jooohs
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 2,524
- 10,287
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu acha basi na ww pia mshikaji wangu unaleta mambo za ajabu[emoji23][emoji23]raha ya story aelezee kila hatuaKuacha ni ngumu maana nina uraibu na usomaji wa stori wakuu
Nimeacha wacha tumvumilie[emoji23]Mkuu acha basi na ww pia mshikaji wangu unaleta mambo za ajabu[emoji23][emoji23]raha ya story aelezee kila hatua
Nitakutoa nje sasa hivi choko ww🙄🙄🙄 endelea kuchonga tu....Stori ishaanza kukosa Radha Haina hata uzuri wowte yaani ,kisa huko chini itaendelea nachokushauri usilete huo mwendelezo badala ya kusema itaendelea andika hata siku mbili au tano kabisa ikisha kamilika ndo uilete hapo hakuna hata Cha kukielewa ,smart people always doing smart thing
mkuu ningekuwa na uwezo huyu kima ningelikwisha mfyekelea mbaliNitakutoa nje sasa hivi choko ww[emoji849][emoji849][emoji849] endelea kuchonga tu....
Tupia nyingine mkuu, tupo hapa wazee wa kasulu, kibondo!MKASA WA PILI -sehemu ya 11
Inaendelea................
Baada ya kuitupa ile line ya simu nilikaa kwa kutulia nikiwaza na kuwazua!," Ina maana kuhangaika kote siku kadhaa za kuitafuta hiyo hela leo hawa majinga wanataka kututoa uhai kisa shilingi 100"?,Nilijisemea!
Basi nilimwambia dogo ahakikishe Anakaa kwa kutulia mpaka hali itakapokuwa shwari maana nilijua wale jamaa wangeendelea kumtafuta pale Bunda hasa ukizingatia mji wenyewe haukuwa mkubwa hivyo!
Kesho yake ilibidi mimi niondoke Pale kwa Mama mdogo kurudi Mwanza maana niliona kila kitu kilikuwa kimeshaharibika!,Nikajisemea ni heri nkaishi masikini kuliko kuendelea kukaa hapo kwa wasiwasi huku maisha yangu yakiwa rehani!
Niliondoka hapo nyumbani Bunda na sikutaka dogo anisindikize maana nilijua anaweza kukamatwa na wale mafia hatimaye mambo yakaharibika!
Niliingia Mwanza mnamo mida ya saa 8 mchana na nilimweleza Bi mkubwa kila tukio lililo kuwa limetokea kwa siku hizo!
Basi kwakuwa siku na kazi ya kufanya kwa wakati huo nilitafuta shule kadhaa pale mjini wa kufundisha tuition,kwa bahati nzuri kuna shule fulani niliipata pale Mjini ambayo nilipewa ajira temporary ya kuwa mwalimu wa History na Geography na nilikuwa nalipwa kila Mwezi 150000/=Nilimshukuru Mungu sana hasa ukizingatia sikuwa na chochote!,Kwahiyo nilikuwa nikitoka kwenye vipindi mchana jioni nilikuwa naenda kuwafundisha wanafunzi niliokuwa nao kwa wakati ule kabla sijaenda Geita na walikuwa wakinilipa 3000 kwa kila topic tunayomaliza!
Baada ya kukaa pale nyumbani kwa muda nilimwambia Bi mkubwa ni wakati sasa na mimi niende kupanga chumba changu ili nijitegemee!,Bi mkubwa alikaataa na akasema nyumba bado ni kubwa na mimi sipaswi kuondoka hapo nyumbani!,Niliona kama Bi mkubwa kanibana maana kuna mitikasi yangu niliona kama haitaenda!,Niliendelea kumsihi Bi mkubwa kwamba ntaenda kupanga ila ntakuwa sikauki pale nyumbani,Baada ya kumsihi sana Bi mkubwa alikubali na akanitaka endapo maisha yakinishinda basi nirudi nyumbani!
Nilikuwa namuhurumia sana Mama yangu kiukweli na nilimpenda sana japo sikuwa na kitu!
Kwakuwa kuna vihela vyangu nilikuwa nimevikusanya kwa wakati huo nilienda kutafuta chumba nkalipia miezi 3 na nkanunua godoro na vyombo kadhaa vya kupikia,nilinunua pia na vitu kadhaa vya ndani na kadri siku zilivyoenda nilipokuwa nikilipwa nilikuwa nikinunua vitu taratibu!
Maisha yalisonga na muda ukayoyoma!,Hatimaye Mungu akasaidia nikauona Mwaka 2011.
Sasa siku moja wakati nikiwa homu Bi mkubwa alinipigia simu akataka niende kule nyumbani maana kuna maongezi!
Basi nkajianda nkasepa zangu mpaka nyumbani,Nilipofika nilimkuta Yule sista mkubwa kaja,Bi mkubwa pia alikuwepo pamoja na wale mabinti waliokuwa wakikaa hapo kwa Bi mkubwa watoto wa Shangazi!
Bi mkubwa alisema ametuita hapo kwasababu kuna jambo kalisikia si zuri!,Nilimuuliza bi mkubwa ni jambo gani hilo?
Ndipo binti mmoja wa Shangazi aliyekuwa mkubwa kuliko yule Mwenzake akawa nasema alikutana na Shemeji yangu mmoja hivi ambaye kwa upande wa Ma sista alikuwa ni wifi yao,kuna maneno aliongea ambayo hayakuwa mazuri!,Yule binti akawa anasema alikutana na Yule shemeji kanisani akawa anamwambia kwamba sisi hapo nyumbani ni Masikini na anajuta hata kaka yao kuuoa hapo nyumbani kwenye ukoo masikini!,Yule shemeji aliendelea kusema kwamba anaogopaga hata kuwapeleka rafiki zake ukweni kwasababu tunanuka umasikini!
