Jamii na maadili yetu yanapotea sana. Kinacho mtokea Hamisa hapa ni kwamba ni fundisho kwa wanawake wote. Ukiona mwanaume ana mwanamke wake ambae anatambulika na huyo mwanaume ana mtambulisha huyo mwanamke wake kama mwenza wake, hata kama hawajafunga ndoa lakini amemtambulisha, wamezaa na wanashirikiana mambo yoote kama bwana na bibi, na wewe unamfahamu huyo mwanamke wake na una urafiki nae, usikae ujiingize kwenye mahusiano na mwanaume huyo, then umzalie mtoto, then uanze vijembe na kumkebehi huyo mwanamke wake. Karma will always find you. Let the man end his relationship na mwanamke wake then aje kwako. Halafu mwanaume anayejua umemkubali na unajua ana mwanamke wake kamwe hatokuheshimu.
Kingine kikubwa, jamani kuna magonjwaaa. Unalala vipi na mwanaume bila kinga na unajua analala na mwanamke wake bila kinga too?