Mikataba anayoingia Waziri Makamba ina mkono wa mkuu wa nchi? Kwanini hatusikii akiikemea? Wananchi wanabakia kunung'unika Taifa lao kufisadiwa

Tabia hizi za kuropoka ropoka zinaendekezwa na watu waliojipendeza kwa Kiongozi mkuu ambaye naye alipenda sana kusifia.
Ilipotolewa Hoja Bungeni ya kufanya Ukaguzi mahususi juu ya Mikopo ya Awamu wa 5, wapo watu walitoa povu wakidai JPM hakukopa. Yupo Mtangazaji wa Star TV alikuwa analaani Hoja hiyo kwenye Kipindi anachoongoza cha Tuongee Asubuhi.
Naamini kuwa hivi sasa anajutia kauli zake, maana sasa imedhihirika kuwa Awamu ya Tano, kwa miaka 5 tu, ilikopa kuliko Awamu ya 4 kwa miaka 10.
Tena mikopo ya Kibiashara, yenye Riba kubwa sana.
Utawala wa Awamu ya 5 uligubikwa na ghilba nyingi sana
 
Awamu ya tano ilikuwa kama vile inashindana na awamu zilizotangulia. Ni kichekesho fulani ukitafakari kwa undani.

JK ni mtu rahimu sana mwenye kujichanganya na kila aina ya watu, hana makuu. JPM alikuwa tofauti kabisa na JK kihulka, alipenda mashindano na alikuwa na ile roho inayoumia akiona mtu fulani anafanikiwa. Akaipandikiza kwa wasaidizi wake, na unoko ukatawala miaka yake yote ikulu.
 
Angeenda huko germany asingekufa? Au unaataka kusema waliopo Germany wakiugua hawafi?
 
Hilo suala nilishalisema hapa na kuweka taarifa zote za BOT na zingine zote, Magufuli hakukopa zaidi ya kikwete.
Magufuli alikopa sana, Ila si zaidi ya kikwete. Tunaweza kumsema aina ya mikopo aliyokopa na pengine kilichofanyika, Ila sio kusema alikopa zaidi ya kikwete.
 
Mimi sifahamu ila ngoja tu nichokoze mada, Since project inahusisha multinational companies hatuoni kwamba yawezekana moja ya vigezo na mashari yake ni ku-hire "mshauri" kutoka nje? kwa maana nyingine yawezekana ni matakwa ya kimkataba.

Na pili je, mkataba hauelekezi kupatikana kwa m-bia kwa upande wa consultancy ambaye ni mzawa?

Anyways, WanaCCM kwenye huu uzi mmenyukana! 😀
 
Fanya kazi, tafuta hela Acha kulialia

Ova
 
Kwani hujui kwa njni Samia alimuondoa Kalemani? Maana ya kula kwa urefu wa kamba yako hujui maana yake?
 
Uko vizuri mno LNG Lindi ni kitendawili!!!!!
 
Tumeambiwa mzee wa jalalani kazi yake ni ku scan mikataba
 
Kwa namna hiyo bora hao wanasheria wa nje watusimamaie tu kwaenye masilahi ya nishati yetu. Wanasheria wa ndani ni hawa eti Kibatala na Lisu,Malya yaani kesi tu ya kuku hawajawahi kushinda.
Hili linalojadiliwa hapa limekuzidi uwezo.bora ukae kimya kupunguza ujinga wako.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Waende kumuona waziri na atawasikiliza?? Sijui hata kama unaelewa, hapo wametangaza tender na ndani yake kunakua na mtu/watu wanaowalenga(10%) na ndio mwisho wanasema wamepata kampuni fulani kutoka sehemu fulani
Ni mtazamo tu.JUST DO IT then uwe na ushahidi ila usidhanie.
 
Mkuu unaelewa maana ya transaction advisor wa mradi wa kiwango cha LNG ?hivi Tanzania kuna firm ipi yenye commercial laywer ?unafikiri miradi hii ukishakuwa mwanasheria inatosha ?tafadhali pitie website ya Baker Botts,ndio utaelewa hali halisi
Sijakuelewa ishu ni kuwa mwanasheria wa Baker and Botts au vipi? Maana nondo za sheria ni zile zile hapa duniani.
 
Ndege yetu ilipokamatwa huko South Afrika wakati huo, ni wanasheria wa kitanzania walioenda kuitetea. Ingekuwa leo, kungekuwa na mkataba wa kampuni fulani la sheria ambao thamani yake ungekuwa ni zaidi ya thamani ya ndege yenyewe !
 
Dili za rada zimerudi. Usihangaike sana. Angalia CV ya Januari ndo utajua kwamba una mtu au kitu wizarani. Inafikia hatua unaelewa ni kwa nini alipewa wizara kama hiyo kwa uelewa mdogo wa sayansi alionao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…