Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI - Sehemu ya 22.


Inaendelea.............



Nilipofika nyumbani kwa mama nilimkuta akiwa na wageni,hizi pesa acheni ziitwe pesa maana wakati hatuna hela yaani hata wageni kututembelea ilikuwa nadra sana.Ile nyumba nilikuwa nimeikarabati sana,nilipiga fensi ya ukuta kuzunguka nyumba nzima,kiukweli ulikuwa ukifika hapo nyumbani kipindi hicho,ulikuwa unashangaa sana.

Basi baada ya muda nilipomaliza kupata chakula nilimuaga mama nikarudi zangu geto kwangu.Nilipofika geto niliyatupa macho kitandani,ndipo nilikuta lile begi limejaa pesa ,safari hii zilikuwa nyingi maana nilianza kuzihesabu nilitumia muda kidogo,nilipata jumla yake milioni 38 zile noti zilikuwa mpya sana!.Kiukweli wakati huo nilikuwa nawaona watu wote wanaotafuta pesa kwa jasho ni wajinga wanaopaswa kuuawa na dunia yote niimiliki mimi!,nilikuwa nina kiburi sana,kwakuwa niliishazoea sasa kukamata hela nyingi kwa mkupuo hata kiwewe kiliniondoka!.Nilizichukua zile hela nikaziweka kwenye begi kubwa na kile kibegi cha mgongoni nikakirudisha chini ya uvungu,Kitu ambacho nakumbuka niliambiwa nisije kufanya ni kuziweka zile pesa kwenye akaunti benki!,Yaani niliambiwa nisije thubutu katu kuweka hizo pesa benki.

Baada ya kupata hizo pesa niliondoka hapo nyumbani kuelekea mjini,lengo langu ilikuwa ni kwenda kununua kila kitu cha ndani,sasa kabla sijanunua,Kuna dada mmoja aliyekuwa hapo dukani aliniambia kuna kampuni ya upambaji wa majumba (decorations) wanafanya nayo kazi,kama nitaweza awapigie simu waje niwapeleke kwenye nyumba yangu na wao watanishauri namna ya kuipamba ile nyumba ili iwe na muonekano mzuri kwa ndani,Kwakuwa sikutaka kuonekana mshamba kwa yule dada ilibidi nimwambie awaite twende Igoma.Wale jamaa hakika walikuwa wamesomea hiyo kazi maana walinishauri kila kitu na aina ya mapazia yanavyopaswa kuendana na masofa.Baada ya kunipatia hayo maelekezo niliwauliza wao kuipendezesha nyumba nzima ingegharimu kiasi gani?,kuna mwanamke aliyekuwa mwarabu,na ndiye alikuwa mmiliki wa ile taasisi aliniambia wao kuweka kila kitu humo ndani mpaka kufikia kuhamia,ilikuwa inagharimu Tsh milioni 25.Basi nilimwambia yule mwanamke wa kiarabu kwamba,turudi mpaka kwenye lile la duka la samani(furniture),wakanisubiri nikawaletee pesa.Tuliondoka huko Igoma kuelekea mjini,tulipofika kwenye lile duka,wao niliwaacha nikawaambia wanisubiri nikawaletee pesa waliyoitaka,ndipo mimi nikaelekea geto kuwachukulia zile pesa.

Baada ya kurudi na zile pesa,kila mtu alishangaa kijana mdogo nawezaje kuwa na pesa nyingi kiasi hicho.

Niilimuuliza yule mwanamke "itachukua siku ngapi mpaka mimi kuhamia kwenye nyumba yangu?".

Aliniambia "Tupatie wiki moja bosi wangu".

Nilimkabidhi ufunguo na ile nyumba nikamwambia awe makini!.Nilipotoka hapo dukani nilielekea mtaa mmoja kuna duka walikuwa wanauza vito vya thamani kama heleni,pete na cheni za dhahabu.Kuna dada mmoja alikuwa mwarabu ambaye wakati huo alikuwa kafunga ushungi ndiye nilimkuta kama muuzaji wa lile duka,pia kuna wauzaji wengine niliwakuta humo ndani lakini mimi nilitaka nihudumiwe na yule mrembo,kilichonipeleka hapo dukani,ni kwamba nilikuwa nataka nimchukulie yule mwanamke wangu mwalimu mkufu na pete ya dhahabu!.Kiukweli yule mwalimu licha ya kutaka kumkomoa lakini nilianza kumpenda sana.Basi nilimsalimia yule mtoto mzuri wa kiarabu aliyekuwa akiuza,bahati nzuri alinisalimia kama tunajuana.Baada ya kuwa nimemaliza kufanya manunuzi,nilimuomba yule dada anipatie namba yake,nilimwambia nilikuwa nina maongezi naye baadae!.

Yule dada aliniambia "Maongezi gani kaka?".

Nilimwambia "ni maongezi ya kawaida tu mrembo".

Aliniambia "Kwani huwezi kuniambia hapa mpaka nikupatie namba yangu ya simu?".

Nilimuuliza "Kwani umeolewa?".

Akaniambia "Hapana".

Nikamuuliza "Sasa kama bado hujaolewa kwanini unaninyima namba?".

Alishindwa kunijibu akawa anaendelea na shughuli zake.

Nilimuuliza "Unaitwa nani?".

Akajibu "Naitwa Zainati".

