Mikataba minne ya ujenzi wa barabara ya kuanzia Kabingo kwenda mpakani mwa Kigoma na Burundi (Km260) imesainiwa

Wachina wanajenga mpaka marekan boss usipende kuzani kila kitu mtu ataweza tu kisa kapewa kipao mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kulaum embu tuletee uzi unao waongelea Hawa wakandaras wabongo walio pewa tenda la kuziba viraka vya barabara kama huna abar zao fatilia yani badala ya kurekebisha tatizo wao ndio wanaongeza wewe umpe mbongo tenda ilo unatafuta lawama na watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu umu Yan bora tu aiponde serekal haangalii anaongea point au pumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusilaumu sana kwanini hawawezi tuangalie pia viongozi wa nyanja mbalimbali wamewawezesha kwa kiasi gani. Kwa mfano kwenye mada nimetoa wazo la wabunge kukaa chini na kujadili sera, miswada, sheria na kanuni mbalimbali za kuwalinda wazawa ikiwemo kutunga sheria za kuwaadabisha pia wale ambao ni wazembe. Mfano mdogo huwezi kumdai mtoto wako matokeo mazuri kama hujamwezesha wala kumpa malengo ya wewe unataka afanye vizuri kiasi gani. Sasa kwa hapa ndani kwetu wengi wazawa wanaishia kuitwa wezi maana kama wale wenye nafasi za usimamizi kutoka serikali wenye ndio wezi wakubwa hawa wanaotafuta kinjanjaa wao wafanyaje? Utaratibu wenye adabu kubwa uwekwe tuone kweli kama sisi watanzania ni wezi au la.
 
Sio jeshi tu na sio wakandarasi wote! Wapo wakandarasi ambao wanafanya ukandarasi kwakua ni "PASSION" walionayo toka wakiwa watoto. Hao ndio tudeal nao tuwajengee uwezo kama wakandarasi hata 20 hivi nchi nzima wawe na kiwango cha kutafuta zabuni kimataifa japo hata Africa ya kati ya kusini. Sisemi wote waliojiandikisha kuwa wakandarasi ni kweli ni wakandarasi wengine ni watafutaji tu na wafanya biashara basi lakini katika hili kundi lote kuna wale ambao wanatamani kufanya mambo makubwa na kuipa nchi heshima.
 
Mkuu, kitendo cha kampuni ya wazawa kupata tenda ya kujenga kilometa 50 ya barabara inayozungumziwa, ilikuwa ni hatua wezeshi kwa kampuni hiyo ambayo ilibahatika kupata tenda hiyo miaka kama minne iliyopita. Ukipima muda na utendaji kazi wa kampuni hiyo mpaka leo ni chini ya viwango tarajiwa. Naamini kama wangekuwa wamefanya kazi inayoonekana na kwa kazi hiyo kuomba kukopeshwa vitendea kazi benki zingewakopesha tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…