzia hapo kila nilipokuwa nikipata pesa kutokana na ajali zile nilizokuwa nikisababisha hapo mjini Mwanza na miji kama Geita na Magu,niliendelea kuisuka upya nyumba yetu na ikawa ya kisasa kabisa kama nyumba za matajiri!
Ulikuwa ukifika hapo nyumbani huwezi kuamini maana nyumba ilikuwa kama ya waziri fulani!
Nyumbani hawakutia shaka sana maana uwezo niliokuwa nao wasingeweza kufahamu zaidi!
Miaka nayo ilikuwa ikienda mbio na mimi pia niliendelea kufanya kafara!,Kuna siku nilishika mkono wangu huu uliokuwa na Irizi nikaanza kuongea "Mbona kafara natoa lakini bado napata pesa kidogo?"
Sauti ilinijibu kwamba muda wa kuwa tajiri haujawadia ila uko karibu!
Hiyo ilikuwa mwaka sasa wa 2013
Basi siku moja nikiwa Geto nilisikia sauti ikiniambia nielekee Mkoani Singida maeneo ya Sekenke ambako ilipaswa kuna watu wafe ili niweze kupata mali nyingi!
Asubuhi ya siku hiyo sikutaka kabisa kupoteza muda!,Kuna dawa nilizichanganya hapo ndani kwangu na nikatamka ya kwamba "Nahitaji kufika sekenke Singida"
Ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua!,Mpaka muda huu nilikuwa nishasema liwalo na liwe kama ni maji nishayavulia nguo sharti niyaoge!
Kwakuwa nilikuwa nina kiburi kwa wakati huo nilijiona kama hakuna wa kuniweza hapa duniani!
Nilipofika maeneo hayo ya Sekenke kuna gari ambayo nilielekezwa toka Mwanzo na ndani yake kuna abiria ambao walikuwa wakisakwa kwa udi na uvumba kutoka huko majini nilikotoka hivyo siku hiyo ilikuwa ndo Mwisho wao!
Basi kuna dawa niliitupa kwenye barabara na ile gari ilipofika yale maeneo ilipasuka tairi ya mbele na kukosa uelekeo hali iliyofanya kupiga mzinga wa maana!Kiukweli nilikuwa nina roho ya kikatili sana kwa wakati huo!,Nilikuwa sina huruma kabisa hata chembe!
Niliokuwa nina huruma nao ni ndugu zangu pamoja na mama yangu!
Baada ya ile gari kuwa imepata mzinga nilisogea pale na kukuta wale watu niliokuwa nimetageti wamebanwa na viti kwa chini,Nilifika nikawachinja kichawi na kuchukua damu zao!Pia nilichukua damu za abiria wengine waliokuwa wamekufa kwa wakati huo na nilihakikisha nawakausha kabisa wasiwe na damu hata tone!
Nilipomaliza nilifanya fasta na kuondoka zangu na mara hiyo nikawa pale geto,Nilichukua kile kibuyu kama kawaida nikakiweka uvunguni!
Niliondoka zangu kuelekea kwa Bi mkubwa kuangalia maendeleo ya nyumba!
Nilipojiridhisha ya kwamba mambo ni mazuri nilirudi zangu tena geto!
Safari hii nilikuta kitandani kwangu kuna begi kubwa yale ya mgongoni ambayo watoto wa shule wanayowekaga madaftari nikakuta limejaa pesa!
Siku hiyo nilikuwa nina furaha sana maana sikuwahi kukamata pesa nyingi kiasi hicho!
Sasa nikaanza kuzihesabu pale nilipata kama milioni thelathini na tano pesa za kitanzania (35,000,000/=)
Niliondoka hapo geto kwangu kuelekea Igoma na lengo ilikuwa ni kutafuta eneo nianze ujenzi!
Kuna dalali nilimpata maeneo ya huko Igoma jamaa akaniambia viwanja vipo lakini kuna nyumba zipo zinauzwa!
Alipo niambia nyumba zipo zinauzwa wazo la kununua uwanja nikalitoa kichwani!,Nilimwambia anipeleke kwenye hizo nyumba anazozifahamu zinazouzwa.
Jamaa alipeleka kwenye nyumba ya kwanza ambayo ilikuwa ya kawaida!,Tuliendelea kutembelea zile nyumba ambazo zilikuwa zikiuzwa na kuna nyumba tulifika kiukweli niliipenda sana!
Jamaa aliniambia nimwachie namba ya simu na atakomuniketi na tajiri wa hiyo nyumba halafu atanijulisha!
Basi nilipoachana na yule dalali wazo lingime ambalo nilikuwa nalo ni kutafuta mwanamke wa kuishi naye ambaye niliambiwa atakuwa akibeba ujauzito wale watoto watakuwa wanatolewa kafara!,Yaani yule mwanamke ntakuwa ninaishi naye kwa kazi hiyo tu!
Na yeye hapaswi kuelewa kitu!
Sasa akilini mwangu niliwaza kwamba nataka nimchukue yule shemeji yangu aliyekuwa na nyodo niwe nampiga shipa na yeye awe kama mke wangu kwa kazi hiyo tu!
Kiukweli nilitaka nimkomoe maana alikuwa na nyodo sana!
Ila nilitaka kwanza nikiisha inunua hiyo nyumba na kuvuta usafiri ndo nifanyie kazi ilo suala!
Nilirudi geto na kukuta tena pesa zimejaa kwenye lile lile begi ambalo mara ya kwanza nilitoa zile pesa!,Japo hazikuwa nyingi kama za mara ya kwanza,Safari hii nilipozihesabu ilikuwa kama milioni 20,Hivyo ukijumlisha na zile za mara kwa za ilikuwa kama milioni hamsini na tano(55,000,000/=),Kiukweli nilipagawa sana!
Nakumbuka siku hiyo nilimpigia mama yangu simu nikamwambia "Mama nimekuagizia gari na wiki hii itakuwa inaingia"
Bi mkubwa aliniuliza "Mwanangu pesa unatoa wapi"?,Niliendelea kumdanganya kwamba nimechukua mkopo kwenye kituo nilichokuwa ninafanya kazi kwa wakati huo!
Ndani ya wiki hiyo nilienda kwenye Show room moja iliyoko karibu na kamanga fery(nisingependa kuitaja) nilitoa pesa cash nikamnunulia Bi mkubwa Murano mpya!
Sasa kwakuwa mimi ilipaswa nikaonane na yule dalali wa Igoma nilimpigia simu nikamwambia anapelekea gari yake!
Kuna dereva wa pale show room nilimpa namba ya Bi mkubwa ili akifika maeneo yale amwelekeze!
Nilipofika Igoma yule dalali alinikutaniaha na mmiliki wa ile nyumba na nikaongea nae jamaa akasema nimpe milioni 60,kwa wakati huo nilikuwa nimebaki kama na milioni 30 maana pesa nyingine nilimnunulia Bi mkubwa gari, siku iliyofuata nilimpelekea na nikamwambia pesa nyingine ningempa siku si nyingi!,Lile jumba lilikuwa la kisasa halafu zuri,hivyo nikaona litanifaa kwenye mambo yangu!
Basi niliondoka kuelekea kwa Bi mkubwa na alifurahi sana maana sasa aliishi maisha kam mtu!
Kwakuwa hakujua kuendesha gari ilibidi nimtafutie dereva na nikawa namlipa kila mwezi!
Siku ziliendelea kusonga na siku moja nilielekea mkoani shinyanga kupiga tukio la kafara kama kawaida!
Itaendelea..............