Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Wakuu kuna kazi naifanya hapa homu na nkimaliza nadhani usiku huu ntaanza kusimulia kisa cha pili kama nilivyoeleza hapo awali,ni kisa kirefu kidogo hivyo muwe na subra!!
Chonde chonde story ijayo itiririshe kwa kila unachokumbuka. Achana na wasiokuwa na subra wanaokulazimisha kufupisha story!! Tunasubiri, nna imani tutapata funzo zaid ktk mkasa ujao.
 
UTAJIRI WA NGUVU ZA GIZA ULIVYOHARIBU MAISHA YANGU- Hiki ndicho kisa cha pili cha maisha yangu,hapo mwanzo nilisema nina visa viwili,cha kwanza nimeshakisimulia,hivyo hiki ni kisa cha pili.KARIBUNI MJIFUNZE.




MKASA WA PILI- Sehemu ya 1.



MWAKA 2012.



Baada ya kuwa nimemaliza shule ya sekondari nilirudi nyumbani Mwanza,baada ya mama kuwa ameuza ile nyumba ya Tarime ilibidi ajenge nyumba nyingine Mwanza,japo haikuwa kubwa kama ile ya Tarime lakini kwa kiasi fulani ilikuwa nzuri naya wastani!,nilirudi nyumbani nikawa nafundisha wanafunzi tuisheni ili angalau niweze kupata hela za kununua sabuni na mahitaji madogo madogo,sikuweza tena kumuomba mama pesa maana tayari nishakuwa mtu zima,pia kwa wakati huo hali ya mama haikuwa nzuri kifedha,kuna shuke moja ambayo haikuwa ya serikali huko maeneo ya buhongwa,waliniajiri kama mwalimu wa muda na wakawa wananilipa kutoka na vipindi ambavyo nilikuwa nikihudhuria,hivyo nilikuwa nikitoka hapo shuleni naelekea ilipokuwa kituo cha tuisheni kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi masomo ya ziada,nilikuwa nalipwa na wale wanafunzi Tsh elfu 3000 kila nilipokuwa nikimaliza topic.

Basi kuna siku katika pitapita zangu mtaani wakati natoka huko shuleni,kwa mbali kidogo nikamuona jamaa mmoja tuliyekuwa tumesoma wote shule ya msingi Turwa kule Tarime,kiukweli sikuweza kufahamu kama ndiye au nilimfananisha,jamaa alikuwa pembeni anaongea na simu,hivyo nilijaribu kusogea karibu nione kama ndiye!.Kweli!,baada ya kusogea karibu nikamwita jina lake,jamaa aliitika na aliponiona alinifanyia ishara kwamba nisubiri kwanza amalize kuongea na simu,basi jamaa alipomaliza kuongea na simu alifurahi sana kukutana na mimi,mimi pia nilifurahi sana maana jamaa alikuwa kabadilika sana na kanenepa ile kishenzi,watoto wa mjini wanasema "Shavu dodo",kiukweli jamaa alikuwa kanawili,nilivyomuona tu nilifahamu lazima alikuwa na maisha mazuri.

Jamaa aliniuliza "Aisee za miaka mingi?".

Nikamjibu "Nzuri".

Jamaa akaniambia "Hebu nikumbushe wewe ni nani na nilikuona wapi vile!".

Kimoyo moyo nilijisemea "Ina maana jamaa mara hii kanisahau au ndiyo mambo ya mjini?".

Basi ilibidi nimkumbushie jina langu na tulisoma wote Tarime,jamaa alicheka sana,ndipo tukaanza kukumbushiana matukio,vimbwanga na vitimbi vya shule!,tulipiga michapo sana na nikamueleza mimi niliendelea na shule na nikamwambia Tarime tulihama muda sana.Jamaa alinichukua tukasogea mbele kidogo kumbe alikuwa kapaki gari!.Tulipanda kwenye gari kuelekea maeneo ya Igoma ambako alikuwa kachukua hoteli huko.Wakati tukiwa kwenye gari alikuwa ananiambia kwamba yeye baada ya kumaliza shule ya msingi matokeo yake hayakuwa mazuri,hivyo ilibidi aende kutafuta maisha,akaniambia yupo huko mkoani Geita sehemu moja inaitwa Katoro,kajenga huko na maisha yake yapo huko,ila siku hiyo alikuwa kaja hapo Mwanza kwa ajili ya biashara zake nyingine.Huyu jamaa kipindi tunasoma alikuwa hajiwezi kimasomo(kilaza),kiukweli ningeshangaa sana kusikia aliendelea na Shule!.