Yule Binti akawa anasema tena yule Shemeji alikuwa anasema kwamba hizo taarifa zimfikie mama maana hatuna la kumfanya kwasababu sisi ni masikini wa kutupa,Alikuwa akilaani sana kwanini kaka yake asingeenda kuoa kwenye familia ya kitajiri akaenda kuoa kwetu kwenye familia masikini!
Hayo ndiyo yalikuwa maelezo ya yule Binti mtoto wa Shangazi!
Labda tu niseme hapa kitu ndugu zanguni
Huyu shemeji kaka yake ndo kamuoa dada yetu yule mdogo ambae wanaishi Arusha,Huyu shemeji alikuwa kaajiriwa Benki fulani hapo Mjini na amekaa sana Africa kusini,Kwahiyo hizi mbwembwe zote Alikuwa anazifanya kwakuwa alikuwa na Ajira benki na kukaa tu hapo afrika kusini!.
Baada ya hayo maelezo nilikuwa najiuliza maswali mengi sana,nilikuwa namuuliza mama kwani umasikini ni nini?,Maana sisi kama ni kula mbona tunakula?,kama ni nyumba mbona tuna nyumba?,Huyo malaya anataka maisha gani ?,au kwakuwa yeye ana gari na kufanya kazi benki ndo anadharau watu?
Toka wakati huo nilimwambia Bi mkubwa kwamba sitokaa niimtambue yule Mume wa sista kama shemeji maana dada yake alikuwa akituahibisha na kutusimanga!
Tulipomaliza yale mazungumzo niliondoka zangu pale nyumbani kuelekea Geto kwangu kulala!,Siku hiyo nzima nilikosa raha sana na kutafakari haya maisha,Nilijiona bado nina safari ndefu sana ya kuwa tajiri!
Pale nyumbani kuna jamaa mmoja tulikuwa tumepakana vyumba na alikuwa Rafiki yangu sana maana hata alipokuwa akielekea kwenye shughuli zake ambazo zilimchukua hata mwezi alikuwa akiniachia funguo!
"Mwanangu mbona leo huna raha?,una shida gani"?,Jamaa aliniuliza.
Nilimwambia nilikuwa sijisikii vizuri tu!,Huyu jamaa alikuwa akifanya kazi kampuni ya ujenzi ya Nyanza,Usiku ule nilimfuata jamaa nikamwambia kwa ujasiri mkubwa "NATAKA KUWA TAJIRI",Jamaa alioneshaa kushituka kidogo na kuniuliza "Mwanangu leo umepatwa na nini?,tafadhali nieleze ukweli"
Basi nilimsimulia yaliyonisibu na kiukweli alihuzunika sana na akanambia nisijali niende nikapumzike halafu kesho tutaongea!
Siku iliyofuata baada ya kutoka kwenye shughuli zangu za kushika chaki ilibidi nimueleze jamaa adhma yangu ya kuutafuta utajiri!
Nilimwambia jamaa "Mimi ninachotaka ni utajiri,haijalishi ni utajiri wa namna gani"
Dhumuni la mimi kutaka kuwa tajiri ni kumuonyeshea uwezo yule shemeji yangu na watu wengine waliokuwa wanatuona sisi masikini!,Kiukweli kwa wakati huo nilikuwa tayari kufanya jambo lolote!
Jamaa aliniambia tafuta nauli twende zetu kigoma maana kuna kipindi tulienda kufanya kazi ya ujenzi wa Barabara kule na kuna Bibi tuliwahi kwenda kwake alikuwa ni balaa!,Jamaa akawa anasema kipindi hicho mimi nilienda kwake kufata dawa ya kinga dhidi ya watu wabaya pale kazini hivyo sikufata utajiri,lakini safari hii nataka na mimi nikatafute dawa ya kupanda cheo na kupata pesa!,
Basi hayo mazungumzo ya jamaa yalinipa faraja kidogo nkajiona siko mpweke!
Niliendelea kutafuta pesa za nauli maana jamaa alinambia nikipata kama laki 200000/= nimshitue ili tuondoke maana yeye alikuwa tayari muda wote!
Mwezi uliofata nakumbuka ulikuwa mwezi wa 4 mwaka 2011 sikutaka kumwambia mtu yeyote na sikutaka kumuaga hata Bi mkubwa naelekea wapi!,Mtu aliyekuwa akifahamu ni huyo jamaa tuliyekuwa tukikaa nae hapo nyumbani vyumba jiarani!
Basi tulipanga safari ya kwenda kigoma na tuliondoka Mwanza siku iliyofuata!
Itaendelea..............
kweli kabisa kaka Mkubwa kama unaangalia sinema mimi pia.nitakuwa.tayar kugombana na wale waaribufu wasijee wakutjkosesha.uhondoKwa kweli mleta uzi ana kipaji cha kusimulia story!
Kwa kweli mleta uzi ana kipaji cha kusimulia story!
kweli kabisa kuna mijitu kazi yao ku criticize tu....wewe kama una hadith yako ya ukweli iweke hapa ubaoni...sio kuanza kukosoa tu kila kitu...kuna vitu vya kujifunza humu...ona sasa mdada wa kazi alivyoiletea shida hii familia.Mimi nataka kujua issue ya baiskeli ya mshkaji iliishia wapi.??
Halafu tafadhali acha kuwasikiliza baadhi ya hawa maandazi wa humu, ona kipande cha mwisho kilivyo hakina ladha kama chips zilizolala kisa tu kufupisha story,
LwandaMagere wewe tuwekee details zote ikiwezekana hata ratiba za msosi wa week nzima, tunaotaka tutasoma wasotaka waende jukwaa la siasa, hatuwezi kosa utamu kisa mafurushi machache..!!