Mikasa ya ndege kubwa kubwa

Asante Kiongozi.
 
Subiri baada ya miaka 50 CIA watakapotoa misiri yao utaelewa kila kitu
Unajaribu kusema haikua ni ajali ya kawaida?

But hebu tuyajenge vizuri, kwa technology ilivyokubwa sasa inawezekana ni kweli baada ya kuzima transponder ndege ikapotea kabisa Mkuu?
 
Hebu nisaidie hilo tukio nilitafute vipi u_tube limeandikwa kiswahili au??
 
Hebu nisaidie hilo tukio nilitafute vipi u_tube limeandikwa kiswahili au??
Andika "For the love of avition... Ethiopian airline takeoff-short field.. Boeng 767" utakuja, au check post #63, Kuna link.
 
Asante mkuu kwa kuelezea kitaalam zaidi! Nasi tumepata kitu kwa maelezo yako.
 
Kwa matukio haya bombadia bado ni ndege bora!!
Inategemea na safari Mkuu, acha kufanisha vitu vya ajabu na Boeng, airbus, imagine Concorde ulikua na uwezo wa kuvuka Antlantic for only 3.5hrs, sasa hilo panga boy lilivuka kwa masaa mangapi?
 
Bado sijakuelewa kitu flani, unavosema aliomba kutua kia akitokea magharib mwa arusha sijaelewa hapo maana mimi nilikuwa arusha pale mianzini siku ya tukio la hiyo ndege na tuliiona ikiwa chini sana watu wakawa wanasema inaenda dondoka hiyooo....
Alafu pia kwa jinsi matairi yalivokuwa yamezama kweny ardhi ilikuwa inajionyesha ile ndege ilitua kutokea mashariki mwa arusha kwa jinsi ilivokuwa
 
Wakuu, kinachofanyika katika matatizo kama ya huyo, ni kuwa wanaweka mafuta kidogo tu ya kumfikisha KIA, na wanatoa viti vyote ndani ya ndege kupunguza uzito yanawezekana tu.
 
Mm leo ndio nimeanza kuangalia ile Malaysia airline 370
 
Hizi ndege bwana watu tunazifurahia sana lakini siku ikiwa yako haupatikani hata nyama

Katika pita pita zangu ajali mbaya zaidi ya ndege ni ile ya "Tenerife Airport Disaster" ya 1997 ilitokea wakati wa mwisho kabisa Spain.

Pata picha ile speed ya Runway halafu zitokee ndege mbili zinazokaribina ukubwa zikavaana zaidi ya watu 500+ walipoteza maisha pale pale.

Ndege zote zilikua Boeing 747 moja ikitokea Netherland nyingine ikitokea Los Angeles baadaye chumba cha kuongoza ndege pale Spain kilidai makosa yalikuwa ya marubani wote wawili ila upande wa Los Angels wakakataa na kusema makosa yalikuwa chumba cha kuongoza marubani pale Tenerife.

Baadaye ilibidi nchi zote zitume wapelelezi maalumu wakagundua makosa yalikuwa kwa rubani wa KLM-Boeing 747 ya Netherland ikabidi nchi na shirika hili la ndege liwajibike kuwalipa waliofiwa na waloliojeruhiwa.

Lakini pia ajali hii ilifanya pande zote mbili kukaa na kuangalia upya mifumo ya mawasiliano viwanjani na kuleta mabadiliko makubwa sana katika mawasiliano pamoja na crew za kuongoza ndege kuanzia kwa marubani mpaka viwanjani

natamani sana kuielezea kwa undani hii ajali sema leo weekend inabidi vingine viendelee-wengine wataendelea nilipoishia
 
Hiyo ya ufaransa baada yakupasuka tairi shosti ilitokea kwenye tank la Mafuta lilipo karibu na tairi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…