Baada ya kufika hapo hotelini alipofikia mimi nilikaa nje yeye akaingia huko ndani,muhudumu alikuja kuniuliza natumia nini lakini nilisita kumwambia maana sikuwa na kitu, mtu ambaye ndiye mwenye pesa alikuwa kaingia ndani,hivyo nisingeweza kuagiza bila ruhusa ya mtoa pesa!,baada ya dakika kadhaa jamaa alikuja kwa mbwembwe huku akiniambia "Mwanangu agiza chochote uletewe ule".


Kabla sijamuita muhudumu jamaa alipaza sauti "Wewe muhudumu njoo umsikilize jamaa hapa".Mrume ndago niliagiza wali samaki pamoja na Soda.

Jamaa aliniuliza "Vipi mwanangu upigi mambo yetu?".

Nikamwambia "Hapana kaka sipigi".

Jamaa akaniambia "inaonekana kijana ushakuwa mlokole,yaani ukorofi na utundu wote ule wa shule ya msingi hupigi huang'unywa?".

Neno "Huang'unywa" alimaanisha pombe,ndizo lugha tulizokuwa tunazitumia kipindi hicho tukiwa wadogo.Basi stori za hapa na pale ziliendelea tukiendelea kukumbushana jamaa na marafiki tuliosoma nao,baada ya kumaliza kula ilibidi nimuulize jamaa alikuwa anapiga ishu gani!,maana alikuwa kanawili sana na ukiangalia mimi wakati huo nilikuwa nimechoka ile kishenzi.Jamaa aliniambia yeye anajihusisha na mambo ya madini ila akasema isingekuwa vyema tuongee pale hilo jambo ila aliniambia nijitahidi nitafute siku niende Geita,ndani ya siku chache ili nika-experience maisha ya kule namna yalivyo.Basi baada ya hapo jamaa akanipa elfu 30 ,mimi nikamuaga ila nilimwambia sina hata simu,aliniambia nisiwaze nijatahidi nitafute siku niende huko Geita kwani angesababisha hayo yote!,Baada ya maongezi nilimuaga jamaa ili kuondoka,alinipakia kwenye gari yake mpaka mabatini kisha nikachukua daladala za kuelekea Nyegezi nyumbani!.

Kiukweli ile elfu 30 niliona kama kanipa milioni,ukizingatia nilikuwa nimepigika na maisha ile sana!,Pia nilikuwa nawaza sana,inawezekanaje mtu niliyemzidi kila kitu kuanzia akili,elimu mpaka maisha enzi hizo leo anizidi maisha?,niliumia sana lakini sikuwa nala kufanya!,sasa pale nyumbani kuna hela nilikuwa nimesevu,hivyo nikachukua na hii jamaa ambayo alinipa nikajumlisha ikawa ya kutosha japo si haba!,kesho yake ilibidi niingie kwenye mitumba kusaka nguo za kushindia hapo mtaani.Nilipata suruali mbili nikanunua na makobazi pamoja na sweta.

Baada ya wiki nilianza kuwaza namna ya kwenda Geita ili nikaonane na jamaa uenda angenipataia kazi yoyote nifanye maana niliona kama nimechelewa sana katika maisha!,jamaa kipindi tupo hotelini kule Igoma, alinipa direction ya kwamba nikifika Katoro kuna jina alilokuwa analitumia huko lilikuwa maarufu sana,hivyo alinitajia hilo jina akasema endapo nitafika hapo nikimuuliza hata watoto wangenipeleka kwake!,lile jina lake la shule ya msingi aliniambia kule hakuna aliyekuwa analifahamu bali lilikuwa limebaki kwenye vyeti vya kuzaliwa tu.




Itaendelea......................
 
haya True story ya pili imeshaanza wengi watapotea ni bora zote zingekuwa post ya kwanza tukaendana na Ashura jini jike
lkn Mtunzi Magere usihofu kuna vijana wakifika wataziunganisha na kusomeka pamoja
 
Mkuu LwandaMagere
Shukrani kwa kisa ulichokileta jukwaani. Binafsi nimeinjoi kukisoma. Lakini zaidi nimefurahia kuisoma mitaa niliyokulia pia. Nimekaa Bomani hapo na nimesoma Buhemba mazoezi, hivyo mitaa unayoitaja mingi nimeiishi. Maisha ya Tarime yalinijenga mno, hasa namna ya kukabiliana na ubabe kwa ubabe, so kusoma hapa mitaa hii imenipa kumbukumbu nzuri.

Kuhusu critics, usiziweke sana akilini. Ukiona mtu anakuponda huku anasoma hadi episode ya mwisho, jua anakukubali kiaina. So write what and how you feel. Tusiofurahia ulichoandika tutakuponda ila bado tutarudi tena kukusoma. Jukwaa lahitaji waandishi wengi so keep them stories coming.

Kiga buhemba sehem gan ndg maana me ndo home na mshkaji anavyosimulia maeneo najiona home kabisa
 
Back
Top Bottom