chrisbleez
JF-Expert Member
- Dec 28, 2016
- 752
- 1,239
MKASA WA PILI - Sehemu ya 18
Inaendelea.............
Asubuhi kulipokucha nilijianda na nilimuaga Mzee Nchibaronda na kuondoka!
Yule Mzee Nchibaronda nilimwachia shilingi laki moja ile ya kitanzania pamoja na kiasi kidogo nilichokuwa nacho cha faranga!
Mzee usiku alikuwa ameniambia kwamba siku nitakayofanikiwa inabidi nirudi kumpa shukurani maana shukurani huwa ni lazima!
Kwakuwa wakati huo nilikuwa nina uwezo wa ajabu kutokana na ile irizi niliyowekewa mkononi kuna jambo nilifanya pale si la kawaida!,Nilitamka ya kwamba "Ninataka muda huu niwe ziwa Tanganyika",na kweli nilijikuta nipo ziwani kwa upande wa kongo!.
Kiukweli nilijiona kama nina bahati kuliko binadamu wote walioko kwenye hii sayari ya dunia!
Nilitembea hapo ufukweni kuelekea kaskazini mwa Congo na muda si mrefu nilifika pale kwenye Bandari ya Kalemii!,Bado nilikuwa sielewi ule uwezo wa kutembea kwa haraka ulitoka wapi lakini yawezekana ilikuwa ile Irizi ya malikia!
Nilipofika pale Bandarini nilikuta Boti nyingi za kisasa na niliuliza pale boti inaelekea kigoma nikaonyeshwa!,nipofika kwenye hiyo boti nilipanda na kuingia ndani na hakuna aliyeweza kuniuliza kuhusu nauli maana nilikuwa ninatamka tu na inakuwa!
Huu mtindo wa kusafiri bila nauli ndo yalikuwa maisha yangu siku zote tangu nilipotoka huko chini ya maji!
Ile boti haikuchukua muda sana ilianza safari kuelekea kigoma na masaa kadhaa ikawa imetia nanga bandari ya kigoma!
Nilipofika kigoma nilijaribu kumtafuta yule jamaa wa Mwanza kwenye simu lakini alikuwa hapatikani,Baada ya kumkosa jamaa nilijaribu kumtafuta mama na alipopatikana tulisalimiana na akaniambia wao wanaendelea vizuri!,Mama aliniuliza "Kwani ukowapi wewe?,mbona hujaja nyumbani takribani wiki mbili?"
Nilimwambia mama "Nitakuja kesho maana nilikuwa bize kuna kazi nilikuwa naifanya"
Baada ya mazungumzo na mama nilielekea hapo kigoma nikatafuta hotel kwa ajili ya kupata msosi!
Baadae nilitafuta hotel maeneo ya hapo kigoma kwa ajili ya kupumzika ili kesho nianze safari ya kuelekea Mwanza!
Usiku huo nilikuwa nawaza namna nitakavyokuwa tajiri na namna ya kufanya watu wasigundue utajiri wangu kuwa niwa kishirikina!
Kulipokucha Asubuhi nilielekea kupanda basi lililokuwa linaelekea Mwanza na kama kawaida nilipanda bure sikuweza kulipa nauli!
Wakati huo mrume ndago nilikuwa nina jeuri na kiburi kisichokuwa na mfano,maana niliona mimi ndiyo mimi na kwamba hakuna mbwa yeyote wa kunibabaisha!,
Kama kawaida Mwanza tuliingia mida ya usiku!
Nilipofika hapo stendi ya Nyegezi nilipanda bodaboda mpaka Geto kwangu!,Kwakuwa ile nyumba tuliyokuwa tumepanga ilikuwa na geti niligonga na kuna jamaa mmoja alikuja kunifungulia!
"Mwanangu mambo vp",jamaa alinisalimia,nkamwambia" poa kaka"
"Ulikuwa wapi kaka maana nilijaribu kukuulizia lakini kila mtu hakuwa na jibu"jamaa aliendelea kuniuliza!
Nilimwambia "Nilisafiri kidogo kaka,siunajua tena utafutaji?"
Basi nilielekea chumbani kwa yule jamaa ambaye tulienda nae kasulu maana nilikuwa nimempa funguo zangu anitunzie!,Nilijaribu kugonga akafungua lakini ilikuwa sura ngeni machoni kwangu!
Alikuwa mwanamke na mimi nilidhani uenda angekuwa mwanamke wa jamaa lakini kumbe kulikuwa na mpangaji mpya kwenye hicho chumba!
Nilimuuliza "Vp jamaa kalala",Yule dada aliniambia "jamaa yupi"?,Aliendelea kuniambia yeye hapo kahamia ana kama wiki mbili hivi!.
Nilimuomba samahani sana maana nilijua uenda ni mwanamke wa jamaa na nkamwambia hapo mwenye chumba alichohamia kulikuwa na mpangaji ambaye nilimwachia funguo za chumbani kwangu maana mimi nilikuwa nimesafiri!
Yule dada aliniambia nijaribu kuwauliza wapangaji wengine maana yeye hafaamu kitu chochote!
Nilienda kumgongea yule jamaa aliyenifungulia nikijaribu kumuulizia labda jamaa atakuwa kamwachia funguo!,Jamaa akasema "Hapana sikuachiwa funguo"
Kuna jamaa mmoja yeye shughuli zake zilikuwa za viwandani huko Igoma na uenda nadhani jamaa ndo alimwachia funguo!
