Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI - Sehemu ya 20.


Inaendelea.............



Niliondoka hapo geto kwangu nikiwa nimejianda kikamilifu kwa ajili ya kuelekea Shinyanga,nilifika maeneo fulani panaitwa Tinde,pale Tinde kuna njia moja ilikuwa ikielekea Kahama.Sasa kabla hujafika Kahama,hapo katikati huwa kuna mji unaitwa Isaka,tukio nililoenda kupiga siku hiyo ilikuwa katikati ya Tinde na Isaka!.Nilipofila pale nilianza kuangalia magari yanayopita!,nilikuwa nina uwezo wa kuliona gari lote na uwezo wa abiria waliokuwemo ndani,Kama hilo gari lilikuwa limebeba watu waliokuwa wamejizindika nilikuwa nina achana nalo.

Mara nyingi mshirikina yeyote au mchawi akimuona mtu hata kama analindwa na Mungu yeye kwa akili yake anajua huyo mtu atakuwa na dawa kali kuliko zake!,hiyo hali na mimi nilikutana nayo kwenye baadhi ya magari na kiukweli nilikuwa nina achana nao maana nilijua naweza kupata majanga.Nilipokaa kwa muda mrefu yale maeneo niliona kuna gari aina ya Noah lilikuwa inakuja kwa kasi sana!,nilipopiga darubini yangu ya kishirikina niliona waliokuwa ndani ya hilo gari walikuwa watupu,hawakuwa na chochote ambacho kingenizuia mimi kufanya tukio.

Kuna tego nililiweka pale barabarani,gari ilipofika yale maeneo ilipata ajali ambayo ilipelekea matairi kuangalia juu,palepale walikufa watu 3,ndani ya lile gari kulikuwa na mwanaume na mwanamke wamekaa mbele na nyuma kulikuwa na abiria 5,kwa muonekano wa lile gari nadhani wale wa mbele walikuwa ni mke na mume ambao walionekana kabisa ndiyo wamiliki wa lile gari,wale wengine nadhani walikuwa tu abiria ambao walikuwa wamewachukua njiani ili kupata hela kidogo!.Nililisogelea lile gari kisha nikachukua kibuyu na kuanza kuweka damu!,nilihakikisha siachi hata tone la damu na wale ambao niliwakuta hai nilihakikisha nawanyonya damu yote kiasi kwamba hata wangepelekwa hospitali wasingefika kabla hawajafa.Nilipomaliza kufanya kilichonipeleka niliondoka yale maeneo pasipo kuonekana na yeyote!.Nilipofika geto kama kawaida nilichukua kile kibuyu nikakiweka chini ya uvungu na mimi nikaondoka zangu kupiga mishemishe zangu za ualimu!.Kwa wakati huo nilikuwa nina pendeza sana na isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kujua nilichokuwa ninakifanya!.

Sasa pale shuleni nilipokuwa nikifundisha kama kuzuga ili nionekane nina kazi,kuna mwanamke mmoja alikuwa mwalimu mwenzangu ameajiriwa,kumbuka mimi nilikuwa mwalimu temporary mpaka wakati huo.Yule Mwalimu alikuwa mzuri sana na alikuwa na maringo sana,kuna wakati unaweza kumsalimia asikuitikie kisa tu alikuwa mzuri,wengine tulionekana vibaka tu kwake,Kwa wakati huo alikuwa na gari ambayo inasemekana alinunuliwa na jamaa yake ambaye tuliambiwa alikuwa na pesa balaa!.Huyo mwalimu alikuwaga na kigari fulani hivi kinaitwa Duet.Nilijiapiza ya kwamba wikiendi itakayofuata,yaani ndani ya wiki hiyo lazima atanitambua maana nilisema lazima nimkung'ute bakora za kim-kakati,basi baada ya vipindi kumalizika nilirudi zangu nyumbani,nilipofika nilikuta kama kawaida begi lile limejaa pesa,nikaanza kuzihesabu mara hii zilikuwa milioni 15,nilizitoa kwenye begi nikaziweka kwenye sanduku ambalo ndilo nilikuwa natunzia hela na lile begi nikalirudisha uvunguni!.Wakati huo kwakuwa ndiyo kwanza mwezi ulikuwa umeanza nilikuwa nimelipwa vihela vya kazi yangu hiyo niliyokuwa naifanya ya ualimu.Kiukweli nilikuwa sioni faida yeyote ya ile hela kwa wakati huo maana nilijiona kama ni pesa nilikuwa nayo ya kutosha,hivyo kule nilienda tu kufanya kazi kama geresha tu!.

