Mikate bora zaidi Tanzania

Mikate bora zaidi Tanzania

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Katika kula kwangu mikate nchi hii sijawahi kuona Mikate iliyo bora zaidi ya Supa Loaf, Sunkist na ile ya Iringa inayouzwa kwenye magari. Hii mikate inahitaji heshima nchi hii kwa sababu ina hadhi zote za kuitwa mikate, kuanzia ladha, harufu, ujazo sahihi wa unga hadi ulaini.
20240627_090816.jpg
 
View attachment 3027259
Supa loaf is the best.....hana mpinzani.
 
Kuna mgeni nilimpokea kutoka Malawi alishangaa sana kwa nini Watanzania wengi hawali mikate kama kitafunwa cha breakfast

Nikampeleka mgahawa fulani akashangaa watu wanakula mboga asubuhi alipoona wanaagiza chapati na supu na kuna siku alishangaa kuona mtu anakula maandazi na mboga (maharage) asubuhi

Kila jioni ilikuwa lazima arudi na mkate nyumbani kwa ajili ya breakfast

Tanzania ni nchi ambayo mkate sio sehemu kuu ya kiamsha kinywa chetu
 
Kumbe chapati marage ni breakfast..
Mi na jamaa angu ndo chakula chetu cha usiku
 
Usiku baadhi ya mabachelor imekuwa msosi wao huo

Migahawa au baba/mama lishe siku hizi wanauza sana ikifika jioni utaona kimeza na viti, pembeni chapati zinachomwa na maandazi yakikaangwa na jungu la maharage likitokota

Wanetu wakijipatia dinner baada ya kutoka kulijenga taifa
 
Back
Top Bottom