Niliona isiwe taabu sana!,Nilielekea chumbani kwangu na niligusa kile kitasa kwa mkono wa kushoto ulokuwa na ile irizi na ukafunguka nikaingia ndani!
Kiukweli sikutaka mtu yeyote lile tukio alione na ndo maana nilijaribu kuutafuta ufunguo wangu na kwakuwa ilishakuwa usiku sikuwa na namna ingawa hakuna aliyeona nafanya nini!
Asubuhi jamaa alipokuja kutoka shift huko kiwandani alishangaa kunikuta nafanya usafi ndani kwangu!
"Aisee mambo vp"?,Umerudi lini"?,yalikuwa ni maswali aliyoniuliza,Nilimjibu nimefika jana usiku!
"Ulikuwa na funguo nyingine nini!,maana jamaa aliniachia funguo zako",Nilimwambia "Ndiyo nilikuwa na funguo moja maana hii niliyompa jamaa naiachaga kama dharula"
Nilimuuliza jamaa kahamia wapi?,Jamaa aliniambia Yule mshikaji tuliyeenda naye kasulu kahamia Kahama mkoani shinyanga maana jamaa anasema alimwambia kuna chimbo la dhahabu kalipata hivyo aliona aachane na ile kampuni ya Ujenzi aelekee mgodini kutafuta mali!
Tuliendelea kupiga stori pale na jamaa na akanipatia ule ufunguo wa chumba changu mi nikaendelea na mambo mengine!
Nilipomaliza kufua nguo nilijilaza ndani nikiwa nawaza namna ya kuianza ile kazi maana niliambiwa nijitahidi ndani ya mwezi huo mwishoni damu iwe imepatikana!
Niliamka na kujianda na kuelekea nyumbani kwa Bi mkubwa na nilipitia sokoni nikanunua matunda na vyakula baadhi nikawapelekea!
Nilimkuta Bi mkubwa pale na nikamsalimia na mambo mengine yakaendelea!
Baadae niliwaaga nikaondoka zangu kurejea geto kwangu!
Siku zilizidi kuyoyoma na nilikuwa na wazo sasa la kuanza kazi rasmi!
Kumbuka niliambiwa nihakikishe kuna chumba maalumu nilichokitenga kwa ajili ya kukiweka kile kibuyu alichonipa Mzee Nchibaronda baada ya kufanya tukio na kiwe na damu!
Hiko kibuyu kilikuwa ni kidogo sana kwa muonekano wa kawaida lakini kilikuwa na uwezo wa kujaza damu kama lita 200 kwa wakati mmoja!,Na kwa kawaida ulikuwa huwezi kukinyanyua mpaka uwe na nguvu za ziada kama nilizokuwa nazo mimi!
Baada kama ya siku mbili nakumbuka ilikuwa mida ya saa tatu usiku nilielekea mitaa ya bugando na kuna ajali niliisababisha ya bodaboda ambapo waligongwa na lori mpaka vichwa vikasagika kabisa!,Nilienda pale na kibuyu changu na nikaweka damu yao wote bodaboda na abiria wake na sikubakiza hata tone la damu maana kuna dawa nilichanganya na nilipofika hapo ilivuta damu zote kwenye ile miili hakikubaki kitu!
Tukio hilo nililifanya pasipo kuonekana na mtu yeyote yule!
Wakati nafika Mwanza nilienda kuitafuta ile miti ya dawa na kuivuna na kuihifadhi ndani,pia kuna dawa nyingine nilitoka nazo kongo pia kuna miti ya dawa baadhi nilienda kununua kwenye maduka ya dawa za asili!
Basi baada ya kuwa nimeiweka ile damu kwenye kibuyu nilielekea nyumbani n nilipofika nilikiweka kile kibuyu chini ya uvungu!
Asubuhi nilipoamka nilikiangalia na sikukuta damu yoyote ndani!nikajua tayari wazee wa kazi watakuwa wamekuja wamechukua chakula chao!
Siku hiyo nilisikia sauti ikinielekeza kwamba nielekee maeneo ya Nyegezi maeneo ya hapo stendi kulikuwa na sheli(kituo cha mafuta),Nisingependa kukitaja jina!
Ile sauti iliniambia kwamba nikifika hayo maeneo kuna dada atakuwa kashika hela na nisiwe na wasiwasi nimsalimie kisha atanipa hizo hela !,Niliambiwa yeye atakuwa anaona ameshika hela kumbe kashikilia gunzi la muhindi!
Nilifanya kama nilivyoagizwa,nilipofika nilimsalimia maana nilimfahamu tu kwa kumuona!,Baada ya kumshika mkono na kumsalimia alinipa pesa zote alizokuwa nazo na yeye alikuwa kashika gunzi la muhindi akidhani pesa!
Nilipozihesabu zile hela zilikuwa kama laki tatu na hamsini!
Nikarud zangu geto kwangu!,Nilipofika ndani kwangu pia kuna hela nilizikuta kitandani zilikuwa burungutu zimefungwa na rubber bendi!
Kiukweli nilifurahi sana na nilianza kuzihesabu zilikuwa milioni 2
Itaendelea.....................
Hii story nilivyokuwa na hamu ya kuendelea kuisoma natamani kama ni cd basi ningehakikisha nanunua episode zoooooooote[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]