Mikasa ya ndege kubwa kubwa

Nijuavyo ni kwamba mafuta kwenye ndege huwa ni mzito sana maana hubeba tonnes. Sasa inapo dump inapunguza uzito hata wakati wa kutua iwe nyepesi....isijipige chini pia inapunguza risk ya kulipuka
 
Hii stori tamu.......
 
Nijuavyo ni kwamba mafuta kwenye ndege huwa ni mzito sana maana hubeba tonnes. Sasa inapo dump inapunguza uzito hata wakati wa kutua iwe nyepesi....isijipige chini pia inapunguza risk ya kulipuka
Asante kwa ufafanuzi Mkuu, kuna ndege moja nimeangalia documentary yake this week, Yaani ilitumbukia bahari coz walirudi tu kudump mafuta ili watoe kwa emergence, moto ulianza kuwaka ndani ya cock pit hivyo ukaunguza mfumo mzima wa wiring mpaka dashboard ikazima ikawa haiendesheki tena,

Ila laiti lisingekuwepo zoezi la kudump mafuta nadhani wangeuwahi ule moto. Thus why nimejiuliza sana,
 
Reactions: Ok9


Tatizo nini? Hivi mnajuana ama hamjuani? Nashangaa!.
 
Soma comment yake ya kwanza halafu angalia nilimuambia nini na kajibu nini.


Mimi naona njia nzr ya kumuonyesha mtu mwingine kuwa ni mjinga nikutobishana nae haswa kama haumjuhi na umejaribu kumuelewesha hataki kuelewa. Muache huyo mtu hasiyekuelewa unavyoelewa na mzigo wake kichwani. Hakuna sbabu ya kugombana na mtu usiyemjua. Naamini kukubali kukosolewa ni sehemu ya kujifunza na ni ungwana hakuna binadamu anayejua kila kitu kila mtu anaujinga wake.
 
Napingana na wewe kuhusu hili. Nitaweza kuitolea maelezo kufuatana na ukweli kuhusiana na safari za anga zinazotumika. Kuna aina nyingi zinazowezesha ndege kutua katika kiwanja/viwanja duniani, na hili linategemeana na aina ya kiwanja (matumizi), hali ya hewa wakati wa kutua, aina ya ndege, sheria za nchi zinazoongoza ndege na aina za leseni walizonazo marubani. Sasa inavyoonekana kwa tukio la Ethiopian Arusha, rubani ama aliomba au alilazimika kutumia utaratibu wa VFR(Visual Flight Rules) yaani kuruka kwa kuangalia nje, kama gari ili kuona unapokwenda. Hivyo basi, wakati wa kutua wanaomba kutumia pia Visual approaches (Ushukaji kwa kuangalia kwa macho). Huu huwa ni mawasiliano njia mbili, mwongozaji ndege toka uwanjani na rubani ndani ya ndege.
Tukiangalia ramani ya TZ, kutokea Ethiopia kuingia anga la Tanzania unatokea kaskazini upande wa Kenya. Hapa kwa utaratibu wa kuruka kwa kuangalia(ambao hutumika tu pale hali ya hewa ikiwa shwari Zaidi-isiyo na mawingu mengi),rubani huulizwa kama amekiona kiwanja (barabara ya kurukia) na akisema amekiona basi hupewa ruhusa kutua. Changamoto iliyopo kati ya Arusha na KIA ni kuwa viwanja vyote viwili vina uelekeo sawa 09/27, hii ni kufuatana na nyuzi za uelekeo wa dunia. Yaani barabara za kurukia ndege zinaanzia nyuzi 90, upande mmoja na nyuzi 270 upande wa pili. Hivyo kufanya makosa ya kibinaadam ni rahisi Zaidi hapo.
Ethiopian aliomba kutua KIA kutokea magharibi ya Arusha kwa hiyo alikuwa atue kwenye barabara kutokea nyuzi 270, alipoangalia akiwa ameelekea nyuzi 270 akaona barabara ya Kisongo akasema nimeona akaruhusiwa, akatua. Nadhani umenielewa. Swala na mafuta kwa rubani siyo rahisi kutokea kihivyo ulivyoelezea.
 
Hivi na lile "dege" la Tanzania lililoanguka Moshi Bar Ukonga-Dar eti lilidunguliwa??
 
Hii itabidi niitafute kama ipo youtube.
Nilikiwa na documentary ya boing mpya sijui 747 dash 8 inaonyesha inapaa kwa emergency kwenye uwanja mfupi mpaka mkia umewekewa kubao cha kuburuzia chini. Sasa sijui Hiyo ilishindwaje
 
Mkuu Uko deep sana, but unaposems magharibi mwa Arusha sio upande huu wa serengeti? Na kwa haraka haraka kwa akili yangu nilidhani itakua ilitokea usawa wa Holili.

Halafu unapowasiliana na control tower si anakwambia hii ni control tower ya wapi?

Na kama ndiyo hivyo maana yake ni kwamba hii ndege ilitua pasi na kuwasiliana na control tower ya kisongo kitu ambacho ni hatari coz kama kungekua na ndege nyingine inaruka si singeumana?

Nimewahi kuona documentary moja ndege ziligongana kwenye run way ilikua usiku mmoja hakuwasha taa.
 
Hii itabidi niitafute kama ipo youtube.
Nilikiwa na documentary ya boing mpya sijui 747 dash 8 inaonyesha inapaa kwa emergency kwenye uwanja mfupi mpaka mkia umewekewa kubao cha kuburuzia chini. Sasa sijui Hiyo ilishindwaje
Haikushindwa Mkuu, Ilipaa, yaani ni vile tu runway ilikua fupi kuliko ndege coz ilitua kimakosa, ila yule mjeda aliirusha.
 
Ni kweli kabisa, upande huo huo unaofikiria ni sawa. Kwa kuwa ndege husafiri kwa mwendo wa kasi, na juu sana, huhitaji umbali mrefu kugeuka na kanza kushuka kidogo kidogo huku ikipunguza mwendo. Kama angetokea upande wa Holili KIA angeiona kwanza hivyo isingekuwa tatizo. Mawasiliano kati ya nchi kavu na ndege yanajulikana kwa masafa ya redio, hivyo yanajulikana kwa kuwa ukiweka masafa Fulani ni ya uwanja Fulani kama redio za kawaida Cluods, Radio Uhuru nk. Pamoja na hayo bado atajitambulisha kuwa yeye ni wa KIA na rubani naye atasema jina la mruko wake kwa wakati ule. Kwa hiyo ni kweli yule alikuwa na bahati tu pale Arusha hapakuwa na kizuizi barabarani maana alishuka bila ruhusa. Alikuwa anawasiliana na KIA ila akatua Arusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…