Sasa niliamua kulivalia njuga suala la yule mwalimu aliyekuwa na maringo,Kuna dawa nilitengeneza hapo ndani nikaiweka mfukoni nikaondoka zangu!.Kwa ile dawa hakukuwa na kiumbe yeyote analiyeitwa mwanamke ambaye alikuwa anauwezo wa kunikataa,mimi na wanawake ilikuwa ni mbalimbali ila nilikuwa nashughulika na wale tu waliyokuwa na nyodo na dharau!.Nilipofika shuleni niliendelea na shughuli zangu kama kawaida na nilipopata wasaa wa mapumziko nilimfata yule mwalimu aliyekuwa kaumbika kila idara,nikamsalimia,siku hiyo aliitikia salamu yangu kwa uchangamfu kama wote!.Nilimuomba atakapotaka kuondoka anipe lift,ndipo akakubali akasema "Ondoa shaka".

Sikuwa na wasiwasi maana nilijua huyu tayari ni wa kwangu!Baadae nilipomaliza kufundisha ilibidi nimsubiri,alipomaliza vipindi vyake tuliondoka zetu akanibeba kwenye hicho kigari chake!.Tukiwa ndani ya gari sikutaka kupoteza muda nilimgusa mkono na palepale alisema "leo naenda kulala kwako".

Nilimuuliza "Kwanini?".

Akaendelea kusema "Huwa nakupendaga muda mrefu sema hujuagi tu".

Nilitambua tayari kitu ile dawa ilikuwa ishafanya kazi yake,alikuwaga hanaga muda na mtu hasa ukizingatia kipindi kile nilikuwa nimechoka isingekuwa rahisi kupendwa na mwanamke mzuri kama yule!.Kwakuwa hapo kwenye hiyo nyumba niliyopanga kulikuwa na geti,hivyo kuliwezesha lile gari lake kupata nafasi ya kupaki!.Ilikuwa mida ya jioni ambapo wapangaji wenzangu walikuwa wakishangaa namna nilivyokuja na yule mwanamke mzuri,wengi walishangaa kwasababu hawakuwahi kuniona pale nyumbani na mwanamke yeyote!.Tulipofika nyumbani nilimwacha geto mimi nikaelekea zangu kununua nyama ya kuchoma na viazi vilivyokaangwa(chips)nikamletea.Mle ndani kwangu nilikuwa najitahidi kupaweka safi maana sikutaka yeyote afahamu kilichokuwa kinaendelea,nilihakikisha kile kibuyu nimekificha kimazingara hakuna yeyote aliyekiona ila mimi tu!.

Kiukweli usiku huo yule mwanamke akuhusahau maana nilimkung'uta bakora za ki-mkakati zilizokuwa na ujazo wa hali ya juu.Asubuhi kulivyokucha alikataa kuamka kabisa akasema kama nikufukuzwa kazi basi afukuzwe ila pale aondoki maana hajawahi kukutana na mwanaume kama mimi!,nilimsihi sana twende kazini lakini aligoma katakata!.Basi siku hiyo nzima tulishinda hapo nyumbani nikimchapa bakora za hali ya juu,kiukweli nilikuwa sichoki maana nilikuwa nina uwezo wa ajabu sababu ya ile irizi!,Nilimchapa bakora za kutosha mpaka alishindwa kuamka kabisa akawa kama mgonjwa siku hiyo nzima.Sasa Kuanzia hapo nilimtengenezea dawa ambayo ilimfanya akamsahau yule jamaa yake ili awe ananiwaza mimi tu,lakini baadae nilikuja kuona anaweza kuwa mwendawazimu maana alikuwa kama kachanganyikiwa kwa ajili yangu!,Nililegeza kidogo akawa anaenda kwa jamaa yake kama kawaida ila nilipomuhitaji nilimpata kwa wakati niliotaka mimi.

