Mikataba ya kazi za Mzee Majuto kupitiwa upya

JOTO LA MOTO

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
758
Reaction score
555
Waziri Mwakyembe amesema hayo bungeni jana, sasa nikajiuliza hivi kama Mtu alishakosea kwenye mikataba itawezekana ku review na kunufaika upya?

Au hao "waliomnyonya" watumie tu uungwana na kumpooza Mzee?
 
Kuna jukumu Serikali wanalikwepa hapa?kupitia mkataba upya haya kama ni wa kinyojaji ni mkataba tayari ushasainiwa na ni maridhiano ya baina za pande mbili, labda kama wataona huo mkataba haukufatwa ama kutekelezwa wanaweza kusaidia.

Lakini kikubwa hapa ni mazingira na mfumo, Je tumewatengenezea mazingira wezeshi na mfumo utakaowafaidisha?

Hii ni biashara tukumbuke, so unaweza kukuta wasanii wetu wanaambulia umaarufu tu, na Copy zinazogongwa ama kuuzwa zikawa hazizidi 500k.

Nadhani tunahitaji mfumo mzuri na mazingira wezeshi, ili filamu ziwe na hadhi, ili kufanya watu wengi kuzipenda, kuwekeza na kununua kazi za wasanii.

Lakini uwekezaji ni mdogo mno, quality ya filamu zetu na za chini mno, na hakuna mazingira bora ya kufanya wasanii wafaidike na kazi zao.

Wenyewe tu hawajitambui.

Nina uhakika kama Kanumba angekuwa hai leo hii Filamu na wasanii wa Filamu wangefaidika na uwekezaji alioanza kuwekeza, pesa yake nyingi ilikuwa kwenye uwekezaji na kuboresha mazingira, kabla ya Matunda yake ndio akatutoka.

Tumuone Dimond kwa wasanii wa Muziki, alimamua kuwekeza kwa gharama kubwa leo hii uwekezaji ule unamlipa na kupelekea kuwafungulia milango wasanii wengine.

Panahitaji mjadala mpana utakaoshirikisha wadau wote wa Sanaa kuweza kuikomboa Sanaa hapa nchini.

Kushughulikia mikataba ya Mzee Majuto na Kanumba sio kutibu tatizo.

Wizara ianze moja ikiwezekana iwapeleke wataalam wake Nigeria kwenda kujifunza, hawa akina Dimond ni wa kuulizwa imekuwaje wamefika hapo walipo.

Hili si kwa Sanaa ya maingizo na mziki peke yake, kwenye ridhaa, mpira wa miguu n.k.

Lazima tutengeneze mazingira na mfumo utakaofanyika wadau wawekeze na wawekezaji wenye uwezo kuja nchini kuwekeza ili kuvuna matunda mazuri na kupata wanariadha, wasanii, wanamuziki na hata wachezaji wazuri.

Wizara wabebe jukumu Lao na si kuwatumia wasanii wetu kwenye kampeni na kuishia kupiga nao picha za Selfie.

Wenzetu imefika kipindi wametenga hadi maeneo kwa ajili ya shughuli za wasanii.
 
Kama nanyonywa kweli kwenye mikataba ni bora Wizara husika ilifuatilie mzee apate haki yake. Ni dhambi kumnyonya mzee wa watu. Majuto ni poa sana alindwe haki zake azipate.
 
Waziri Mwakyembe amesema hayo bungeni jana, sasa nikajiuliza hivi kama Mtu alishakosea kwenye mikataba itawezekana ku review na kunufaika upya?

Au hao "waliomnyonya" watumie tu uungwana na kumpooza Mzee?

Hili ni wazo jema na zuri lakini halitoweza kubadilisha alicho sign mwenyewe na kukikubali labda kama mikataba aliyo nayo ina nafasi ya kupitia upya mkataba...

Halafu sidhani kama mzee Majuto alikuwa ana sign mwenyewe mikataba bila kuwepo na mtu karibu bila shaka kuna dalali katikati na ndiye anaye faidika na hayo matangazo...


