Napingana na wewe kuhusu hili. Nitaweza kuitolea maelezo kufuatana na ukweli kuhusiana na safari za anga zinazotumika. Kuna aina nyingi zinazowezesha ndege kutua katika kiwanja/viwanja duniani, na hili linategemeana na aina ya kiwanja (matumizi), hali ya hewa wakati wa kutua, aina ya ndege, sheria za nchi zinazoongoza ndege na aina za leseni walizonazo marubani. Sasa inavyoonekana kwa tukio la Ethiopian Arusha, rubani ama aliomba au alilazimika kutumia utaratibu wa VFR(Visual Flight Rules) yaani kuruka kwa kuangalia nje, kama gari ili kuona unapokwenda. Hivyo basi, wakati wa kutua wanaomba kutumia pia Visual approaches (Ushukaji kwa kuangalia kwa macho). Huu huwa ni mawasiliano njia mbili, mwongozaji ndege toka uwanjani na rubani ndani ya ndege.
Tukiangalia ramani ya TZ, kutokea Ethiopia kuingia anga la Tanzania unatokea kaskazini upande wa Kenya. Hapa kwa utaratibu wa kuruka kwa kuangalia(ambao hutumika tu pale hali ya hewa ikiwa shwari Zaidi-isiyo na mawingu mengi),rubani huulizwa kama amekiona kiwanja (barabara ya kurukia) na akisema amekiona basi hupewa ruhusa kutua. Changamoto iliyopo kati ya Arusha na KIA ni kuwa viwanja vyote viwili vina uelekeo sawa 09/27, hii ni kufuatana na nyuzi za uelekeo wa dunia. Yaani barabara za kurukia ndege zinaanzia nyuzi 90, upande mmoja na nyuzi 270 upande wa pili. Hivyo kufanya makosa ya kibinaadam ni rahisi Zaidi hapo.
Ethiopian aliomba kutua KIA kutokea magharibi ya Arusha kwa hiyo alikuwa atue kwenye barabara kutokea nyuzi 270, alipoangalia akiwa ameelekea nyuzi 270 akaona barabara ya Kisongo akasema nimeona akaruhusiwa, akatua. Nadhani umenielewa. Swala na mafuta kwa rubani siyo rahisi kutokea kihivyo ulivyoelezea.