Nilimsihi sana Zainati anipatie namba yake lakini akasema hawezi kutoa namba na endapo nikiendelea kumsumbua angemuita mlinzi!,basi nikaona isiwe kesi sana maana kuna wateja wengine walianza kuingia mle dukani.

Nilimwambia "Yaani Zainati pamoja na kutumia gharama kubwa kukuchangia lakini bado unaniona kama kibaka?".

Niliachana naye nikawa nimeondoka zangu lakini niliapa nikasema "lazima anitambue mimi ni nani,hawezi kuniletea dharau kiasi hiki wakati uwezo wote ninao".

Jioni nilimpigia simu yule mwalimu akaja geto kwangu nikampa zile zawadi zake,kiukweli alifurahi sana na alinishukuru sana.Basi siku hiyo alilala hapo kwangu na asubuhi kulivyokucha alielekea shuleni kama kawaida,mimi nilimwambia kuna mahala nilikuwa naelekea hivyo nisingeenda huko shuleni siku hiyo.Nilikaa nikawaza nikasema sasa ilipaswa nirudi kwa mzee Nchibaronda kumrudishia shukurani kama alivyoniambia,Pia kuna dawa kadhaa pale ndani zilianza kuniishia,hivyo nilitaka nikaongeze nyingine.Siku hiyo nilishinda hapo nyumbani lakini alfajiri ya siku iliyofuata niliondoka kuelekea Kigoma,Nilipofika kigoma sikutaka itumia ile njia ya mkato ya kutamka,maana mzee aliwahi kuniambia hilo ziwa Tanganyika lina nguvu za ajabu hivyo niwe makini,nilifahamu ningetumia ile njia ya kuukamata mkono na kutamka ingekuwa ni hatari kwenye lile ziwa,hivyo nilitumia boti kama kawaida mpaka Kalemii na nilipofika Kalemii niliunganisha kwenda mpaka Moba kisha nikachukua usafiri mpaka kijiji cha Kirungu.Wakati huo sikuwa na pasipoti ila hakuna aliyeniuliza kwasababu nilikuwa nikitumia ushirikina.

Nilimkuta mzee Nchibaronda na aliponiona aliniambia "Wewe kijana ni mwaminifu sana".Tulipiga stori sana akawa ananiuliza namna nilivyoweza kufanikiwa!.Nilitoa kiasi cha milioni 2 nikampatia mzee na akaniambia huo ni mwanzo tu bali mambo mazuri yanakuja.Nilimweleza kilichonipeleka kwake mbali ya kutoa pesa ya shukurani lakini pia kuna dawa zilianza kuisha.

Mzee aliniambia "Ondoa shaka mwanangu hapa umefika".

Aliniambia "Kesho tutaongozana wote msituni tukachume dawa!".

Asubuhi kulipokucha tulielekea msituni tukaanza kuchuma dawa kwenye ile miti aliyoifahamu yeye na mingine pia niliifahamu.Basi kuna mti mmoja alinionyesha pale akanimbia kwamba "Unauona huu mti?".

Nilimjibu "ndiyo nauona mzee".

Akanimbia "huu mti kuna dawa unaichanganya halafu unaitengeneza kama chai na ukiinywa unaweza kulala na wanawake hata watano kwa pamoja na ukawashughulikia kisawasawa,wasipo zimia basi wanaweza kabisa kupoteza maisha maana wewe utakuwa huchoki ila wao cha moto watakiona!".

Huo mti nakumbuka wakati nikiwa Tabora kwenye pilika zangu za ushirikina niliwahi kuuona.

Basi mzee akaanza kunielekeza namna ya kutengeneza ulikuwa unachanganya na majani fulani hivi ya mti fulani halafu unaukausha!.Nilikuwa najisemea kimoyo moyo kwamba nikirudi Mwanza nataka Zainati anitambue vizuri kwamba mimi ni nani!,mzee alinichumia dawa nyingi za kutosha,kwakuwa nilikuwa ninafahamu sasa namna ya kuzichanganya sikupata shida sana!.Tuliondoka msituni kurudi kwa mzee Nchibaronda na mimi sikutaka kupoteza muda nilimuaga mzee akaniambia ananitakia mafanikio mema.Niliondoka zangu kurejea Kigoma ili nirudi Mwanza!.Nilifika kigoma muda ulikuwa umekwenda sana hivyo nililazimika kulala hotelini na asubuhi nilidamka kuelekea kwenye magari ya Mwanza kwa ajili ya safari.





Itaendelea....................
 
Aloo mkuu hii episode ya 20 imenifanya nitafute nyumba ya ibada nikaswali.
 
Unasema kweli??
 
Nilikuwa nashauri pia hizi contacts uziweke mwisho wa kila post yako, ili namba zako ziwe rahisi kuwa traced...!!

We're together in this one usijali.!
Carleen mpnz. Sevu Ile namba kwenye hiyo iPhone yako, Kisha kabla ya kufanya shopping ya Xmas kwa vitu visivyo vya muhimu. Mtumbukizie mRume ka hamsini au hata ka laki..
 
Ni youtube mama sio uzi wa humu

Ila kwa humu kuna uzi wa Bilionea Bazoka ndio nilikua napotezea mawazo naposubiri hii sema yule mwandishi mnyanyasaji sana
Niite huko basi, ila huko youtube pia ntaenda[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…