Yule jamaa wa Igoma mwenye nyumba alinipigia simu akawa ananikumbushia kuhusu kile kiasi kilichokuwa kimebaki,nilimwambia ndani ya siku mbili ningempatia.Kwenye begi nilikuwa nina milioni 15,hivyo pungufu ya kumpa mzee ilibaki milioni 15 nyingine!,kwakuwa wakati huo haukuwa mwisho wa mwezi ambapo niingeenda kufanya tukio ili nipate pesa,nilitumia dawa na nguvu ya irizi niliyokuwa kumshawishi yule mwanamke mwalimu amwambie mumewe ampe milioni 15,nilitamka pale kwenye mkono wangu wa kushoto uliyokuwa na ile irizi ya kwamba amuombe yule jamaa yake hiyo hela aniletee na jamaa asihoji chochote!.Hivyo ndivyo ilivyokuwa!,Yule mwanamke alionekana kuchizika na mimi kwani kila nililomuambia kwa wakati huo alilifanya.Baada ya siku hizo nilizomuahidi mzee kweli nilimpelekea ile hela kisha tukaandikishiana,ndipo sasa nikakabidhiwa ile nyumba rasmi!.Kiukweli lilikuwa bonge la nyumba ambalo niliona lingenifaa sana kwenye shughuli zangu.

Nilipanga ya kwamba,ikifika mwisho wa mwezi nikienda kupiga tukio pesa ambayo ningepata ningenunua kila kitu cha ndani na kuhamia huko Igoma.



Itaendelea...................
 
Hapa nimejifunza kitu..
Usione mtu kachepuka/kakuacha /upendo umepungua ukajua ni hali ya kawaida aisee jamani maombi ni muhimu sana kwenye mahusiano/ndoa zetu, Mungu atusaidie kwakweli..
 
Vijana wakisikia watapata uwezo wa kupiga shipa demu yyt yule wanachanganyikiwaaaa!!

Mzee twende kazi... Ndo tushafika
 
Shusha nondo mzee baba
 
Nimeshaanza nayo hii ya Zabron leo niko episode ya tatu

Huwa sipendi ujinga
 
Tukeshe tikiomba, mie huwa sio muombaji wa Mara kwa Mara, ila kwa huu ushuhuda ni mwendo wa maombi bila kukoma. Wadau maombi ni silaha tosha. Tayari nishawachapa dada zangu ombi la asubuhi wanaelekea Mwanza ndani ya Ally's Star.

NB. Wadau wadau msiombe dawa mwende mkapige Dada zetu shipa la kimkakati, muwaache wawapende wenyewe, halafu sasa uzuri akikupenda yeye utamkunja utakavyo bila stress.
 
Jamani huyu Mwalimu anayepigwa shipa na Magere si atakiona hicho kibuyu na fuko la pesa uvunguni mwa kitanda?
hebu tusubir labda akahamie Igoma, akiendekeza kuwatandika atahariu dawa sasa hivi
 
Jamani huyu Mwalimu anayepigwa shipa na Magere si atakiona hicho kibuyu na fuko la pesa uvunguni mwa kitanda?
hebu tusubir labda akahamie Igoma, akiendekeza kuwatandika atahariu dawa sasa hivi
Jamaa keshakwambia hizo vibuyu amezifanyia mambo anaviona yeye tu...Soma ukiwa umetulia jombaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…