Na nina hakika matangazo mengi yanayo onekana kwenye tv ni wazi walishampa chake na alikubali na wakamalizana..........
Tatizo la Majuto lina changiwa na madalali.....

Kujaribu sio mbaya hasa kama hasa kuna watu waliokuwa hajamlipa pesa yake itasaidia kumpa chake lakini kwenye kubadilisha mkataba inaweza kuwa ngumu ....
 
Duh, hapo umetaja copy laki tano, ila nikwambie ndugu kungekuwa na watu makini hata kwa kuuza copy laki moja au mbili Wasanii wangeneemeka sana tu.

Na wala hatuhitaji kwenda Nigeria au wapi, kinachotuangusha ni mikakati ya kibiashara tu, Wasanii wapo tayari na wana majina yanayoweza kufanya biashara.
 
Hicho ndio exactly nilichojaribu kusema.

Mikataba ipo kisheria na sidhani kama dunia ya leo kampuni kubwa zitakuwa zinafanya makosa mepesi, lazima watashikana mashati kisawa sawa.

labda kama watatumia tu uungwana wa kusema ngoja tuongeze, au la kufanya kazi nyingine kwa kuboresha hiyo mikataba.

Any way tungoje tuone watakapofikia.
 
Sure lakini wengi wao hajajitambua/hawajajiweka kibiashara, wanalewa sifa mapema kabla ya kufaidika, umaarufu sio faida ya msanii, lakini pia mazingira ya kutambua kipaji na kukilea kibiashara nayo ni changamoto, hiyo kazi itauzwaje dukani
 
Wasanii hawapeleki mikataba kwa wanasheria kabla ya kusaini wao wanaangalia kilichopo mezani tu
Changamoto za kimaisha na kutokuwa na uhakika wa kesho ndio kunachangia.

Mtu ana madeni lukuki nyumbani na mtaani anawekewa mabunda ya milioni tano mezani, anaona hata hayo makaratasi yao ni kero.
 
Sure lakini wengi wao hajajitambua/hawajajiweka kibiashara, wanalewa sifa mapema kabla ya kufaidika, umaarufu sio faida ya msanii, lakini pia mazingira ya kutambua kipaji na kukilea kibiashara nayo ni changamoto, hiyo kazi itauzwaje dukani
Hizo sifa na umaarufu ni sehemu ya biashara yao pia, Msanii asiyesikika sikika ni vigumu kuvutia mashabiki, ila siongelei kusikia kwa mambo yasiyo maadili.

Ni vigumu kufanya kazi/biashara na Msanii ambaye hatovutia Walaji/mashabiki ili bidhaa yake iuzike.
 
Hao madalali unaowataja Mkuu ndio changamoto kubwa ya nchi hii.

Wapo watu wanaishi kwa migongo ya wenzao, na hao ndio wapo mbele na hata wakati mwingine ndio huwa viongozi.

Hii tabia ya "kufanya dili" imetulemaza sana Wabongo, matokeo yake hata migongo ya wengine ni dili.

Na huwezi kumamini nguvu waliyonayo wanaweza hata kukutishia kuwa "tuone na kipaji chako utaenda wapi" na kweli wewe na kipaji chako ukafa njaa.
 
Wasanii hawapeleki mikataba kwa wanasheria kabla ya kusaini wao wanaangalia kilichopo mezani tu
Pia kinachowamaliza hawa Wasanii ni umimi.

Hawana elimu yoyote ya kufanya kazi zao kiweledi zaidi ya kujigamba tu kuwa wana vipaji.

Wafike mahali waheshimu taaluma zitakazowawezesha wafanye kazi nzuri na waone manufaa ya kazi zao.
 
Pia kinachowamaliza hawa Wasanii ni umimi.

Hawana elimu yoyote ya kufanya kazi zao kiweledi zaidi ya kujigamba tu kuwa wana vipaji.

Wafike mahali waheshimu taaluma zitakazowawezesha wafanye kazi nzuri na waone manufaa ya kazi zao.
Ubunifu pia hawana, ukiangalia Nollywood nyingi ni picha za Hollywood lakini wanaongeza manjonjo ya kiafrika ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…