Mikataba kwa wasaidizi wa kazi za ndani, je ni vigezo gani vinavyozingatia kwa nchi husika kukubali mikataba hiyo?

Mikataba kwa wasaidizi wa kazi za ndani, je ni vigezo gani vinavyozingatia kwa nchi husika kukubali mikataba hiyo?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Nimeuliza swali hili kutokana na kauli ya rais Samia leo kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi.
Kwamba hapa nchini waajiri wengi wa wasaidizi wa kazi za ndani, hawazingatii maslahi ya hao wafanyakazi pamoja na mikataba ya kimailtaifa.

Natamani kujua, hivi kila mkataba ni lazima taifa likubaliane nao hata kama hauendani na mazingira ya nchi husika?
Kwa mfano aliposema kwamba, kama mfanyakazi ana mwenza wake, basi anatakiwa kupewa chumba chake yeye na mwenza wake. Je, uchumi wa watanzania unaendana na mkataba huo?
Ikiwa baadhi ya watumishi wa serikali hawana hata makazi bora, wanapanga chumba na sebule, na anatakiwa kukaa kazini kwa saa 8-9.
Na kwa kuwa ana familia, inabidi atafute msaidizi.
Je, ni lazima kukubali kila mkataba?
 
Yaani housemate awe na mwenza wake hapo kwako 🥺?.
 
Back
Top Bottom